Chadema ilifanya makosa uteuzi wa Wabunge Viti Maalumu 2015

The golden

JF-Expert Member
Sep 11, 2018
1,379
2,553
Moja ya kasoro kubwa tulinayo watanzania tuliowengi ni kwamba hatupendi kukosolewa, zaidi sana hatupendi watu wenye mawazo tofauti na sisi.

Tabia hii tusipoiacha itatutesa sana. Tunapigana na kuumizana kwa sababu hatupendi kukosolewa.

Miongoni mwa Wabunge wa Viti Maalumu walioteuliwa na Chadema mwaka 2015, walikuwa na uwezo mdogo sana, kiasi kwamba mtu ungeweza kushangaa iweje Chama chenye watu wenye akili kama Chadema kilifanya makosa makubwa kiasi hicho.

Nadhani kwa kuwa chama hiki kina watu makini basi naamini watakuwa wamejifunza jambo fulani hivi. Makosa haya hayatajirudia tena.
 
Sugu na Msigwa walimshitaki Salum mwalimu kwa kuuza viti maalum kwa miliono 50 kwa kiti na bao mbili. Mwenyekiti kaizima kesi kwa kuwa Mwalimu ni mtu wake,pengine ametumwa na mwenyekiti
 
Sugu na msigwa walimshitaki Salum mwalimu kwa kuuza viti maalum kwa miliono 50 kwa kiti na bao mbili
Mwenyekiti kaizima kesi kwa kuwa Mwalimu ni mtu wake,pengine ametumwa na mwenyekiti
Umechelewa wapi ndugu? Peleka haraka kwa Ndugai ili muwahi TAKUKURU.
 
kuna baadhi ya wabunge walipelekwa baadhi ya mikoa sijui walipotokea. mfano mtu analetwa Shinyanga hata wenyeji tunajiuliza katokea wapi huyu?atakuwa na impact gani hata kukipromot chama. niliwahi kumtumia sms Mbowe,huu ni ujinga matokea yake mbunge hayupo jimboni miaka yote
 
Moja ya kasoro kubwa tulinayo watanzania tuliowengi ni kwamba hatupendi kukosolewa, zaidi sana hatupendi watu wenye mawazo tofauti na sisi.

Tabia hii tusipoiacha itatutesa sana. Tunapigana na kuumizana kwa sababu hatupendi kukosolewa.

Miongoni mwa wabunge wa viti maalumu walioteuliwa na Chadema mwaka 2015 , walikuwa na uwezo mdogo sana. Kiasi kwamba mtu ungeweza kushangaa iweje Chama chenye watu wenye akili kama Chadema kilifanya makosa makubwa kiasi hicho.

Nadhani kwa kuwa chama hiki kina watu makini basi naamini watakuwa wamejifunza jambo fulani hivi. Makosa haya hayatajirudia tena.
Wanalilia matumbo yao waache waende zao kwanza sikuwasikia hata mara moja.
 
kuna baadhi ya wabunge walipelekwa baadhi ya mikoa sijui walipotokea. mfano mtu analetwa Shinyanga hata wenyeji tunajiuliza katokea wapi huyu?atakuwa na impact gani hata kukipromot chama. niliwahi kumtumia sms Mbowe,huu ni ujinga matokea yake mbunge hayupo jimboni miaka yote
Alikujibuje huyo Mbowe?

Kwani watu wanapopiga kelele kwamba wabunge wa viti maalumu wa chadema wanateuliwa kimkakati wa chakula ya kubwa huwa mnakuwa mmeziba masikio na pamba?
 
Moja ya kasoro kubwa tulinayo watanzania tuliowengi ni kwamba hatupendi kukosolewa, zaidi sana hatupendi watu wenye mawazo tofauti na sisi.

Tabia hii tusipoiacha itatutesa sana. Tunapigana na kuumizana kwa sababu hatupendi kukosolewa.

Miongoni mwa wabunge wa viti maalumu walioteuliwa na Chadema mwaka 2015 , walikuwa na uwezo mdogo sana. Kiasi kwamba mtu ungeweza kushangaa iweje Chama chenye watu wenye akili kama Chadema kilifanya makosa makubwa kiasi hicho.

Nadhani kwa kuwa chama hiki kina watu makini basi naamini watakuwa wamejifunza jambo fulani hivi. Makosa haya hayatajirudia tena.
Anaandika MALISA G. J

Wabunge watatu Chadema, Latifa Chande, Anne Giderya na Dr.Immaculate Sware (wote viti maalum) wamehamia CCM. Hii sio habari. Ni haki yao kuhama na ni jambo lililotarajiwa. Wapo wengine pia watakaoendelea kuhama.
Ila nina hoja mbili kuhusu suala hili;

#Mosi; niliwahi kubishana na viongozi kuhusu hamahama ya wabunge. Wao waliamini wanaohama ni wabunge wa majimbo kwa sababu wameahidiwa kugombea tena kupitia CCM. Hawakuamini mbunge wa viti maalum anaweza kuhama.
Ilifika mahali ikatengenezwa "mentality" kwamba wanawake ni "strong" kuliko wanaume eti kwa sababu wanaume ndio wanaohama.

