Rogate
JF-Expert Member
- Sep 29, 2010
- 215
- 45
Niukweli uliowazi kuwa ccm haikotayari kutoka madarakani kwa kura peke yake. Ukweli huu umedhihirika zaidi ya mara moja kwa matukio ya kushambulia watu na vyama vilivyokuwa mstari wa mbele kuipinga serikali au kutishia kuitoa madarakani mifano hai ni Mrema enzi za NCCR-Mageuzi, CUF enzi za ngangari na sasa CHADEMA.
Vyama hivi vyote vilikutana na vitisho vipigo na hujuma mbalimbali zilizifanikiwa kuviondoa kabisa au kupunguza chachu yake kwa jamii.
Nataka kusema CCM imekomaa kwa michezo ya aina hiyo (good experience in dirty games) hivyo yeyote atakayeingia kwenye ngoma hiyo sio rahisi kushinda. Niwazi kuwa CCM inashambulia wapinzani kwasababu moja ya kubwa ambayo ni kuwapa wananchi taarifa za jinsi serikali inavyotakiwa kuwajibika kwa wananchi na mapungufu ya serikali na viongozi wake.
CCM haipo tayari kuona mapungufu ya serikali inayoiongoza yanajulika na wanachi walio wengi. Mhanga mkuu wa vitisho,vipigo na hujuma kwa sasa CHADEMA inapaswa kuongeza nguvu kwa kuwafikia wananchi walio wengi zaidi. Ndio wataendelea kutishiwa,kupigwa,kushambuliwa na hata kuuliwa, katu wasirudi nyuma mpaka kieleweke na kitaeleweka.
CHADEMA isiache kuwekeza kwa kuwafikia wananchi wengi, chonde chonde CHADEMA isiwekeze kujilinda ikasahau mikakati ya kuwafikia wananchi katika kata, vitongoji na vijijini.
M4C ndio inayotishia uhai wa CCM na hii ndio chanzo cha vipigo nk. CHADEMA ikicheza ngoma ya CCM hakika tutarudi kwenye historia ya NCCR na CUF.