CHADEMA, CCM wachuana matangazo ya Televisheni

CHADEMA, CCM wachuana matangazo ya Televisheni

Zanzibar-ASP

JF-Expert Member
Joined
Nov 28, 2013
Posts
12,151
Reaction score
44,071
Vikwazo dhidi ya kampeni za UKAWA za urais zimezidi kuongezeka baada ya vituo kadhaa vya television vya hapa nchini ambavyo vilikuwa tayari vimefanya makubaliano na UKAWA ya kurusha matangazo ya moja kwa moja ya Luninga(Live) 'kuzuiwa' kurusha matangazo hayo kwa madai kuwa CCM nao wanataka siku hiyo hiyo ya Jumamosi warushiwe matangazo yao ya moja kwa moja ya mkutano wao wa kampeni za urais kutoka mkoani Mbeya.
Huu utakuwa ni mwendelezo wa vikwazo dhidi ya UKAWA na mgombea wao wa urais Edward Lowassa.

Mpaka sasa Lowassa na UKAWA hawajazindua kampeni zao, lakini mvuto na ushawishi wao mkubwa umeteka kabisa mwelekeo mzima wa kampeni za kisiasa mpaka sasa.

SOURCE:Gazeti la Mwananchi la Leo.


=======================

attachment.php
 

Attachments

  • Mwananchi.jpg
    Mwananchi.jpg
    125.5 KB · Views: 1,626
Hata wafanyeje wasubiri hasira za watanzania wanaojielewa; sio wale ambao wako lindi la umasikini na wanawapa wali; kesho yake wanawapa kura, ni dharau kubwa sana!!
 
suala la kurusha matangazo ni biashara pale...na mkataba uliopo kwa siku hiyo na kwa muda huo...mimi ninachoona hapa vyote ni propaganda tu.....
 
Kichapo kwa ccm kipo palepale, kwa hali ilipofika ukawa wanaweza kusitisha kampeni ikasubiriwa tarehe ya kupiga kura na tsunami yake ikawa balaa vilevile.
 
Nchi hii ina television moja? Na hao ccm wamelipia TV station zote siku hiyo? Mambo mengine mkiambiwa basi changanyeni na zenu
Unadhani kila tv ina watazamaji zingine zinaishia chalinze au hazina watazamaji.
 
Acheni kusingizia kila uongo kwa ccm. ITV ni wafanyabiashara, anayelipa ndiye anapewa airtime, mwambieni Mbowe awagawie wenzake mgao wa mabilioni ya Lowasa ili kampeni zenu zichangamke sio kujifanya kuminya hela na kuwadanganya wenzake eti anayetia saini (katibu mkuu) hapatikani wakati yupo tu! Hela hawanaaa! Zote kachikichia Mbowe, Msilete visingizio.
 
Kwani hawa CCM si wana Tv station zao, TBC na Star Tv???
 
Ninachoona hapa ni kuwa ukawa wamekuwa Wajanja zaidi ya ccm, baada ya uzinduzi wa ccm keshoye jamaa kaibukia kwenye dala dala aka draw attention ya media na kupunguza mwangwi wa ccm.
 
Nchi hii ina television moja? Na hao ccm wamelipia TV station zote siku hiyo? Mambo mengine mkiambiwa basi changanyeni na zenu
We unaambiwa mwenzako kashabook kwa sababu serikali mnayo eti na nyny mnajifanya mnataka,...mnadhani mtashinda kwa dhuluma zenu?,uwanja wa taifa mmegoma,jangwani mmezingua na kwenye TV mnazingua wabongo tunawacheki tu nahata wana CCM wasiopenda dhuluma hawafurahishwi na upuuzi huo....ila upinzani ni watu wenye akili sana na ndo maana wanawanyima usingizi,hamtaamini kitakachotokea mbna.
 
Back
Top Bottom