Uchaguzi 2020 CHADEMA hampati hata jimbo moja hapa Kilimanjaro

Mushi Masawe

Member
Mar 31, 2020
13
13
Huu ndio ukweli wa mambo, Tuliwaamini tukapoteza muda wetu kwa ajiri ya chama. Watoto wetu wameumizwa nyie mmebaki kujaza matumbo yenu tu.

Sasa hatutaki ukabila wala ushabiki tunamuunga mkono Rais Magufuli kama ndugu yetu Mrema alivyofanya.

Mbowe hapa Hai hatumtaki kabisa tena bora aache siasa arudi kupiga mziki.
Magufuli ndio rais mchapakazi tulikuwa na miaka karibu 25 hatujaona treni leo kuna treni inakuja Moshi.

Jana nilikuwa natoka kimara nakuja Moshi daraja la wami linakaribia kukamilika nani awachague nyie tena? Mbowe anajinufaisha na mke wake na watoto wake tu.

Hata huku kilimanjaro tumewachoka hatuwataki tena.
 
Hebu mtuambie tumejiandaaje na Corona/? kuanzia wataalam, vifaa na Dawa. Endeleeni kunywa kahawa kwanza
 
Ulichokosea cha kwanza ni kujiita Mushi Masawe baada ya kufungua id mpya. Hakuna mtu ana surnames mbili.

Pili, haingii akilini mtu ambae hamumtaki anakuumiza kichwa hadi umemfungulia id mpya! Kitendo cha kujiita Mushi Masawe ni kuwa unataka kupambana na Mbowe na una lengo la kujifanya mchaga

Tatu, aliyejenga daraja la wami ni serekali na si Magufuli na juu ya yote ni kazi na wajibu wa serekali kujenga madaraja na barabara na sio privilage kwako ndugu. Wasingejenga ndio una haki kulaumu na si wakijenga, sawa?
 
Hatuna Mushi Masawe. Pia hatuna neno ukabila.
Haya yanaonyesha hii account ni fake.
Tatizo ccm kilimanjaro haitimizi wajibu wao. Imetekwa na wenye njaa wanaojitokeza dakika za mwisho.
Kila kata ina changamoto zake lakini mpaka sasa hakuna mdau mwenye nia aliyefanya lolote.

Sent using Jamii Forums mobile app
Mkuu hiyo ni ID tu isikupe shida!
 
Back
Top Bottom