Mtizamo wangu ulikua tofauti kabisa. Niliamini si kweli kwamba wabunge wanawake ni strong. Isipokua hawakua na alternative.

Mbunge wa viti maalumu akihama anapoteza ubunge wake. Na nafasi yake inajazwa na mtu mwingine kutoka Chadema humohumo. Hii ilifanya wengi wafiche makucha yao. Wakabaki Chadema hata kama mioyo yao ilikua CCM.

Niliwahi kusema hawa tunaowaita "wabunge strong" ipo siku watatuprove wrong. Na ndivyo ilivyotokea. Kwa sasa wamehakikishiwa mafao yao na kulindiwa ubunge wao. Kati ya wabunge 38 viti maalumu watakaobaki ni wachache sana. Hawa ndio mlikua mnawaita strong?

#Pili; ni kuhusu upatikanaji wao. Ukweli ni kwamba "machinery" iliyoteua wabunge viti maalum 2015 ilipwaya sana. Kuna watu walipewa ubunge ambao kimsingi hawakustahili hata kuwa madiwani. Wapo wenye sifa walioachwa wakapewa vihiyo.

Mfano mzuri huyu Anna Gidarya. Mpaka anateuliwa alikua Katibu wa UVCCM Mbulu. Sijui kama unaelewa? Yani akiwa ofisini kwake UVCCM Mbulu, alisikia kwenye radio kwamba ameteuliwa Mbunge viti maalum Chadema. Uteuzi wake uliibua mjadala mkubwa sana. Kivipi kiongozi wa CCM ateuliwe ubunge Chadema? Hakuna majibu ya kuridhisha yaliyotolewa zaidi ya kutakiwa kuheshimu maamuzi ya chama.

Huyu Anna mwaka 2017 aligombea Makamu M/kiti Kanda ya kaskazini. Nilimpinga kwa nguvu zote. Lakini nikambiwa nafanya personal attack. Uchaguzi ukaahirishwa. Uliporudiwa mwaka jana akachaguliwa Mweka hazina. Just imagine?

Tunahitaji reform kubwa, hasa namna ya kurecruit na kupata viongozi wetu. Kuacha watu wenye sifa na kurecruit type za akina "Giderya" ni kukinajisi chama na kuwavunja moyo waTZ wanaotuamini.!
 
Moja ya kasoro kubwa tulinayo watanzania tuliowengi ni kwamba hatupendi kukosolewa, zaidi sana hatupendi watu wenye mawazo tofauti na sisi.

Tabia hii tusipoiacha itatutesa sana. Tunapigana na kuumizana kwa sababu hatupendi kukosolewa.

Miongoni mwa wabunge wa viti maalumu walioteuliwa na Chadema mwaka 2015 , walikuwa na uwezo mdogo sana. Kiasi kwamba mtu ungeweza kushangaa iweje Chama chenye watu wenye akili kama Chadema kilifanya makosa makubwa kiasi hicho.

Nadhani kwa kuwa chama hiki kina watu makini basi naamini watakuwa wamejifunza jambo fulani hivi. Makosa haya hayatajirudia tena.
Hamjui Chadema Inapita kwenye kipindi gani hivi sasa. Siasa za UPINZANI ni ngumu lakini najua yataisha tu haya
 
Ni kweli cdm inapitia kipindi kigumu, lakini kama uteuzi wa viti maalum ulikuwa wenye udhaifu wa hivyo ulitegemea nini?
 
Moja ya kasoro kubwa tulinayo watanzania tuliowengi ni kwamba hatupendi kukosolewa, zaidi sana hatupendi watu wenye mawazo tofauti na sisi.

Tabia hii tusipoiacha itatutesa sana. Tunapigana na kuumizana kwa sababu hatupendi kukosolewa.

Miongoni mwa wabunge wa viti maalumu walioteuliwa na Chadema mwaka 2015 , walikuwa na uwezo mdogo sana. Kiasi kwamba mtu ungeweza kushangaa iweje Chama chenye watu wenye akili kama Chadema kilifanya makosa makubwa kiasi hicho.

Nadhani kwa kuwa chama hiki kina watu makini basi naamini watakuwa wamejifunza jambo fulani hivi. Makosa haya hayatajirudia tena.
Mkuu umesikika na hoja yako itafanyiwa kazi
 
2 Reactions
Reply
Back
Top Bottom