Ah
Kumbe mandamano ya CHADEMA ni Muhimu
Nimekuwa nikifuatilia hoja zinazoibuliwa na CHADEMA nyakati mbalimbali na pia wakati wa mandamano ambayo Ah
Kumbe mandamano ya CHADEMA ni Muhimu
Nimekuwa nikifuatilia hoja zinazoibuliwa na CHADEMA nyakati mbalimbali na pia wakati wa mandamano ambayo
yamefanyika maeneo mbalimbali ya nchi. Mfano:-
Suala la bei ghali ya bidhaa na ugumu wa maisha: Baada ya Kikwete kuona CDM imeibua suala hili muhimu, alikuja na kusema bei ya sukari ipungue. Baadhi ya sehemu ilipungua na sehemu zingine haikupungua.
Bei ya mafuta (dizeli, petrol na mafuta ya taa): Bajeti ya ahadi iliyowasilishwa hivi karibuni imeonesha kama
inawajali wananchi. Kama serikali ikiweza kusimamia kushuka kwa bei ya mafuta (mfano kufikia 1,600 au 1,800 kwa lita) serikali inaweza kuaminiwa kidogo. Hata hivyo ni kufanyia kazi masuala yanayoibuliwa na CDM.
Suala la mafisadi: Wote tunajua kuwa CCM haina uwezo wa kupambana na mafisadi na kupitia mjumbe wa
Halmashauri kuu ya Taifa ambaye pia ni waziri mkuu, Mizengo Pinda, alisema mafisadi hawawezekani. Lakini kwa sasa CCM inajifanya kuwa inaweza kupambana na mafisadi ili kuwahadaa wananchi. Lakini aliyeibua hoja hii si mwingine ni CDM kwa nyakati mbalimbali.
Katiba mpya: Wakati wa kampeni za uchaguzi mwaka jana na katika mandamano, CDM walidai uandikwaji wa katiba
mpya ni lazima na ikaungwa mkono na wasomi mbalimbali na wapenda uzalendo. Leo hii bado katiba ni suala nyeti
(hot issue) ambalo si la CDM tena bali la kitaifa. Mpaka Tanzania Law Society (TCS) wameunda kamati maalum ya
katiba na taasisi nyingi zinazojihusisha na haki za binadamu zimeanzisha harakati kuhakikisha uwepo wa katiba
mpya ya Tanzania.
Katika mambo hayo yote, kama CDM wasingeandamana, lini selikali ingetoa tamko juu ya hayo?
Itabidi tuanze kuhakiki ahadi zilizotolewa na wagombea kujua zipi zimetekelezwa na nani bado.
yamefanyika maeneo mbalimbali ya nchi. Mfano:-
Suala la bei ghali ya bidhaa na ugumu wa maisha: Baada ya Kikwete kuona CDM imeibua suala hili muhimu, alikuja
na kusema bei ya sukari ipungue. Baadhi ya sehemu ilipungua na sehemu zingine haikupungua.
Bei ya mafuta (dizeli, petrol na mafuta ya taa): Bajeti ya ahadi iliyowasilishwa hivi karibuni imeonesha kama
inawajali wananchi. Kama serikali ikiweza kusimamia kushuka kwa bei ya mafuta (mfano kufikia 1,600 au 1,800 kwa
lita) serikali inaweza kuaminiwa kidogo. Hata hivyo ni kufanyia kazi masuala yanayoibuliwa na CDM.
Suala la mafisadi: Wote tunajua kuwa CCM haina uwezo wa kupambana na mafisadi na kupitia mjumbe wa
Halmashauri kuu ya Taifa ambaye pia ni waziri mkuu, Mizengo Pinda, alisema mafisadi hawawezekani. Lakini kwa
sasa CCM inajifanya kuwa inaweza kupambana na mafisadi ili kuwahadaa wananchi. Lakini aliyeibua hoja hii si
mwingine ni CDM kwa nyakati mbalimbali.
Katiba mpya: Wakati wa kampeni za uchaguzi mwaka jana na katika mandamano, CDM walidai uandikwaji wa katiba
mpya ni lazima na ikaungwa mkono na wasomi mbalimbali na wapenda uzalendo. Leo hii bado katiba ni suala nyeti
(hot issue) ambalo si la CDM tena bali la kitaifa. Mpaka Tanzania Law Society (TCS) wameunda kamati maalum ya
katiba na taasisi nyingi zinazojihusisha na haki za binadamu zimeanzisha harakati kuhakikisha uwepo wa katiba mpya
ya Tanzania.
Katika mambo hayo yote, kama CDM wasingeandamana, lini selikali ingetoa tamko juu ya hayo?
Itabidi tuanze kuhakiki ahadi zilizotolewa na wagombea kujua zipi zimetekelezwa na nani bado.
Karibu kwa nyongeza