chadema hili turekebishe!!

kumbe Mhe lema mlokole? mwenye uelewa wa kutosha naomba anijuze maana ya ulokole kama hata Godbless yumo!!!!!

tena ameandika na kitabu ambacho kinaweza kukufanya ukajukusimama na mungu katika maisha yako kipo ni biblecommentary but jina limenitoka kidogo.
 
Nunua cd za mikutano iliyofanyika recently utapata majibu yote!lakini haya mambo yanahitaji marekebisho kidogo,natumaini viongozi wetu wamesikia,lakini kikubwa tunachohitaji ni ukombozi ili tuondokane na hili gari bovu lenye miaka hamsini haiwezi kutufikisha safari tunayotaka kwenda cause it's way far!
 
umetumwa weewe na hii haitakusaidia chama kile kiko kwenye kukomboa watanzania na sio waumini
 
wanapiga nyimbo za dini ili kukimbiza wachawi na mashetani ambayo yanaweza yakawa yametumwa kuja kuvuruga mikutano

nyimbo za dini za kupunga mapepo/mashetani ni kwaya pekee?!

CDM Arusha kweli wanachemsha sometimes. wakipiga PA (public announcement) zao mtaani, kwaya zinatawala mpaka inakuwa kero. mtoa mada yupo sahihi kabisa.
hata sisi wapagani tumo chamani. we all need to be recognised as one CDM family.
 
  • Thanks
Reactions: Axe
Mleta hoja Axe ana hoja, wana CDM tusibeze kila kitu. Ni kweli ukisikiliza miziki hasa inayopigwa NMC-Unga ltd ina beats za nyimbo za kidini, PJ ameleta mfano wa wimbo unaosema 'Mungu kwanini umeruhusu haya?', lakini vile vile kuna nyimbo zenye beats kama nyimbo za Beatrice Mhone kwa wanaozifahamu. In short haipendezi si kwa chama pekee bali pia masikioni mwa wenye imani tofauti. Mara nyingi hii inatokea hasa Arusha, ukifika mkutanoni sometimes unaweza usitofautishe na mkutano wa kidini kwa nyimbo zinazopigwa hata baadhi ya makamanda wanavyohutubia utadhani wanakemea mapepo. Tujirekebishe. Ila labda cha msingi mtu anayefika mkutanoni asikilize ujumbe zaidi kuliko beats za mziki.
 
Last edited by a moderator:
  • Thanks
Reactions: Axe
Now days hata baa hizi nyimbo zinapigwasana! Ila ushauri ni mzuri, Mi mwenyewe nineokoka lakini Biblia inasema ole kwa wanaosababisha makwazo, so kama kuna watu wanakwazika tutafute normal songs. Zenye maana, wasanii wapi watumieni Waring's nyimbo normal to both sides!
 
Mwenye akili anajua nia ya huyu bwana. Sio nzuri. Nimehudhuria mikutano mingi ya CHADEMA, sijasikia hizo nyimbo hata siku moja
 
  • Thanks
Reactions: Axe
Umesaambiwa nunua cd then sikiliza hatuko hapa kubishana tuko hapa kurekebishana!
 
Mimi ni mwanachama wa cdm na mpenda mageuzi kinachonikera kwenye hichi Chama changu ninachokipenda sana!! ni hizi nyimbo za kidini zinazopigwa kwenye mikutano ya cdm napa Arusha sina uhakika na sehemu nyingine ukifika kwenye mikutano hii utazani mzee wa upako au kakobe anahutubia nataka niwakumbushe viongozi wangu na mbunge wangu mheshimiwa lema bado wewe ni mbunge wangu najua wewe ni mlokole lakini kumbuka wanachama wote cdm si wakristo na mikutano ya kisiasa sio ya kidini na wala Chama hakina dini na kwamtu ambaye si mkisto sehemu Kama ile anakua uncomfortable to be honest ingekua wewe ni mkristo na kwenye mkutano wa Chama chako ikawa inapigwa KASWIDA ungejisikiaje? Leo cdm inatakiwa kuunganisha watu wote na dini zote ili kuchukua dola na isifanye makosa ya cuf kuzani unaweza kuchukua dola na watu wa dini moja ili tufike tunakoenda lazima tukosoane na kuelezana ukweli people's power!!
Nimekukubali sana kaka.. ukweli usemwe haiwezekani upende kitu bila kukikosoa pale unapoona ndivyo sivyo... pamoja.. peopleeeeee power
 
Mi na cd za CHADEMA za mauaji arusha inayoitwa "SAFARI KUELEKEA DEMOCRASIA YA KWELI"
Inaonesha chanzo cha mgogoro hatua na hatimaye polisi walivyoua raia. Kweli kwenye mikutano sijasikia nyimbo zma namna hiyo.

Kwenye mkutano mwanza kupinga mfumuko wa bei Zilipigwa nyimbo za Sarafina "FREEDOM IS COMING TOMMOROW" Sa haya sijui yanatoka wapi

kuweni makini na mada kama hizi ni wazi mada hii Itaongeza chuki za kidini zidi ya chadema!
 
jambo hili kama lina ukweli linawagawa watanzania hasa wale wenye upeo mdogo. kwa namna nyingine wale wanaosema kuwa chadema ni chama cha kikikristo watapata mwanya mkubwa na vielelezo vitaongezeka.

ukweli ni kwamba CHADEMA ipo hivyo ilivyo kwa kuwa viongozi wake wanamwogopa mungu wa kweli. mungu anayetangaza mapendo daima na asiye wa kisasi au anayeruhusu mauaji!

nadhani wote ni mashuhuda wa ile mikutano ya waislamu iliyotangaza hadharani kuwa chadema ni chama cha wakristo! sasa tukizubaa watapata pointi zaidi hawa watu wenye uduni wa kufikiria.

lengo la chadema laweza kuwa zuri kupiga nyimbo hizo lakini ni muhimu sana kutazama mazingira ya kufanyia jambo hilo!
 
kama ni kweli tabia hii itomezwe mara moja...mimi ni mkristo lakini CDM ni ya imani zote
kama si kweli basi hakuna haja ya malumbano, mikutano hiyo inahudhuriwa na maelfu na watu na hizo nyimbo hazipigwi kwa sauti ya kunongona, Penye ukweli uongo utajitenga
 
Back
Top Bottom