CHADEMA ili mchukue nchi 2015 zingatieni haya | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

CHADEMA ili mchukue nchi 2015 zingatieni haya

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by mambomoto, Jan 19, 2012.

 1. m

  mambomoto JF-Expert Member

  #1
  Jan 19, 2012
  Joined: May 10, 2011
  Messages: 327
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 35
  1. Mshikamano ndani ya chama ni muhimu, Migogoro mwiko. Matatizo yamalizwe ndani ya chama na pale mtu yeyote anakwenda kinyume na malengo na katiba ya chama muondoeni bila kujali hadhi yake. Hakuna aliye juu ya chama
  2. Elimu zaidi ya uraia kwa wananchi hasa wale wa pembezoni
  3. Ni vizuri mkawa na mtandao wa mawasiliano mfano redio au TV ili kuwafikia watu wengi zaidi kwa muda mfupi.
  4. Kuweni makini na propaganda za udini, ukabila na ukanda zinazoenezwa na maadui wa demokrasia Tz.
  5. Lazima muwe na watu makini katika mambo makini, wenye uwezo wa kufikiri kwa marefu na mapana kwa uhakika. Vilaza wa kutoa majibu mepesi kwa mambo muhimu
  6. Vita dhidi ya rushwa na ufisadi lazima iwe endelevu katika kufichua bila woga
  7. Mambo yanayohusu maslahi ya umma lazima yawe ndiyo kipaumbele kwenu
  8. Lazima mtambue kuwa muda uliobaki kufikia 2015 ni mfupi sana hivyo ni lazima mujipange vizuri ikiwa ni pamoja na kupata usimamizi wa dhati na uwakilishi majimbo yote TZ. Hii ni pamoja na kuwa na mawakala wa kuaminika
  9. Mtambue JINAMIZI la CCM ni kama nyani mzee asiyeishiwa na mbinu. Hivyo watatumia mbinu mbali mbali kuwavurugeni ikiwa ni pamoja na kuwaletea mamluki kama mzee wetu .........Maswa
  10. wadau mnaweza kuendelea.........................................
   
 2. m

  mariantonia Senior Member

  #2
  Jan 19, 2012
  Joined: Jan 6, 2012
  Messages: 135
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  ili cdm ichukue nchi inabidi ugumu wa maisha uzidi maradufu manake wanawake ndio wapiga kura wengi wa ccm ilihali wao ni waadhirika wakubwa wa ubaya wa uchumi
   
 3. 1800

  1800 JF-Expert Member

  #3
  Jan 19, 2012
  Joined: Dec 27, 2010
  Messages: 2,217
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 135
  Nakubaliana na mleta uzi kwa asilimia zote,cha ajabu watu waliotharika na sera mbovu za kuinua uchumi,na waliokosa elimu ndio washabaki wakuu wa magamba,last week nilikua kanda ya kati hapa,kuna watu nikawa najaribu kuwapa somo yaani mpaka nilitamani kulia,watu hawaelewi kabisa kua rasilimali na kodi zinatakiwa zitumike kwa ajili ya unafuu wao!kazi bado ni kubwa,elimu ya uraia inatakiwa sana!kweli ukitaka uwatawale milele basi walishe ujinga
   
 4. Kaliua urambo

  Kaliua urambo JF-Expert Member

  #4
  Jan 19, 2012
  Joined: Apr 21, 2009
  Messages: 606
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  11.kufungua ofisi wilayani,tarafani,katani,mpaka vijijini,kazi sana kushinda wakati huna watu vijijini ,unaonekana wakati wa uchaguzi tu ,Igunga tawi lilifunguliwa wakati wa uchaguzi mdogo,inatakiwa kipaumbele kiwe kwenye ofisi/matawi sasa
   
 5. RICH OIL SHEIKH

  RICH OIL SHEIKH JF-Expert Member

  #5
  Jan 19, 2012
  Joined: Jan 2, 2012
  Messages: 882
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0

  Utata na mvurugano utaanzia pale kamanda SHIBUDA atakapotaka kupambana na KIBABU PADRE katika kugombea urais. Kamanda SHIBUDA ameshaprove numerous times kama yeye ni mkubwa kuliko CDM kwani ameshapingana hadi na sera/misimamo muhimu ya chama lakini wote wameufyata wameenda kuwatimua madiwani wa machalii zetu.
   
