CHADEMA ikitwaa Madaraka 2025, nitapendekeza Byakanwa avuliwe Ubalozi, hana sifa hiyo

Erythrocyte

JF-Expert Member
Nov 6, 2012
117,660
218,148
Tumekwishaandika humu mara kadhaa kwamba wale wote waliosababisha uchafu kwenye nchi hii hawapaswi kuwa Mabalozi, Hii ni kwa sababu Balozi ni Mwakilishi wa Nchi yetu kwenye mataifa mengine, yaani Balozi ndio Taswira ya Nchi yetu kule Ugenini.

Mtu kama Gellasius Byakanwa, mtu mwenye roho mbaya na msiginaji mkubwa wa Katiba ya nchi hapaswi kuwa mwakilishi wa Tanzania popote, Uchafu alioutenda mtu huyu wakati wa awamu ya 5 hakuna aliyeusahau, huyu kuwa Taswira ya Tanzania Ugenini ni Aibu kwa nchi yetu, hapa Mamlaka ya Uteuzi imeteleza au imewadharau wananchi wa Tanzania kutokana na Kiburi cha madaraka.

Wakati wa uteuzi kama huu wa Humphrey Polepole niliweka andiko lenye kila ushahidi kwamba mtu yule hakupaswa kuwa balozi, na leo narudia tena kwa huyu Byakanwa, uteuzi huu unadhalilisha nchi.

Serikali iache kuwadharau raia wake kwa kuwateulia watu wasio na maadili yoyote, kwa vile raia hawana la kuwafanya, ikumbuke kwamba yupo Mungu ambaye hajawahi kukubali Ujinga.
 
Hivi nini kimelipata Taifa letu?

No vetting, no accountability - ni kama mfumo na taasisi zetu zimezidi kuwa dhaifu kwenye mambo muhimu......yaani kifupi hatuko serious hata kidogo kwenye mambo muhimu. Diplomacy ni uwanja mkubwa na muhimu kwa mustakabali wa nchi na taifa lolote. Kwa nini hatuonyeshi kujali?

Vyeo vimekuwa kama zawadi tu "apendavyo Rais". HAPANA!
Na tatizo hili tatizo liliota mizizi hasa kuanzia awamu ya nne, ya tano likaongezeka na limekuwa kubwa mno. HAPANA.
 
Ubarikiwe sana
 
Imeandikwa katika Biblia takatifu, kitabu Cha Mithali 14:34
Haki huinua Taifa na dhambi huliangamiza Taifa
 
....mtu mwenye roho mbaya na msiginaji mkubwa wa Katiba....
Hivi Kuna kijana aliyekuwa na roho mbaya kama yule aliyekuwa anatembea na sumu Mkononi ( hatujasahau), hivi Kuna mwenyewe roho mbaya kama aliyetishia watu kuwa kugombea nafasi Fulani ndani ya Chama Fulani ni sawa na kuonja sumu kwa ulimi??

Au roho mbaya hujui maana yake??
===
Yaani kushughulikia wale waliokuwa wanaendesha genge la kuhujumu Uchumi ndiyo Roho mbaya??
 
Back
Top Bottom