CHADEMA ikifa Watanzania WATAINGIA MSITUNI...

CHADEMA ikifa Watanzania WATAINGIA MSITUNI...

Mleta uzi umejitahidi sana!!! Chadema ndio mkombozi wa Nchi hii kama haotakuwepo lazima wapenda haki na wananchi kwa ujumla watatafuta njia mbadala ya kuwaondoa mafisadi!!!....
 
Na jinsi wabunge wa cdm wanavyo penda kula bata sijui kama watamaliza wiki mbili kichakani. Nassari alipigwa kofi moja tu mpaka akalazwa. Tumeona sugu alivyo bebwa kama gunia la mahindi. Hao ndio makamanda.
jifunze kutumia lugha nzuri na kuchangia mada kwa ustaraabu pasipo kutaja majina ya watu
 
Ningeshangaa ungeandika point, kwani ulichoandika na JINA LAKO VINALINGANA na kwa kusema ukweli umejitahidi- umepata 63.2223%.Anyway kwa wale wenye akili timamu mnaweza kuuwekea irabu huo ujumbe. Kifupi, hata CHADEMA ikifa basi itakuwa imejimaliza yenyewe. Mifano:
  1. 1. Kura zimepigwa bungeni(kwa maombi yao) wakashindwa hawakutaka kukubali, wakabebwa juu juu na walinzi wa bunge imekuwa skendo. Ni nani hapo mjinga?
  2. Miezi kadhaa iliyopita wametoa hoja ya kuanzisha JESHI LAO, nje ya kanuni na sheria za JMT. Wanafikiri watanzania watawasamehe? Adhabu yake watanzania watakisusia CHAMA_ NDio kifo chake.
  3. Wanashawishi kuleta vurugu huko Kilimanjaro, ikiwa na pamoja na kuhusika na mauaji ya watu wasiowataka kwa kisingizio kuwa serikali au ccm ndio wahusika
  4. Walisusia bunge na kutoa tamko kuwa nchi hii haitatawalika-Hapo tuliwaweka ktk kitabu cheusi.
  5. Wanamalumbano kibao ktk chama chao juu ya nani agombee Uraisi-2015 mpaka wanataka kutoana koo- Hapo kuna chama tena
  6. Na........Na..........kibao naona niachie hapa.
Wajameni hiki sio chama ni NGO ya watu.......acha kife tu.

Hiki si chama cha kwanza kufa wala si cha mwisho.
 
KATIKA HARAKATI HIZI ZA kisiasa watu wamekubali kujiunga na vyama vya siasa ili kufuata utaratibu wa kidemokrasia wa kubadilisha utawala. Wasiwasi wangu ni kuwa kama hzi harakati za kutaka kukiuwa chama hiki zitafanikiwa basi ni wazi kuwa watanzania wengi hawatataka tena kupoteza muda kwenye siasa ili kubadilisha utawala. Watanzania watajiunga au wataunda jeshi ili kuiondoa serikali iliyopo madarakani. hii ni kwa kuwa watakuwa wameona kuwa hamna haja tena ya kujishughulisha na siasa wakati wanaona bado kuna uhuni unafanyika katika nchi yao.
hili linaweza kuingiza nchi katika machafuko...na kama viongozi waliopo madarakani hawatakuwa na nia thabiti, nia njema kwa nchi hii basi waendelee na hii mikakati ya kutaka kuzima vyama vya upinzan ambavyo vinaonekana kukubalika kwa wananchi. kwa hatua ambayo watu wamefika kwa sasa ni wazi kuna watanzania ambao wapo tayari kabisa kujiunga na jeshi la uasi kama itatokea. tumeona matokeo katika mambo mbalimbali ambayo wananchi wamejitolea kupigwa mabomu , kupigwa,kuteswa na hata kuuawa. waswas wangu je wakiambiwa tukiingie msituni kudai haki hawatakubali?

Watanzania waingie msituni kutafuta Nini, labda kuni. Unadanganyika wewe. Usidanganyike ila unaweza kujidanganya.
 
Chadema wasiwachukulie WaTZ kama wanakubaliana na uongo wao. Kuna Chama kilianza kuonyesha kuwa cha kupenda mambo ya ushari shari, kiliishia wapi. Chadema kama mnadhani ushari utawasaidia mnajidanganya mtatupwa pembeni na WaTZ.take care.
 
KATIKA HARAKATI HIZI ZA kisiasa watu wamekubali kujiunga na vyama vya siasa ili kufuata utaratibu wa kidemokrasia wa kubadilisha utawala. Wasiwasi wangu ni kuwa kama hzi harakati za kutaka kukiuwa chama hiki zitafanikiwa basi ni wazi kuwa watanzania wengi hawatataka tena kupoteza muda kwenye siasa ili kubadilisha utawala. Watanzania watajiunga au wataunda jeshi ili kuiondoa serikali iliyopo madarakani. hii ni kwa kuwa watakuwa wameona kuwa hamna haja tena ya kujishughulisha na siasa wakati wanaona bado kuna uhuni unafanyika katika nchi yao.
hili linaweza kuingiza nchi katika machafuko...na kama viongozi waliopo madarakani hawatakuwa na nia thabiti, nia njema kwa nchi hii basi waendelee na hii mikakati ya kutaka kuzima vyama vya upinzan ambavyo vinaonekana kukubalika kwa wananchi. kwa hatua ambayo watu wamefika kwa sasa ni wazi kuna watanzania ambao wapo tayari kabisa kujiunga na jeshi la uasi kama itatokea. tumeona matokeo katika mambo mbalimbali ambayo wananchi wamejitolea kupigwa mabomu , kupigwa,kuteswa na hata kuuawa. waswas wangu je wakiambiwa tukiingie msituni kudai haki hawatakubali?