 6. mchambuzixx

  mchambuzixx JF-Expert Member

  #6
  Feb 7, 2012
  Joined: Nov 11, 2011
  Messages: 1,294
  Likes Received: 77
  Trophy Points: 145
  First
  nimekuwa nikijiuliza sana kwa kuwa chadema imeshindwa kufungua matawi kila kata basi hiki chama kingeanzisha utaratibu wa kuwa na makamanda wawili wa kila mtaa na wawe wanatambulika na chama kitaifa,mkoa,wilaya na kijiji na uanzishwe utaratibu wa viongozi kwenda kuwasimika makamanda hawa katika kila kona ya nchi na kazi yao kubwa iwe kupeleka elimu ya uraia kwa mtaa anaoishi na hawa wawe wanapewa majukumu yote kwa mtaa husika zikiwemo kadi na vitu vingine hii itasaidia kupunguza wimbi la ccm kurubuni viongozi wa chadema na kuwanunua sababu kutakuwa na mtandao mkubwa wa viongozi wa chadema na hapa itakuwa rahisi kupata viongozi wa kata/wilaya/mkoa au kijiji na pia uwekwe utaratibu wa makamanda hawa wawekwe kwenye website pamoja na information zao, kufanya watu wa makao makuu kuwasiliana nao moja kwa moja either kwa kutumia email au simu pia watumike kuchukua matatizo ya mtaa husika kuwasilisha kwenye ofisi ya kata/kijiji/wilaya/mkoa

  second
  kwa kufanya hivyo chama kitajenga mtandao ulionea nchi nzima bila kutumia gharama kubwa na litengwe fungu maalumu ambalo sio kubwa sana litumike kuwawezesha hawa makamanda liwe tofauti na lile la wilaya au mkoa hapa hakuna haja ya kufungua matawi bendera tu inatosha nikiweka kwenye chumba au nyumba, kwamba killa habari inayohusu chama kwenye ule mtaa itapatikana kwa makamanda hawa operation zao ziwe tofauti na zile za wilaya na mkoa na kazi ya kuwasimika hawa ifanywe na bavicha makao makuu wapite kila mkoa,wilaya,kata na kijiji ili kuwe na mtandao mkubwa nchini utakaowachanganya sana ccm washindwe kujua yupi wa kumnunua..hapa tupunguze kidogo habari za maandamano tutumie mwaka mmoja kujenga hiki chama na hapa ndo tutaona watu wanaokitumikia chama na wale vibaraka

  peoplesssssss powerrrrrrrrrr
   
 7. g

  goldernboy New Member

  #7
  Feb 7, 2012
  Joined: Feb 1, 2012
  Messages: 4
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  4 real nmeipenda comment yako, kazi kwa viongozi wa CHADEMA kwa hili kulifanyia kazi
   
 8. mshana org

  mshana org JF-Expert Member

  #8
  Feb 7, 2012
  Joined: Jan 28, 2012
  Messages: 2,102
  Likes Received: 99
  Trophy Points: 145
  nimeipenda
   
 9. Ringo Edmund

  Ringo Edmund JF-Expert Member

  #9
  Feb 7, 2012
  Joined: May 10, 2010
  Messages: 4,895
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 0
  kazi ianze mara moja.
   
 10. m

  mwakipwete New Member

  #10
  Feb 7, 2012
  Joined: Jan 25, 2012
  Messages: 1
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  kwa mpango huu, kama utakamilika, vijijini kote tutatisha
   
 11. kingxvi

  kingxvi JF-Expert Member

  #11
  Feb 7, 2012
  Joined: Feb 11, 2011
  Messages: 883
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  mnatujazia server tu kwani chadema hujui ofisi zao zilipo?
  Au ungemuinbox padri slaa
   
 12. m

  mtengwa JF-Expert Member

  #12
  Feb 7, 2012
  Joined: Aug 20, 2011
  Messages: 1,745
  Likes Received: 225
  Trophy Points: 160
  Naunga mkono
   
