CHADEMA Igharamie uchunguzi Binafsi Kuhusu Clip ya video iliyotolewa

ninvyoamini mm humu jf walio wengi ni wasomi na waelewa sana tena wa hali ya juu. sasa inapotokea issue kama hii ya lwakatare na watu wamejitokeza wengfi tuu kuueleza umma hapa jf kasoro kadha wa kadha kuhusu ile video clip na kuwalete baadhi ta clips ambazo zimeingizwa maneno ili kuwaonyeha watu kuwa teknolojia hiyo ipo na wala tusi jiaminishe asilimia mia kuwa ni kweli. lkn inaonekana hata members ambao wanauelewa juu ya uwapo wa hii teknolojia wanabisha na kukataa kabisa kana kwamba uwezekano wa kutengeneza video ile haupo sasa je wananchi wa kawaida ambao uelewa hawana itakuwaje? kumbe tz tumeathiriwa na mfumo wa chama kimoja tu na ndio maana mambo hayaendi. wanapotokea wanamageuzi basi hufanyiwa kila njama kuwadhoofisha badala ya kuudhihirishia umma kwa kutekeleza ilani za chama (ccm). maskini tanzania.
 
Tunataka majibu sahihi kwann kiongozi mkuu wa chama anajihusisha na vitendo vya kigaidi?
 
Tunachotakiwa kujiuliza kwa nini Lwakatare hajaachiwa hadi sasa hivi, ninavyofahamu mimi kama clip hii ni fake Lwakatare atakuja na ushahidi tosha wa hii Clip ilikuwa ni wapi na ilihusu nini na akina nani aliokuwa nao kwa siku hiyo. Ila kwa Uharamia wa hawa watu yaani CCM na vyombo vyao vya Dora wasije kumpoteza(kumuua) Lwakatare na tukabaki dilema bila kujua kinachoendelea ninachoomba Viongozi wa Juu wa CHADEMA kwa sasa sio muda wa kulala wafuatilie kwa makini na kuhakikisha usalama wa Lwakatare huko alipo na kuhakikisha anatoka akiwa salama.
 
Tunataka majibu sahihi kwann kiongozi mkuu wa chama anajihusisha na vitendo vya kigaidi?

Nenda kawaulize poliCCM pia utafute na majibu kwa nini Mwenyekiti wa CDM kule Usariver aliuawa na miongoni mwa waliofanya mauaji ni kiongozi wa CCM na kwa nini watuhumiwa walitoroka mbele ya Polisi na hadi leo hawajakamatwa.
 
na inawekana kupewa sumu ya kumuua taratibu ili wananchi tubaki dilema kuhusu hili. maana hili liko wazi tu kuwa limepikwa na mwisho wake litakuwa wazi. sasa kwa kuogopa kuumbuka magamba wanaweza kumpa sumu ya kumuua taratibu.
 
Nimefuatilia kwa makini sakata hili la video ya uchochezi iliyotolewa kwenye mtandao na kuchukuliwa kwa uzito wa juu na kasi ya ajabu na jeshi letu la Polisi.Pia tamko la CHADEMA kupitia katibu wake mkuu.

Kwa muono wangu hili jambo sio zuri kwa pande zote, kama alivyosema Slaa kuwa mkanda "umepikwa" nadhani hiyo haitoshi maana wapinzani wao na Polisi yao wanaweza kukomaa kuwa kwa uchunguzi wao ni kuwa mkanda ni wa kweli.

Lakini hata kwa CCM na serikali yake kama itadhibitika mkanda umechakachuliwa hilo litakuwa pigo la mwisho kwa tuhuma kuwa kuna mkono wa serikali katika matukio yote ya aina hiyo yanayotokea.

Nawashauri CHADEMA wasiishie kusema wanasubiri kesi ipelekwe mahakamani pekee,maana hata kesi kuwa mahakamani inaweza chukua hata miaka mitatu na huku propaganda chafu zikiendelea na imani ikitoweka kwa wale ambao uelewa wao wa masuala ya tekinolojia hii ni mdogo( Ambao ni wengi sana miongoni mwetu)

CHADEMA wagharamie kwa uwazi kuweka wapelelezi hata wa nje wanaofanya kazi kisheria na wenye uwezo wa kungamua nini kimefanyika na kutoa taarifa ya wazi kwa jamii ya Kitanzania na hata nje ya nchi ili watawala wetu wafahamike wanafanya nini katika nchi inayopigiwa upatu kuwa ni ya Amani.

Kila jambo jema lina gharama yake.

Ushauri mzuri, natumaini viongozi wa Chadema watafuatilia
 
R U Really SERIOUS? CHADEMA Ikodishe WACHUNGUZI wa KIMATAIFA wao KAMA NANI? Hawana DOLA; Tangu lini CHama cha UPINZANI kikaitisha Wachunguzi toka NJE ya nchi? Hiyo itakuwa ni sawa na kuleta Jeshi toka Nje kwa CHAMA PINZANI... Sio rahisi kama Chama Tawalatika chenye Serikali... WOW kweli tutafika???

