ntamaholo
JF-Expert Member
- Aug 30, 2011
- 12,906
- 6,909
HARAKA HARAKA HAINA BARAKA, RPC Kasema wenye taarifa wapeleke nyie mnalazimisha akamate! Amkamate nani!? Kwani yeye alikuwepo kwenye tukio? Aliyekuwepo kwenye tukio ndo wa kutaja ni nani alikuwa na Panga na Shoka na awe tayari kuisaidia Polisi ili mtuhumiwa aweze kufikishwa mbele ya sheria.JF tuwe Great Thinker kweli sio kubwabwaja. Mfano kuna mtu kachangia hapa kwa kumtaja mtu hadi na namba yake ya Gari je, yuko tayari kwenda Polisi kuelezea? Je alishafanya hivyo!? Yuko tayari kwenda mbele ya Mahakama kutoa ushahidi huo!? Au ni chuki binafsi!? JF sio Polisi una uhakika kamuone RPC na ushahidi wako wa uhakika achukue maelezo ayafanyie kazi. Kusema itumike nguvu ya umma bado ni muendelezo wa uvunjifu wa amani kitu ambcho serikali yoyote haiko tayari maana azima itaingia kuwalinde wengine na hapo ndo LOH!
umesema vizuri mkuu.
wengi wanatanguliza ushabiki wa CDM halafu wanatelekeza utafakari wao.
Tanzania mambo yako hivi. Ukitendewa kosa, cha kwanza ni kwenda POLISI kufungua kesi, unapewa RB. Katika kufungua kesi, unataja tukio limetokea vipi, nani alihusika, alitumia nini, walikuwa wangapi na yanayofanan na hayo. ukisha fungua kesi, kinachofuata ni wewe kuonesha ushirikiano kuhakikisha wote waliohusika wanakamatwa. wakisha kamatwa, ushahidi unaandaliwa, wanaandikwa maelezo ndipo kesi inapelekwa kwa mwanasheria wa serikali, baada ya hapo kesi inapelekwa mahakamani na taratibu nyingine zinaendelea.
sasa hawa jamaa, wameshambuliwa usiku, tena wa manane, hatujajua kama wamefungua kesi na kama waliwataja wahusika, lakini wanataka wakamatwe. utamkamata nani wakati hana kesi inayomkabili? kama siyo kumuunea ni nini? fuata utaratibu ili uwe na sababu ya kulalamika.
lakini pia hawa wabunge waje watueleze kwa kina saa nane usiku walikuwa wanashughuli gani kwenye mitaa ya watu usiku