 13. C

  Curriculum Specialist JF-Expert Member

  #13
  Feb 7, 2012
  Joined: Oct 8, 2007
  Messages: 2,736
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Ushauri ni mzuri kabisa, lakini hautofautiani sana na utaratibu wa kikatiba wa Chadema wa kuwa na viongozi kwenye ngazi ya msingi, tawi na kata kwa nchi nzima, na mwaka huu ni wa uchaguzi kwa ngazi zote za chama, tumia muda huu pia kuhakikisha kata yako na tawi lako la chadema lina uongozi, ratiba itatangazwa soon. Ushauri ambao ninataka kuupigia mstari zaidi ni ule wa viongozi wa vijana taifa, na wakurugenzi kwenda kuwasimika viongozi hawa watakaochaguliwa kila kona ya nchi, mwaka mzima utumike kujenga chama, hatufanyi maandamano this time ni mikutano ya hadhara, ndani, na kufungua misingi na matawi nchi nzima! 2013, ni maandamano na mikutano ya hadhara nchi nzima, 2014 ni uchaguzi wa serikali za mitaa, 2015 ni safari kuelekea Magogoni! peeople's.....
   
 14. RICH OIL SHEIKH

  RICH OIL SHEIKH JF-Expert Member

  #14
  Feb 7, 2012
  Joined: Jan 2, 2012
  Messages: 882
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0

  Hii itafanikiwa kaskazini mwa nchi tu
   
 15. Bra-joe

  Bra-joe JF-Expert Member

  #15
  May 22, 2012
  Joined: Apr 2, 2012
  Messages: 1,559
  Likes Received: 510
  Trophy Points: 280
  Chadema kwa sasa ndiyo tumaini la ukombozi kwa watanzania wengi na kinakua kwa kasi ya ajabu, hivyo basi ccm wanatafuta mbinu za kukisambaratisha. Ushauri wangu: 1. Tumtangulize MUNGU katika kila jambo. 2. Katika kila mkutano kuwe na watu maalumu walioandaliwa kuongea, wangine watambulishwe tu. 3. Akipokewa kiongozi kutoka ccm asipewe madaraka yoyote ndani ya chama hata ktk ngazi ya kata kwa muda wa miaka5. 4. Katika mikutano kusiwe na kauli zozote za kikanda, kikabila, kitabaka au kidini, kuwe na kauli za kisisasa tu. 5. Kiongozi anapokosea viongozi wengine wasimkosoe kwa kauli zao binafsi, bali akosolewe au kuadhibiwa kupitia vikao halali vya Chama. 5. Viongozi au wanachama tunapoonewa na serikali au taasisi zake tusilete vurugu bali tuwasubiri kwenye kupiga kura tuwapige chini vibaya. Chama/wanachama tukizingatia hayo, hakuna kitu kitaweza sambaratisha Chadema. Long live Chadema.
   
 16. STK ONE

  STK ONE JF-Expert Member

  #16
  May 22, 2012
  Joined: Dec 31, 2011
  Messages: 628
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Nzuri....bila shaka wahusika wanapita humu na ni matumaini yangu kuwa watayafanyia kazi!!!!
   
 17. P

  Precise Pangolin JF-Expert Member

  #17
  May 22, 2012
  Joined: Jan 4, 2012
  Messages: 12,199
  Likes Received: 1,978
  Trophy Points: 280
  Mkuu Nakubaliana na wewe asilimia 90 lakini kwenye sanduku la kura mbona tunashinda sana lakini tunaibiwa sana . Toa ufafanuzi jinsi ya kulinda kura acha longolongo
   
 18. Bra-joe

  Bra-joe JF-Expert Member

  #18
  May 22, 2012
  Joined: Apr 2, 2012
  Messages: 1,559
  Likes Received: 510
  Trophy Points: 280
  walikuwa wanaiba kura kwa kuwa walikuwa wanapata kidogo, halafu wanajazia na za wizi, lkn kwa hali ya sasa hawapati hata kidogo, kwahiyo hawataweza kuiba za kujazia. Mfano, ubunge Shy mjini, walishindwa kwa kiasi kidogo ndiyo maana ikawa rahisi kwao kuiba.
   
 19. mayane

  mayane Member

  #19
  May 22, 2012
  Joined: Apr 17, 2012
  Messages: 27
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 3
  Sawa bra jo together we can
   
 20. SONGOKA

  SONGOKA JF-Expert Member

  #20
  May 22, 2012
  Joined: Mar 8, 2012
  Messages: 1,710
  Likes Received: 877
  Trophy Points: 280
  no 2 muhimu sana mkuu,lately vijana wetu wamekua wanatoa statement zinazotupa wakati mgumu sana kuzitolea ufafanuzi
   
Loading...