CHADEMA chama bora cha siasa Afrika

inchaji

JF-Expert Member
Jul 5, 2019
2,420
4,922
Chama cha demokrasia, CHADEMA, kinabaki na kinaendelea kuwa moja ya vyama bora cha siasa Afrika. ni chama pekee japo hakikushika dola bado, kinakidhi matakwa ya umma na kikatiba ya kuiongoza nchi.

Chama hichi ni mpango wa Mungu. japo wale walioko madarakani wamekuwa wakikisakama
Chama hichi kwa hila nyingi huku wakitumia vyombo ya dola ambavyo kimsingi ni vyombo vya umma, kukiandama, bado CHADEMA kimeendelea kuonesha ustahimilivu na ukomavu wa hali ya juu. wanachama wake ambao ni sisi tunaziishi tunu zilezile zilizoanzishwa na waasisi wa nchi Mwalimu Nyerere na Mzee Karume.

Wanachama wa CHADEMA tumeendelea kuwa wamoja na wastahimilivu katika misukosuko yote ambayo viongozi wetu na chama chetu wanapitia. kila jaribio lenye nia ovu ya kuvuruga umoja wetu Mungu amekuwa akisimama nasi akiwapiga watesi na kuwarudisha kilomita 100 nyuma waanze upya. hakika tunamshukuru Mungu.

Kwa wanachama wenzangu wa CHADEMA tuendelee kuwa watulivu. huku tukimuomba na kumtukuza Mungu siku zote. tukifata maagizo ya viongozi wetu kama tulivyofanya kipindi cha uchaguzi haramu wa serikali za mitaa. mabadiliko katika nchi ni lazima na CHADEMA ni chombo kiteule kwa ajili ya kuleta hayo mabadiliko ambacho Mungu amekileta kwetu. CHADEMA ni tunu ya demokrasia Tanzania. tukitunze kama mboni ya jicho.

Kwa viongozi wetu eleweni kuwa mapambano bado hayajaanza bado. jipangeni kwa mapambano msilale. msife moyo. tupo nanyi katika demokrasia, Ibada na sala. tekelezeni majukumu yenu kwa kadiri ya Katiba ya Jamhuri. Mungu hatawapungukia.

Kwa watesi wetu tunawapa salaam. hila zenu zote tunaziona. hakika mnahaha. mnatia huruma. mmechelewa sana. kuna watu wamekufa, na wengine kunusurika kufa kwa hila wakiipigania demokrasia ya nchi kupitia CHADEMA. hawa hatuwezi kuwasaliti. ni mashujaa wetu. Tanzania itakuja kutuuliza ikiwa tutawasaliti mashujaa hawa. tafuteni namna nyingine ya kupambana na Chama Cha Demokrasia. nawashauri mtafute maridhiano. jambo la hila huwa na halikuwahi kufanikiwa.

Tambueni kuwa kwa kuwa sote sisi ni Watanzania basi sisi na ninyi ni ndugu. mlipo tupo, na tulipo mpo. kuweni wastaarabu. fitna zenu hazifanikiwi na hamtafanikiwa. tupo wengi mno ila tu sisi ni wastaarabu. acheni kusumbua viongozi wetu kwani hakuna mantiki yoyote kwa sababu nyuma ya hao viongozi mnaoweza kuwahesabu kwa vidole kuna kundi kubwa kwa mamilioni ya wanachama. we deserve so much respect please acheni siasa za kipuuzi.

Mungu Ibariki Tanzania, Mungu Kibariki Chama cha Demokrasia, CHADEMA.
 
Haya Mbowe na genge lako njooni mdhibitishe hili povu kama kuna ukweli ndani yake
 
Hakika Mkuu inchaji umeunena ukweli mchungu, ambao hata wenyewe wanaccm, wanaukiri kimoyomoyo ukweli huo.......

Tatizo kubwa kwenye utawala huu wa awamu ya tano, Jiwe anaendelea kuwatia hofu na kuwatisha wote hata ndani ya CCM, ili wasiueleze ukweli huu halisi
 
Back
Top Bottom