sirluta
JF-Expert Member
- Nov 28, 2012
- 6,325
- 2,487
Chama cha Demokrasia na Maendeleo [CHADEMA] kama kinavyojiita, ni jina tu hakina demokrasia ya kweli wala hakina maendeleo yeyote.
1. Tangu kuanzishwa kwake ni zaidi ya miaka 20 ambapo mtoto aliyezaliwa pamoja na chama hiki, leo ni kijana ambaye amehitimu chuo kikuu, ana kazi yake na anajitegemea tofauti na chama hiki kinategemea ugali wa shikamoo kwa baba serikali. Je chaweza kuwa chama cha upinzani? Maendeleo waliyo nayo ni yepi kama hata ofisi wameshindwa kujenga?
2. Ni demokrasia ipi wanaizungumzia kama wanachama na hata baadhi ya viongozi hawana sauti na chama kinawanyima uhuru wa kutoa mawazo yao? Mfano wapo wanachama na viongozi wanaovutiwa na kasi ya utendaji wa Dr. JPM ila hawawezi kusema maana chama kitawashughulikia. Hata wapo baadhi ya waliokuwa wanachama walijitoa baada ya kukosekana kwa demokrasia ya kweli ndani ya chama wakiwemo Zitto na Dr. Slaa.
Ni vema chama kikajitathmini na kujitafutia jina linaloendana na hicho chama na kama watashindwa walete mjadala watafutiwe jina maana hiyo demokrasia wanayoisema haipo, na hayo maendeleo pia hawana.
Usiku mwema. Kesho naamkia buku 7 yangu pale lumumba nisiulizwe lakini ujumbe mmeupata.