Nani kakwambia kuwa kukodi wapelelezi kunahitaji kuwa na dola? Sijui umri wako ila nikupe kisa kimoja kilichowahi kutokea miaka ya mwanzaoni ya 70. Wenye kumbukumbu nzuri zaidi yangu wataiweka sawa.
Mama mmoja wa Kihindi aliyetoka katika familia ya kitajiri aliwekewa bima ya maisha ya kiwango kikubwa na familia yake na akaja kuolewa na mhindi mwenzake ambaye(huyo mume) hakuwa mwaminifu. Mume aka tengeneza ajali iliyoondoa uhai wa mkewe katika maeneo ya milima ya Lukumbulu barabara ya Njombe- Songea ili apate urithi wa fedha ya ile bima.
Familia haikuridhika na upelelezi wa Polisi wetu,hivyo ilikodi wapelelezi toka nje (kama sikosei Scotland yard) na ushahidi wa kuhusika kwa mume katika ajali ile ulitumika katika mahakama ya TZ na akahukumiwa kifo. Huyu ni mmoja ya waliotekelezewa adhabu hiyo enzi za Nyerere. Jee wale wahindi walikuwa na dola?

Pia jambo lingine ni kuwa clip iko Youtube hivyo kuijua kuwa imechakachuliwa hakuna ulazima kwa wao kuja mpaka huku,kwa nini hili la upelelezi toka nje mnaliogopa kama mnavyoogopa kuundwa kwa tume ya kimahakama?
 
Kaka kama uelewa wako wa mambo ni mdogo afadhali uache kuropokaropoka hovyo. Kwa taarifa yako CDM wakiamua kukodisha wataalamu wa IT kutoka nje inawezekana kabisa. Kwani ni lazima wafike kwenye nchi inayoendeshwa na wakoloni weusi waweze kufanya kazi yao? Wanaweza kufanya kazi yao na kutengeneza evidence wangali katika nchi zao. Kinachofanyika ni kucheza tu na teknolojia na kufanya analysis ili kuthibitisha sauti halisi na iliyopikwa; recording halisi na iliyopikwa. Tena wataalamu hao wakifanyia kazi huko kwao ndio itakuwa rahisi zaidi kwani wataaccess mitambo yao kirahisi zaidi na hawatakuwa na hofu ya kumwagiwa tindikali ama kutekwa na kuteswa. LOL!!!!!!
 
Hata kama bajeti inapiga chenga, wananchi wenye mapenzi mema na CDM tutachangia ili kuwashinda wadhalimu dhidi ya CDM na maisha ya wanyonge. Nashauri viongozi wa CDM wafanye juu chini watengeneze mkakati wa kufanya uchunguzi mapema kabla sumu haijasambazwa na wadhalimu ... ni vyema wakati wanataka kupeleka ushahidi maakamani wakutane na ushahidi wa kweli ili waumbuke asubuhi na mapema!!!! Hii itatuimarisha sana kwenye kampeni za kuingia ikulu kwani tutakuwa na recorded evidence!!!!!
 
Wazo zuri sana, inashangaza mikakati ya hatari kama hiyo inayoonekana kwenye ile clip kufanywa sehemu ambayo watu wanapita pita. Hii clip kwa vyovyote vile ni moja ya mikakati ya akina Nchemba na mzee wa gombe ya kuimaliza Chadema kabla ya 2014.
CCM mtaua watu lakini mwisho wa siku damu ya mtu haipotei bure, mtaumbuka tu. only time will tell.

Hapo kwenye red hapo! Jeshi letu la maombi kwa sasa lipo imara, amealikwa kwenye uzinduzi wa album na pale kuna roho mtakatifu atatenda cku hiyo hivyo wenye tunguri watalia kwa malaria ya pepo mchafu. Nitawajulisheni kitakachofanyika pale maana Mungu wetu ni mwenye nguvu na lazima atatenda, Amen
 
Sasa unataka wachunguze nini wakati wameshasema kuwa ni ya kupikwa?

Kauli yao kuwa hii video ni ya kupikwa inamaana tayari wameshachunguza. Wanachotakiwa kufanya sasa ni kuelezea objectively ili kila mtu aelewe kuwa kweli imepikwa.
 
