Chadema + Cuf Umeya Mwanza, Arusha imetegua kitendawili? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Chadema + Cuf Umeya Mwanza, Arusha imetegua kitendawili?

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Candid Scope, Sep 28, 2012.

 1. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #1
  Sep 28, 2012
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  [​IMG] [​IMG]

  Makubaliano ya Chadema na CUF kusafisha njia ya kupitisha Meya wa Chadema na Kaimu CUF ndoa yao ya mkeka imekuja kutalikiwa na sintofahamu ya kinachoendelea Arusha hali halisi inaweza kusomeka hivyo kutokana na kurushiana makombora mazito ya kutuhumiana kwa vurugu za Arusha ambazo zilisababisha mtafaruku dhidi ya CUF kuituhumu Chadema kuvuruga misafara yao, wakati huo huo pilikapilika za uchaguzi Meya Mwanza zikiendelea. Malalamiko ya CUF dhidi ya rough za wafuasi wa Chadema Arusha kuna uwezekano wa kutengua ndoa ya mkeka.

  Tofauti zinazojitokeza sasa hivi Huko Arusha ni dalili tosha kwamba adui mkubwa wa vyama vya upinzani nchini ametumia ufa huo kumrudisha ndani mwandani wake aliyeelekea kuvutiwa na mwingine mpya, lakini wakiwa mkekani kabla hawajavishana pete amemwahi na kumrudisha ndani kwa mtindo wa kiaina.

  Tatizo linalokuja kuonekana wazi ambalo tangu kuanza kwa mfumo wa vyama vingi vya siasa ni pale CCM inapotumia mfumo wa Mwingireza wa
  divide and rule. Vyama vya upinzani vimeonekana kutafuta suluhisho la kufanya pamoja inapohitajika kupata kura. Hali ya kujenga kuungana kiitikadi kwa upeo wa muda mrefu ili kuwaletea ushindi dhidi ya CCM umekuwa mgumu kwa vile mwendelezo wa kuungana kwa msimu ili kukusanya kura ndio mwanya ambao CCM inatumia kunyakua ushindi kama ilivyotokea sasa huko Mwanza.

  Naam, vyama vya upinzani ukata ndio unaovitavuna, wakati vyanzo vya mapato ni kidogo, matokeo CCM rahisi kuwahadaa wenye njaa ili kujirudishia himaya ili kuzidi kujenga hoja ya kujiaminisha nguvu bado wanayo.

  Yeah, ubinafsi nao ukipata nafasi sisi tupate vyote matokeo ndio haya, wenzetu Kenya Mwai Kibaki asingekuwa flexable na wenzake katu KANU isingesambaratika tuonavyo leo. Kuna ya kujifunza kutokana na haya ili kukuza demokrasia nchini, kwani siasa za leo zinaendeshwa kisayansi kuliko wentu tufikiriavyo.
   
Loading...