CHADEMA chatoa masaa 36 waliowavamia wabunge wake kukamatwa...

only83

JF-Expert Member
Oct 15, 2010
5,343
2,525
...Uongozi wa CHADEMA mkoani mwanza ukiungwa mkono na uongozi wa kitaifa wa CHADEMA wametoa masaa 36 wahuni na majambazi wa CCM waliowavamia wabunge wa ilemela na Ukerewe wakamatwe.La sivyo nguvu ya umma ifanye kazi.Akiongea na wananchi mbunge Wenje amesema hawawezi kuvumilia kauli zinazotofautiana kila siku toka kwa kamanda wa mkoa wa Mwanza.

Source: Radio free africa.
 
Hili swala la makamanda kucharagwa maanga linakaa kisheria zaidi.Nguvu ya umma itaumiza wengine wasio na hatia.
 
Waliofanya ilo tukio wanajulikana,kwa nini wasichukuliwe hatua?au jeshi la polisi linataka mpaka umma u react ndio waanze kuchukua hatua?hii nchi na taasisi zake bwana!?!!
 
Wenje alimananisha nini aliposema nguvu ya umma itatumika kama alifafanua?
 
polepole kwanza tungeshughulika na wagonjwa mpaka sasa hatujui hatina yao kuliko kupeleka nguvu kubwa kutafuta mchawi
 
Waliofanya ilo tukio wanajulikana,kwa nini wasichukuliwe hatua?au jeshi la polisi linataka mpaka umma u react ndio waanze kuchukua hatua?hii nchi na taasisi zake bwana!?!!

weka wazi majina yao na sisi tuwajue kama wanafahamika
 
polepole kwanza tungeshughulika na wagonjwa mpaka sasa hatujui hatina yao kuliko kupeleka nguvu kubwa kutafuta mchawi

Mkuu wa Porojo umerudi. sasa mapanga mmewakata wenyewe na bado hamjui hatma yao? mpaka jana wameonyeshwa kwenye TV wakiwa wanaendelea vizuri. Au ulitaka usikie wamekufa ndo ujue hatima yao?
Polisi wa CCM ni viazi sana. wanasubiri amri ya amiri jeshi wao ndo wachukue hatua?
Ingekuwa ulaya yngeiona hiyo nguvu ya umma inavyokuwa. Maanadamano mwanzo mwisho na Waziri Nahodha angeshajiuzulu.
Wenje hiyo nguvu ya umma imechelewa sana ilitakiwa iwe ishatoa hukumu.
 
Hili swala la makamanda kucharagwa maanga linakaa kisheria zaidi.Nguvu ya umma itaumiza wengine wasio na hatia.

Mkuu hapo kwenye red nadhani umepotoka au hauishi nchini Tanzania. Sheria huku ni za kuwatetea mafisadi na wanyonyaji na wahalifu walioshindikana. Tukisubiri sheria utakuta upelezi unaendelea mpaka 2020.
 
wanawajua lakini ?, kama wanawajua kwanza waanze kuwataja na wasipokamatwa ndio kwenda plan nyingine..

Hii kamata kamata hii badala ya kukamata mamba unaweza kukuta kenge na mijusi nao wanasombwa...,
 
Hili swala la makamanda kucharagwa maanga linakaa kisheria zaidi.Nguvu ya umma itaumiza wengine wasio na hatia.

Sidhani kama unamaanisha Tanzania unapoongea "kisheria zaidi" Nijuavyo mimi sheria hupindishwa na ndo maana wenzio wameshaanza kusema "walipicharangwa mapanga na wananchi wenye hasira kali walivyowakamata wabunge wakigawa pesa nyumba kwa nyuma".Hebu subiria hizo sheria kama utapata ukweli.....wenje nakupa big up kamanda,lazima nguvu ya umma imshtue RPC afanye haraka kuwaarest watuhumiwa....
 
Ahmed Kilinda wa u.v.c.c.m na mmiliki wa gari no T 397 ANU hao ndio prime suspect, una lingine?

Kamanda wa polisi alitoa kauli mbili tata, ningependa kuwaasa CDM kuacha kutoa au kuamrisha jeshi, wao kama wana ushahidi basi wafuate taratibu zote za kisheria kuuwakilisha panapohusika, nguvu ya umma haihitajiki, mimi naunga mkono wahuni hao wakamatwe,mambo yajieleze yenyewe, ule ukatili kwa wabunge ni wa kutisha, na serikali itoe tamko la kulaani sambamba na kushughulikia jambo hili sio kusema ni vita vya kijadi,mara wabunge walikuwa wanatoa rushwa....
 
Viongozi wa chama haiwezekani kufanyiwa unyama halafu waliowafanyia unyama huo waendelee kudunda mitaani kwa raha zao zote.
Lazima tule nao sahani moja kama sio bakuli moja. Lazima tuwanyweshe maji yaliyochanganywa na sifongo.Kudadadekiiiiiiiiii huu ni unyama mtupu ni nani asiyeuona.
 
sasa kama rpc kawekwa mfukoni na masamaki na gachuma, wht do u expect? badala ya wao polisi kukamata hao wahalifu wanaojulikana, rpc bila chembe ya aibu anasema wananchi wenye taarifa wapeleke...,hii kazi ya nani sasa,, naona ni kama wanakula mishahara ya bure tu! Inaudhi saaana,,

Ukitaka kujua hawa watu(hasa maofisa) hutumika sana na wafanyabiashara wakubwa angalia scale ya mishahara yao then linganisha na utajiri wao.., angalia tibaigana, mahita, hata gewe kipindi kile..,

Hata kama mnatumika na hao wafanyabiashara, mara nyingine mjaribu kutenda haki.., na kitu kimoja ambacho wengi wao hawa mapolisi hawajui..., mtu anayekutumia kwa manufaa yake anakudharau saana, hata kama hakuoneshi kwa vitendo lakini ndani ya moyo wake, you are a very cheap thing!

moshe dayan,
haifa,
 
Back
Top Bottom