Nenda taratibu unaijua historia ya CHADEMA? kilianza kwa nguvu NCCR ilipokuja na mrema CHADEMA kilikuwa kiko kimekufa.NCCR ndio kilikuwa chenye nguvu watu wakaapa kama unavyoapa wewe kuwa NCCR ikifa na mrema asiposhinda uraisi wanaingia msituni.Yaliyotokea baadaye tunayaona Mrema yuko hoi kisiasa na NCCR hoi.

Akaja Kikwete CHADEMA kikafufuka kutoka umauti kikapata nguvu sababu raisi Kikwete mvumilivu tofauti na waliomtangulia kina nguvu maeneo ya mijini hasa majiji makuu yenye wafanyabiashara wa kati kama Arusha,Mwanza,Dar esalaam,Mbeya kwenye mrundikano wa wafanyabiashara wa mikoa ya kaskazini ya nchi.Kila panapokuwa na mrundikano wa wafanyabiashara wa mikoa ya kaskazini unakuta CHADEMA imestawi hapo na matawi yapo.Lakini maeneo mengine shughuli bado pevu.Hivyo kikishindwa hata 2015 usishangae bado mtandao haujakaa vizuri kufikia ile asilimia 85 ya wapiga kura walioko vijijini na kigingi kingine kiko Zanzibar kule mtandao wa wafanyabiashara wa kaskazini ni mdogo mno hivyo matawi kule machache mno na kura 2015 ina maana CHADEMA zanzibar isahau.Hivyo mgombea uraisi wa CHADEMA kushinda Zanzibar ni hakuna na ndio maana CHADEMA wangependa kuwe na serikali tatu wabaki wagombee huku bara tu maana zanzibar ngoma nzito kupata kura za uraisi kule lakini hata bara ngoma nzito sehemu ambako mtandao wa CHADEMA mdogo hasa vijijini.

Kwa sasa fikiria tu kazi ya kujenga chama kazi bado kubwa mno wanachama waliopo CHADEMA wachache na wapiga kura ni wachache zaidi.Hizo za kuingia msituni sahau kwanza walishindwa NCCR,WAKASHINDWA CUF WEWE HUWEZI.
 
NI mhhimu kupigani a nchi yetu maana ndiyo inatupatia maisha zaidi ya chama cha kifisadi kwa hiyo kama 2015 watachakachua, tutawapopoa mawe kama vianbaka wa mitaani, nchi hii si kwaajili ya magamba, ..nzuri sana watu wameamka wakipewa pesa chafu wanatia ndani na kura hawatoi, labda majaribu mtindo wa kupiga mabomu kwenye mikutano...lakinini wazi sana ukombozi umefika. nchi sasa itasafishwa, biashara wa sembe itakuwa history!
 
KATIKA HARAKATI HIZI ZA kisiasa watu wamekubali kujiunga na vyama vya siasa ili kufuata utaratibu wa kidemokrasia wa kubadilisha utawala. Wasiwasi wangu ni kuwa kama hzi harakati za kutaka kukiuwa chama hiki zitafanikiwa basi ni wazi kuwa watanzania wengi hawatataka tena kupoteza muda kwenye siasa ili kubadilisha utawala. Watanzania watajiunga au wataunda jeshi ili kuiondoa serikali iliyopo madarakani. hii ni kwa kuwa watakuwa wameona kuwa hamna haja tena ya kujishughulisha na siasa wakati wanaona bado kuna uhuni unafanyika katika nchi yao.
hili linaweza kuingiza nchi katika machafuko...na kama viongozi waliopo madarakani hawatakuwa na nia thabiti, nia njema kwa nchi hii basi waendelee na hii mikakati ya kutaka kuzima vyama vya upinzan ambavyo vinaonekana kukubalika kwa wananchi. kwa hatua ambayo watu wamefika kwa sasa ni wazi kuna watanzania ambao wapo tayari kabisa kujiunga na jeshi la uasi kama itatokea. tumeona matokeo katika mambo mbalimbali ambayo wananchi wamejitolea kupigwa mabomu , kupigwa,kuteswa na hata kuuawa. waswas wangu je wakiambiwa tukiingie msituni kudai haki hawatakubali?

Jina lako linajitosheleza... Msituni kufanya nini? Ushaona dalili za chama kufa eeeh! Na kitakufa tu Chama hakina hata sera...
 
Back
Top Bottom