CHADEMA, CCM na Serikali Vs Askofu Gwajima

mmh

JF-Expert Member
Nov 9, 2010
2,910
5,081
Huu ni Uzi wa tathimini yangu juu ya yanayoendelea kwa ujumla katika saga la Waziri na Askofu Gwajima.

Siku zote CHADEMA wamekuwa wakiwaomba viongozi wa dini kukosoa na kuikemea Serikali ya CCM. Tumeshuhudia maaskofu kama Mwamakua, Shoo na Bagonza wakioneshwa kuwa mashujaa kwa wanachadema kwa kudiriki kumkosoa mkuu wa nchi au Serikali.

Sasa toka Corona ilivyoingia msimamo wa CHADEMA waliusema na kufikia hatua ya kususia vikao vya bunge wakililia lock down, tukatoboa hivyohivyo.

Sasa toka kipindi kile Askofu Gwajima aliwaombea au aliwaamuru wakose Ubunge ili waiingie wazalendo Bungeni akiwemo yeye. Kweli CHADEMA walikosa na yeye akaingia bungeni.

Imekuja hii issue ya Askofu na Waziri kutofautiana naona CHADEMA wanaisukuma Dola na Serikali imuadabishe Askofu sio kwamba kakosea Bali ndo nafasi walioipata kulipiza kisasi. Kwa sasa CHADEMA wako tayari hata kumkafara mwenyekiti wao Mbowe ili tu Gwajima aadhibiwe yaleyale ya Yesu na Baraba!

Kwa sasa Serikali imekuwa Malaika kwa CHADEMA dhidi ya Gwajima why now!

Fungukeni akili na mkumbuke vizuri sababu zake!

Kama ndivyo mamlaka ziache kabisa kuwasikiliza watu ambao ni biased badala yake izingatie misingi na hoja.

Mkitaka kuwafurahisha CHADEMA wanataka kuona majembe ya serikali na chama yote yanaparaganyika ili wapate wepesi.
 
Mkuu kichwa Cha habari ungekiandika hivi,

Chadema Vs Dola / Polisi ,na CCM vs Bunge /Serikali,

Maana mpinzanza wa Chadema ni vyombo vya Dola,na CCM mpinzani wake ni wabunge na mawazili
 
Back
Top Bottom