ninvyoamini mm humu jf walio wengi ni wasomi na waelewa sana tena wa hali ya juu. sasa inapotokea issue kama hii ya lwakatare na watu wamejitokeza wengfi tuu kuueleza umma hapa jf kasoro kadha wa kadha kuhusu ile video clip na kuwalete baadhi ta clips ambazo zimeingizwa maneno ili kuwaonyeha watu kuwa teknolojia hiyo ipo na wala tusi jiaminishe asilimia mia kuwa ni kweli. lkn inaonekana hata members ambao wanauelewa juu ya uwapo wa hii teknolojia wanabisha na kukataa kabisa kana kwamba uwezekano wa kutengeneza video ile haupo sasa je wananchi wa kawaida ambao uelewa hawana itakuwaje? kumbe tz tumeathiriwa na mfumo wa chama kimoja tu na ndio maana mambo hayaendi. wanapotokea wanamageuzi basi hufanyiwa kila njama kuwadhoofisha badala ya kuudhihirishia umma kwa kutekeleza ilani za chama (ccm). maskini tanzania.
Tanzania is full of opportunists and hypocrites, kuna watu wameshaamua "YOU CANT FIGHT THEM YOU JOIN THEM" akina STEVE BIKO Tanzania hawapo ndugu yangu.. Ila Nyerere alituua kisaikolojia hata tunaojifanya wasomi...badala ya shuleni kufundishwa CIVICS (Elimu ya Uraia) watu tukafundihwa ELIMU YA SIASA matiokeo yakw watanzania ni waoga hawajui haki zao, wajibu wao na wajibu wa serikali!! Matokeo yake wamebaki kuwa waoga tu, bila hata ya kujua wanachokiogopa (FEAR OF THE UNKNOWN FACTOR)! Na haya mauaji yanayotokea na utekwaji na utesaji unaoendelea na kukua kwa kasi basi sote tuliosoma elimu ya siasa magoti yanagongana kwa HOFU..!! Ndio maana watanzania ukiwapa nafasi ya kuongea wanaongea kwa jazba maana wana hasira ya kitu ambacho hawakijui!!
 
R U Really SERIOUS? CHADEMA Ikodishe WACHUNGUZI wa KIMATAIFA wao KAMA NANI? Hawana DOLA; Tangu lini CHama cha UPINZANI kikaitisha Wachunguzi toka NJE ya nchi? Hiyo itakuwa ni sawa na kuleta Jeshi toka Nje kwa CHAMA PINZANI... Sio rahisi kama Chama Tawala chenye Serikali... WOW kweli tutafika???

is that your opinion or you have authority to prove your statement? Private investigation hairuhusiwi? Yaani cdm wakiomba hiyo clip ichunguzwe na private international investigators haiwezekani? You must be joking be serious!
 
R U Really SERIOUS? CHADEMA Ikodishe WACHUNGUZI wa KIMATAIFA wao KAMA NANI? Hawana DOLA; Tangu lini CHama cha UPINZANI kikaitisha Wachunguzi toka NJE ya nchi? Hiyo itakuwa ni sawa na kuleta Jeshi toka Nje kwa CHAMA PINZANI... Sio rahisi kama Chama Tawala chenye Serikali... WOW kweli tutafika???
mkuu sijui unachobishia ni kitu gani, CHADEMA kufanya uchunguzi binafsi ni ili kujihami na zile tume za uchunguzi zinazoundwa na serikali hii dhalimu ya CCM (haziaminiki). ila umenishangaza kuita uchunguzi binafsi sawa na kuingiza jeshi toka nje, loh.
 
Nimefuatilia kwa makini sakata hili la video ya uchochezi iliyotolewa kwenye mtandao na kuchukuliwa kwa uzito wa juu na kasi ya ajabu na jeshi letu la Polisi.Pia tamko la CHADEMA kupitia katibu wake mkuu.

Kwa muono wangu hili jambo sio zuri kwa pande zote, kama alivyosema Slaa kuwa mkanda "umepikwa" nadhani hiyo haitoshi maana wapinzani wao na Polisi yao wanaweza kukomaa kuwa kwa uchunguzi wao ni kuwa mkanda ni wa kweli.

Lakini hata kwa CCM na serikali yake kama itadhibitika mkanda umechakachuliwa hilo litakuwa pigo la mwisho kwa tuhuma kuwa kuna mkono wa serikali katika matukio yote ya aina hiyo yanayotokea.

Nawashauri CHADEMA wasiishie kusema wanasubiri kesi ipelekwe mahakamani pekee,maana hata kesi kuwa mahakamani inaweza chukua hata miaka mitatu na huku propaganda chafu zikiendelea na imani ikitoweka kwa wale ambao uelewa wao wa masuala ya tekinolojia hii ni mdogo( Ambao ni wengi sana miongoni mwetu)

CHADEMA wagharamie kwa uwazi kuweka wapelelezi hata wa nje wanaofanya kazi kisheria na wenye uwezo wa kungamua nini kimefanyika na kutoa taarifa ya wazi kwa jamii ya Kitanzania na hata nje ya nchi ili watawala wetu wafahamike wanafanya nini katika nchi inayopigiwa upatu kuwa ni ya Amani.

Kila jambo jema lina gharama yake.
kuna haja ya kufanya uchunguzi kama Chadema kilikuwa na ugomvi wa kimaslahi au kisiasa na waandishi wa habari wachombo kilichotajwa. habari hizo zichambuliwe na kama Rwakatare alishalalamika au kutoa madai yoyote. baadae tuangalie kama hilo lingeweza kupelekea kulipa kisasi. mwisho hiyo video ifanyiwe utafiti wa kitaalamu ikiwa ni pamoja na sauti yake kama ni ya mhusika
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom