CHADEMA huwalipa wanaoandamana

CHADEMA huwalipa wanaoandamana

Joseph Ludovick

JF-Expert Member
Joined
Aug 11, 2013
Posts
382
Reaction score
506
Ndugu,

Wakati maandamano yametangazwa nchi nzima na chama chetu, na kwa kweli mimi nilisema sitashiriki kwa sababu ambazo nilieleza, na zote zimeonekana kuwa kweli, dhamiri yangu imenituma kuongea jambo jingine ambalo laweza kusaidia baadhi ya watu. Ingawa najua chama changu hakitafurahishwa na hii revelation, lakini napenda nihukumiwe kwa kuutumikia ukweli.

Ndugu, wengi wa makamanda wetu hujitolea kufanya kazi za chama. Na kwa kweli umati wa wanaojitokeza kwenye shughuli za chama chetu CHADEMA kama mikutano ya hadhara ama maandamano, huja wenyewe bila kupewa fedha. lakini hii siyo kwa wote.

Chama chetu kwa muda sasa kinao utaratibu wa kuwalipa watu ili wajitokeze kuhamasisha wengine kujitokeza kwenye maandamano.

Hii ni kweli kwenye mikutano ya hadhara pia, ingawa sisi hupenda sana wengi wa wanaojitolea na wapinzani wetu wa CCM wasijue kuwa huwa tunagharimia mambo hayo.

Nakumbuka tukiwa chuo kikuu, mimi nikiwa mwenyekiti wa CHASO DUCE, tulivyokuwa tukilipa makundi ya wanafunzi ili wajitokeze kwenye makongamano ya katiba siku hizo.

Mzee Warioba amewahi kuzomewa na kundi la wanafunzi wanachama wa chadema pale Karimjee hall alipoanza speech yake kwa kusapoti ile orodha iliyoitwa siku zile "sacrosanct issues" hakika tulimzomea. alikatisha hotuba yake. Vilevile, tulikuwa tukiwalipa hela kutoka makao makuu ya chama wanafunzi baadhi ili wahamasishe maandamano na migomo chuoni.

Hivyo basi kwenye mikutano yetu, huwajazia mafuta bodaboda na watu wa bajaji, na katika maandamano huwa wanalipwa baadhi ya watu ili kuhimiza wengine.

Ni kweli hawalipwi wote, lakini hakika kuna wanaokuwa wamelipwa ili kuonyesha kuwa tunaungwa mkono na hao waongoze kuitikia hatimaye wengine wajiunge nao. Kwa hiyo katika maandamano kuna wanaolipwa na kuna wengi wasiolipwa.

Naandika mada hii kuwasadia wale ambao hujitolea tu wajue kuwa katika mkusanyiko huo kuna wenzao ambao huwa wamelipwa hela na hawa wakishawahamasisha wengine wao huishia zao kwahiyo wanaokuja kupatwa na matatizo hasa ni wale wanaojitolea tu bila kulipwa chochote.

Najua kisa kimoja Mbeya, pale waandamanaji walipoumizwa, walijiuguza wao wenyewe bila msaada wa chama. jambo hilo liliumiza sana familia zao na kwa hali ya sasa mbeya na hasa Mwanjelwa lilipotokea tukio lile, vijana hawajitokezi kwenye maandamano, bali wanadai na watoto wa viongozi nao waje mbele ndipo wataandamana. kwa hiyo ndiyo maana pia Mbeya wamegomea maandamano haya ya CHADEMA.

Hatimaye, nawaomba wananchi watafakari kama kila mtu ataachwa kucheza na sheria atakavyo, nini itakuwa future ya nchi yetu!. nina hakika chama chetu cha CHADEMA kikiingia madarakani mwaka 2015 (???) hatutaruhusu maandamano kama haya ya sasa.

Mfano tumeshaonyesha kwa chama kuzuia wanachama wake na mashabiki kuhudhuria mikutano ya Zitto Kabwe. hulka hiyo itakuwa kubwa kwa wapinzani mwaka kesho tutakapochukua dola!

Wenye masikio na wasikie.

Mwl.Ludovick
 
Ni bora Propaganda za akina Ritz, MSALANI Lizaboni Simiyu Yetu Chabruma chama,@kiroriti na wote wale Nyumbu wa Lumumba ambazo huwaga tunazichukulia kam kuchangamsha genge,lakini za Kwako,tunazichukulia kama taka taka zinazotoka kwa mtu aliyekata tamaa ki maisha,hohe hahe asiye na mbele wala nyuma,anayetegeea fadhili za mtu yoyote yule ili walau Mkono wake uende Kinywani.
Watu kama wewe ni hatar hata kwa maisha ya ndugu zako wa karibu kabisa,kama vile Mama na Babaako,watu kama nyie mko tayar kuwatoa kafara wapendwa wenu kwa waganga wa kienyeji ili mpate utajiri.
Kimsingi nina kudharau sana.
 
Last edited by a moderator:
ungekua na uwezo wa kuifuta chadema nina uhakika sasa hivi ingekua imebaki historia tu.maana hii chuki imevuka mipaka!Kweli kaka unakipenda sana chama chako.
 
Duh! Kuumbe! Nadhani na ile ishu ya kugawa viroba kwanza kwa waandamanaji itakuwa ni kweli.
 
We ulitakaje!

Make hata ukitaka kula lazma uliwe.

Katika jambo lolote lile, lazma kuna wanaolipwa.

Nitajie kitu ambacho utakifanya bila kulipia au mwenzako kufaidika.

Ukienda kuoa, lazma mahari utoe.
Unataka kusema kwenye miaka 50 ya uhuru hakuna waliolipwa!
Wakimbiza mwenge na wanaoshughudia hulipwa?

Ivi kukiwa na onyesho la bore uwanja wa taifa, na mgeni rasmi ni rais, unadhani hakuna watakaolipwa?
 
We Mzee wa kuasisi Mkanda wa Ugaidi upo? - Yule jamaa muasisi mwenzako sasa hivi anakula bata tu, kashakusahau kama bado unaishi duniani. Wakati wewe unahangaika na vi-sredi vya kuchonga humu JF ili watu wajue bado una exist. na bado kama ulikuwa huijui ile policy na USE AND DUMP inayotumika pale Lumumba - utaisoma.
 
Ni bora Propaganda za akina Ritz, MSALANI Lizaboni Simiyu Yetu Chabruma chama,@kiroriti na wote wale Nyumbu wa Lumumba ambazo huwaga tunazichukulia kam kuchangamsha genge,lakini za Kwako,tunazichukulia kama taka taka zinazotoka kwa mtu aliyekata tamaa ki maisha,hohe hahe asiye na mbele wala nyuma,anayetegeea fadhili za mtu yoyote yule ili walau Mkono wake uende Kinywani.
Watu kama wewe ni hatar hata kwa maisha ya ndugu zako wa karibu kabisa,kama vile Mama na Babaako,watu kama nyie mko tayar kuwatoa kafara wapendwa wenu kwa waganga wa kienyeji ili mpate utajiri.
Kimsingi nina kudharau sana.

- Jibu hoja wacha matusi yangekuwa mali mngeshashika dola, jibu hoja kama huna kaa pembeni waachie wenye hoja mamabo ya baba na mama yako yantokea wapi hapa, le mburulazzzz

Le Mutuz
 
We Mzee wa kuasisi Mkanda wa Ugaidi upo? - Yule jamaa muasisi mwenzako sasa hivi anakula bata tu, kashakusahau kama bado unaishi duniani. Wakati wewe unahangaika na vi-sredi vya kuchonga humu JF ili watu wajue bado una exist. na bado kama ulikuwa huijui ile policy na USE AND DUMP inayotumika pale Lumumba - utaisoma.

- Jibu hoja kama huna kaa pembeni tumechoka na maneno yenu ya hovyo hovyo weka hoja hapa wachana na mjumbe jibu hoja zake

Le Mutuz
 
Mkuu umekosea ni ccm ndio wanaokodi watu
 
Kumekucha! Endelea kutujuza! Kumbe nao wana walipa waandamanaji duuu ndio maana kuna mtu alisema yuko tayari kupigwa Risasi!
 
Ndugu,

Wakati maandamano yametangazwa nchi nzima na chama chetu, na kwa kweli mimi nilisema sitashiriki kwa sababu ambazo nilieleza, na zote zimeonekana kuwa kweli, dhamiri yangu imenituma kuongea jambo jingine ambalo laweza kusaidia baadhi ya watu. Ingawa najua chama changu hakitafurahishwa na hii revelation, lakini napenda nihukumiwe kwa kuutumikia ukweli.

Ndugu, wengi wa makamanda wetu hujitolea kufanya kazi za chama. Na kwa kweli umati wa wanaojitokeza kwenye shughuli za chama chetu CHADEMA kama mikutano ya hadhara ama maandamano, huja wenyewe bila kupewa fedha. lakini hii siyo kwa wote.

Chama chetu kwa muda sasa kinao utaratibu wa kuwalipa watu ili wajitokeze kuhamasisha wengine kujitokeza kwenye maandamano.

Hii ni kweli kwenye mikutano ya hadhara pia, ingawa sisi hupenda sana wengi wa wanaojitolea na wapinzani wetu wa CCM wasijue kuwa huwa tunagharimia mambo hayo.

Nakumbuka tukiwa chuo kikuu, mimi nikiwa mwenyekiti wa CHASO DUCE, tulivyokuwa tukilipa makundi ya wanafunzi ili wajitokeze kwenye makongamano ya katiba siku hizo.

Mzee Warioba amewahi kuzomewa na kundi la wanafunzi wanachama wa chadema pale Karimjee hall alipoanza speech yake kwa kusapoti ile orodha iliyoitwa siku zile "sacrosanct issues" hakika tulimzomea. alikatisha hotuba yake. Vilevile, tulikuwa tukiwalipa hela kutoka makao makuu ya chama wanafunzi baadhi ili wahamasishe maandamano na migomo chuoni.

Hivyo basi kwenye mikutano yetu, huwajazia mafuta bodaboda na watu wa bajaji, na katika maandamano huwa wanalipwa baadhi ya watu ili kuhimiza wengine.

Ni kweli hawalipwi wote, lakini hakika kuna wanaokuwa wamelipwa ili kuonyesha kuwa tunaungwa mkono na hao waongoze kuitikia hatimaye wengine wajiunge nao. Kwa hiyo katika maandamano kuna wanaolipwa na kuna wengi wasiolipwa.

Naandika mada hii kuwasadia wale ambao hujitolea tu wajue kuwa katika mkusanyiko huo kuna wenzao ambao huwa wamelipwa hela na hawa wakishawahamasisha wengine wao huishia zao kwahiyo wanaokuja kupatwa na matatizo hasa ni wale wanaojitolea tu bila kulipwa chochote.

Najua kisa kimoja Mbeya, pale waandamanaji walipoumizwa, walijiuguza wao wenyewe bila msaada wa chama. jambo hilo liliumiza sana familia zao na kwa hali ya sasa mbeya na hasa Mwanjelwa lilipotokea tukio lile, vijana hawajitokezi kwenye maandamano, bali wanadai na watoto wa viongozi nao waje mbele ndipo wataandamana. kwa hiyo ndiyo maana pia Mbeya wamegomea maandamano haya ya CHADEMA.

Hatimaye, nawaomba wananchi watafakari kama kila mtu ataachwa kucheza na sheria atakavyo, nini itakuwa future ya nchi yetu!. nina hakika chama chetu cha CHADEMA kikiingia madarakani mwaka 2015 (???) hatutaruhusu maandamano kama haya ya sasa.

Mfano tumeshaonyesha kwa chama kuzuia wanachama wake na mashabiki kuhudhuria mikutano ya Zitto Kabwe. hulka hiyo itakuwa kubwa kwa wapinzani mwaka kesho tutakapochukua dola!

Wenye masikio na wasikie.

Mwl.Ludovick

- Kumbe ulipokuwa huko Chadema umejonea mengi ya ajabu na hawa wanafiki wakubwa, ndio maana miaka 30 hakuna dola wanaishia side lines na kuandamana na kugoma tu, wewe sema wasikutishe hawana lolote na matusi yao ya kizamani zamani wakati huku mjini kuna matusi mapya kabisa le mburulazzz, weka habari hapa tuone mchele na pumba kujibu hoja hawawezi kwa sababu hawa ni wapambe tu hawajui lolote kile chama kina wenyewe muulize yule kijana waliyekuwa wanamtumia kutukana Viongozi wa CCM mitandaoni walivyomtupa kwenye uchaguzi wao hahahahahaha!!

Le Big Show
 
HEHEHEHEHEHEHE....Bwahahahahahahahah.......Mzee wa mabebz akimshangilia muuaji men.....
 
- Kumbe ulipokuwa huko Chadema umejonea mengi ya ajabu na hawa wanafiki wakubwa, ndio maana miaka 30 hakuna dola wanaishia side lines na kuandamana na kugoma tu, wewe sema wasikutishe hawana lolote na matusi yao ya kizamani zamani wakati huku mjini kuna matusi mapya kabisa le mburulazzz, weka habari hapa tuone mchele na pumba kujibu hoja hawawezi kwa sababu hawa ni wapambe tu hawajui lolote kile chama kina wenyewe muulize yule kijana waliyekuwa wanamtumia kutukana Viongozi wa CCM mitandaoni walivyomtupa kwenye uchaguzi wao hahahahahaha!!

Le Big Show

Hakika mwaka huu watu wameanza kufunguka bado yule dereva wa Chacha!
 
Back
Top Bottom