Poteza muda wako kuandika unafiki tu. Nitajie wimbo mmoja wa kwaya au injili ulipigwa ktk mikutano hapa Arusha. Umetumwa na nani wewe kibuyu?
(i declare my interest mimi ni CDM)
chama chetu kimefikia hapa kilipo kutokana na mchanganyiko wa michakato na juhudi za aina nyingi sana lakini kikubwa kilichofanya chama kuwa na nguvu hasa hivi karibuni ni kutokana na KUSHINDWA kwa ccm kusimamia maslahi ya wananchi na badala yake kuendekeza ubinafsi na ufisadi, napenda kuamini kuwa ni kwa ubinafsi huu wa chama TAWALA, chadema waliamua kuwa na kauli mbiu zinazo onyesha ushirikishwaji wa wanachi kwa ujumla kama ile ya PEOPLES.... and M4C.
Mambo makubwa yaliyofanya CCM ifikie hapo ni KIBURI, DHARAU, NA MAZOEA kwa viongozi waandamizi na wafuasi pia, hawa nduguzetu kila walipokua wakikosolewa walitoa kauli tata na za kashfa kama..UMETUMWA, WIVU WA KIKE, MTAKULA MAJANI LAKINI NDEGE TUTANUNUA, VIJISENTI, WANANCHI OMBA OMBA,NA MTAJIJU. wanachama pia walitetea viongozi wao kwa kauli hizo hizo za ajabu.Kilichofuata ni anguko na kimsingi wanajiandaa kukabidhi madaraka
MSINGI wa hayo apo juu ni hii tabia ambayo baadhi ya washabiki(wanachama) mmeianzisha,naogopa kusema kuwa tumeingiwa na kiburi cha mwangaza wa mafanikio na kuanza kupuuza hoja za muhimu za baadhi ya wanachama au hata wapinzani wanaotukosoa. Kila thread inayokosoa chama hata kwa mambo yaliyowazi,itapokelewa kwa kauli za kashfa na kejeli hata kama ilikua na lengo la kujenga mwenendo mzima wa hiki chama. Kinachofuata tutaogopa kukosoa na kutunga nyimbo za kusifia tu kama JOHN KOMBA na nyimbo zake kwa magamba, kitu ambacho kinaua utendaji mzuri wa chama.MTOA HOJA ana lalamiko la msingi kama ambavyo wamekuwa wengine waliopita...tungemjibu kwa hoja na si haya maneno ya nayofanana sana na yale ya CCM wakati ule walipokuwa wamejisahau..CDM si malaika na ni vyema ku discuss changamoto mwanzoni kuliko kusuburi mpaka zinapokua zimezoeleka na kuwa TABIA
wenye maskio na mskie.....PEOPLEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEESSSSSSSSSSSSSSSS