CHADEMA hawana Ikulu wanarusha chopa tatu angani kujenga chama, wakichukua nchi itakuwaje?

mchlmmnl2

Senior Member
Jul 13, 2013
168
53
Kurusha Helkopta kutoka Dar-Arusha (Takriban 450KM) kunagharimu takriban 5M, hii ni pamoja na Fuel, parking fees, Mshahara wa rubani na check up.

2. Kurusha helkopta 3 kwa wakati mmoja kuzunguka mikoa 9 (Takriban 4,050KM) kutagharimu zaidi ya 45M

3. Usafiri wa ndani ya mikoa 9 kwa magari, chakula na malazi kwa viongozi kutagharimu takriban TShs laki 5 kwa kila kiongozi mmoja kwa siku.

4. Maandalizi ya sehemu za mikutano, majukwaa, vipaza sauti, umeme na viburudisho kutagharimu takriban TShs laki 5 kwa sehemu moja kwa kila siku moja.

5. Gharama za usalama (Redbigades) mikutanoni, chakula na usafiri vinaweza kugharimu TShs 5,000 kwa kila kijana mmoja kwa siku kwa eneo moja la mkutano.

Inaweza kugharimu chama zaidi ya TShs 600M kwa mzunguko wa mikoa 9 kwa siku chache.

Ni nini vyanzo vya fedha kwa matumizi haya, ruzuku, wafadhili wa ndani/nje au mkopo?

Haya yanafanyika huku chama kikiwa na ofisi za kupanga, huku ofisi nyingine zikiwa zimefungwa kutokana na kushindwa kulipa kodi, Baadhi ya ofisi za mikoa zikitumia magari binafsi ya wanachama waliojitolea huku viongozi wakuu wakisafiri na familia zao kubwa na watumishi wa ndani kwa gharama za chama.

AKILI NI MALI, KIJANA USIKUBALI KUTUMIKA NA WANASIASA
 
Kwani ni nani ana chama mpaka na wewe ungependa uwe nacho acha mahesabu ya kifukara unafikiri Tanzania ni kama mtaa wenu kila jambo lina maandalizi yake we mwenyewe unasubili kwa ham kitenge ,kofia majarida nyimbo misafara
 
Habari ndo hiyo! CDM ndo habari ya mjini. Mwenye wivu ajinyonge!

attachment.php
 
Safari za Mwenyekiti wa CCM USA na Ulaya zimetugharimu kiasi gani cha fedha, Je ni kiasi gani hao Vigogo wa CCM wameficha USWISS, Ni gharama kiasi ani tumepigwa kwa mikataba ya kifisadi, Kama unadhani Elimu wanayotoa CAHDEMA ni Ghali jaribu Ujinga wa kuwafagilia mafisadi wanaotuahidi watavua Gamba na GAMBA likawashinda kuvua, waliotuahidi maisha bora kwa kila Mtanzania kumbe ni Maisha mabaya kwa Kila Mtanzania, umeme, mfumuko wa bei za vyakula juu kabisa
 
Hii ndo gharama ya demokrasia.

Ukitaka ufanikiwa ni lazima uwekeze vya kutosha. Helcopta hizi kuna watu hawawezi kufika huko na wamejitolea watanzania wakombolewe.

Ukombozi ni gharama kubwa sana, na hata Nyerere alitoa vifaa vya kijeshi na jeshi kwa ukombozi wa Uganda, Mozambique, Angola na Zimbabwe.

Na viongozi wetu ni wa thamani sana kwa wananchi wa Tanzania ndo maana wanastahili kupanda chopa.

Chadema kimejengwa na itaendelea kujengwa sio kwa kukaa tu Dar bali kwa kwenda mikoani kwa gharama yoyote. Ndo maana nawaambia mtahaha usiku na mchana. CCM hamjachangia fedha yeyote zaidi ya kuhonga tu, Chadema wanatumia kujenga chama ninyi kununua wanachama wachovu mkidhani mnaua. Chadema ni kama hewa ya Oxygen kwa Tanzania utaivuta tu hata ukileta nyodo zako.

Chadema ni Chama cha thamani kubwa sana na tunakisupport kwa hali zote na mali ili tulete ukombozi wa kweli na kuteketeza ukoo huu wa panya.

Hata nyumbani kwako ili kumzuia mwizi ni lazima utumie gharama kubwa kujenga system ya mwizi kutopenya, na ndo Chadema wanajenga system hiyo ili kuwainua watanzania wanaoteseka kila siku kwa udhalimu wa magamba.

It is cost but liberation is coming soon
 
Nimependa andiko lako lakini umeonesha uwezo mdogo wa kupambanua mambo. Wahenga usema " KUPANGA NI KUCHAGUA" - Uliyoyaandika yanaeleweka wewe chaguo lako kwa Chadema ni kujenga ofisi lakini lao wenyewe ni mikutano ya nje. Wewe chaguo lako ni kwenda mikoani kwa magari wao chaguo lao ni helicopta.....

Ndugu yangu usisahau pia "DUA LA KUKU ALIMPATI MWEWE" Kwani nani asiyejua umuhimu wa kuokoa MUDA katika dunia ya leo na nchi yenye miundombinu mibaya ya barabara kama Tanzania? Mwisho kabisa "KUCHAMBA KWINGI UTOA MAVI" ushauri wako wa mlinganisho wa bei siyo sahihi kwani helcopta haigharimu kiasi cha 5m kwa 450 kms. Piga hesabu vizuri maana ukiangalia vizuri they save money kwa kutumia helicopta.
 

