Kwa kweli mimi nimechoka na nimechoka hizi siasa za Tanzania.Unaweza jutia kuzaliwa Tanzania ambapo kusema uongo na kuusimamia wenzako wanakushangilia,lakini tutakwenda wapi?Yatupasa kuipigania nchi yetu ili pale haki inapostahili ipatikane.
CCM wanatapatapa,hakuna cha maana wanachokifanya.Sasa hivi mikakati yote ni kudidimiza vyama vya upinzani ili yale maovu yasijulikane kwa wananchi.Ndo maana wanajiandaa kupeleka mswada wa kukataza maandamano,na mibunge ya CCM inavyofikilia kwa kutumia Masabuli,wataupitisha lakini wajue wananchi wa karne hii si wale wa enzi za ndiyo mzee.
Mda unakuja ambapo wananchi watasema hapana kwa uonevu,dalili ni nzuri kwa mwananchi wa kawaida kusimama na kuhoji mambo ya msingi,japo ukihoji unaonekana mbaya,lakini ukweli utabaki pale pale.
Heko Dr Slaa wa ukweli,mwenye hekima na busara,asante Mungu kutuletea vijana wanaona mbali,CHADEMA imeweza kuwaamsha wananchi na kujitambua.Songa mbele,wazalendo tuko nanyi japo maadui ni wengi,DAIMA HATAKA KATIKA MAISHA YA KILA SIKU,TANGULIZA MUNGU,ANZA NA MUNGU KWA KILA JAMBO NA MWISHO MALIZA NA MUNGU NA usiwe mnafiki,sema asante MUNGU KWA YOTE ULIYONITENDEA.
Nawasilisha