Lakini hizo HELIKOPTA haziui watu... ZINAKWENDA SEHEMU AMBAZO VIONGOZi hawawafikii Wananchi na NAPONGEZA sana

LAKINI Kwa CCM wao WATANUNUA MAGARI au KUJIHUSISHA na BIASHARA za UNGA na PEMBE bila kujali Uwezekano gani Utawawezesha hao VIONGOZI waVIVU wa CHAMA TAWALA kuwafikia wananchi na kusikiliza MAHITAJI YAO; Ambayo Sio MENGI na SIO ya KIUFAHARI isipokuwa ni ya KINADHARIA kabisa...

Ukiangalia CHADEMA inarusha HIZO HELIKOPTA sehemu ambazo Wananchi hawajawahi kupata kutembelewa na VIONGOZI na kusikilizwa Mahitaji yao; na Angalia picha ni UMATI wa Wananchi

Lakini CHAMA TAWALA haita dhubuti kwenda sehemu hizo NYETI; wao watakwenda sehemu ambazo ni rahisi kuvuta watu kwa MABASI; Kuwapa PESA; Kuwapa T-Shirts; Khanga, Vitenge, Skafu, Kofia na Wanawapikia Wali na NYAMA na kwasababu wengi wa hao Wananchi Wamezichoka hizo hotuba za CHUKI na MATUSI toka kwa VIONGOZI hao wa CCM wanaleta Wanamuziki VIJANA ambao viingilio vyao ni vya GHARAMA haswa mfano ni DIAMOND (Naseeb)
 
Uishi maisha marefu F. A. Mbowe, tupo tayari kukutumikia, hatuta sikiliza propoaganda za namna yeyote ile, OPARATION PAMOJA DAIMA-pamoja tutashinda, peoplessssssssssssssssssssss..........
 
Kweli akili yako ni ndogo sana mpaka unashindwa kupambanua mambo, hebu anza na mwenyekiti wako wa ccm taifa amefanya safari ngapi nje ya nchi?, unajua gharama anazotumia kwa safari moja?, je hizo safari zimeleta manufaa gani kwa wananchi wanyonge walioko kijijini?, Iwapo Marekani nchi yenye uchumi mzuri duniani, rais wake ana safari chache sana na hata marais wa nchi zilizoendelea kwa nini sisi tunafuja pesa hovyo? JITAMBUE....Ama kwa hakika nina wasi wasi na akili yako yani Helicopta kutoka Dar mpaka Arusha inagharimu 5Mil😨😨😨 .... Ni bora chadema inayotumia gharama kubwa kuwafikia wananchi walioko kijijini, kuwapa elimu juu ya katiba mpya, kuwapa matumaini mapya na elimu juu ya daftari la kudumu la wapiga kura....

My take: Dont post something just to have the record, i believe in Jamii Forum members in here are great thinkers, i dont expect such craps from you guys, try figuring things out before you post.
 
Siasa za chadema na dhana ya majinga ndo yaliwayo-hongera mbowe kwa kuthibisha ubingwa wako katika ujasiliamali.-
 
Mtoa mada,Hivi lengo lako ni nini hasa? Maana inaonekana hujui thamani ya muda na hujui lengo kusudiwa au wewe ndiyo wale hata mkeo akwambia mnunulie mwanao kitabu unalalamika anamatumizi mabaya ya fedha
 
Habari ndo hiyo! CDM ndo habari ya mjini. Mwenye wivu ajinyonge!

attachment.php

Kama hali ni Hii kwa kila Mkutano, Basi hela yao Imerudi maana kuna kile chama cha Mizigo hakipati hata Robo ya hao watu na bado kinakopa Mpaka Mfao ya wafanyakazi wake NSSF na mpaka leo hakija Lipa.
 
pesa za vyama ni kutokana na ruzuku kwa kiasi kikubwa

pesa za serikali inaniuma saaaaana najua kwa sababu ni ushuru niulipao mimi mwenye.

Kama ni vyanzo halali Ccm watumie pesa watakavyo ila kama wanachota hazina roho yaniuma saana.
 
CT-Scan ni shilingi ngapi vileeeeeeee????????????

Na Kwenye Hospital ya Taifa zako ngapi vileeeeeeeeeeeee?????????????
 
Utafiti uliofanywa kwa muda mfupi; imeonyesha wananchi wanahudhulia kushangaa helikopita za viongozi badala ya lengo mahususi

hii imedhirika wakati mh slaa alipotumia gari kwenda kigoma,tabora na singida . Mahudhulio ya mikutano yalikuwa hafifu sana.

Niwakati wa kupeleka ujumbe na kuwajenga wananchi na sio kupeleka helikopita ata mimi ni mshamba sijawahi ona helikopita.

Niwakati wa chama kukata gharama ; bilioni moja za kukodi helikopta kwa wakenya na kuuingizia uchumi wa kenya shilingi bilioni moja kwa siku 14; cdm viongozi ni janga ; ingekuwa bora wakakodi ndege ndogo zinazomilikiwa na watanzania na sehemu nyingine kutumia magari.
Wananchi na wanachama tuchukue hatua dhidi ya udhalimu wa viongozi wakati arumeru hakuna maji, karatu, musoma hakuna maji , dawa
bilioni moja ni bajeti ya wilaya nzima .
 
Back
Top Bottom