- Matukio ya hivi karibuni kati ya Wabunge Nassari na Shibuda, yanaleta maswali magumu sana kuliko majibu yake. Ninasema hivi CCM wasipuuze maneno ya Nassari na pia Chadema wasipuuze maneno ya Shibuda wayatafakari na kuyafanyia kazi, mifano ipo mingi sana kwa mfano kuna wakati hatukutaka kuongelea katiba wala Muungano, lakini sasa wakati umefika ambapo ukweli upo wazi kwamba tungenongea haya kule nyuma, saa hizi tungekwua mbali sana.
- So Chadema na CCM, wasiwapuuze Nassari na Shibuda, kwa sababu reading between the lines kuna ujumbe mzito wa kisiasa kwenye maneno yao.
William.
Sibuda chdema wamesha m-paralyse, alichoongea Nassari si mnachotafsiri.Ni mitizamo mliyokuwa nayo vichwani ndio yamepelekea kuwa na tafsiri hiyo haraka.Na ni ngumu kuwabadili.
Ila CCM wajue kuwa watoto wadogo wa shule huwa sometimes CCM na serikali yake wanapofanya upuuzi ,huwa kajiografia chao kadogo kanawapeleka jiuliza kwanini bandari ya Tanga, istumike saidia ukanda unaoanzia tanga,Kili, Arusha hadi mwanza?Hata mimi miaka yote nimekuwa naona maamuzi yanayofanyika hapo dar huwa hayafai ukanda huu, na hata watu wa Mbeya mpaka katavi wanaona hivyo. So si mbaya pia mkaona na kutambua habari ya watu wa north kujiona kuwa wangefanikiwa zaidi nje ya bla blah za DSM.
Chukulia mfano wa utalii? mawaziri wengie hawajui hata aina 5 za utalii, ndio maana watu kibao .wanshangaa serikali haijaona kuwa dara inaweza fanya utalii mkubwa kuliko hata bagamoyo, achilia mbali madini km Tanzanite, mikataba imeingiwa hapo magogoni ila inaathiri watu wa Kaskazini na uchumi wa nchi.na masuala ya ardhi ,hao wa magogo manadhani mzungu ni km mchaga anayemvua mzaramo nyumba Kariakoo.Wazungu wakichukua maeneo wanafanya kila kitu private. private road, private water source, etc.Na yote haya yana maanisha kuingia ktk mtaa tuu na si nyumba ya mtu binafsi unaihitaji permit.
Magogoni hawajaona matukio mabaya nje ya pua, beaches zote dar mafisadi wanajenga wanaziba njia ili masikini wasifike huko na ikibidi hata serikali isifike huko,ndio maana kuna bandari kibao haramu.Yote haya yanaashiria tofauti za mitizamo na vipaumbele ktk maisha.
kuna mambo yanatia kichefuchefu km kupata documents, kupata huduma za bandari lazima uje dar na mara nyingine unamkuta mtu kachoka kifikra na hajui unachotaka akusaidie kwa vile ni nje ya fikra zake ila ndio hivyo ana mamlaka.Kwa nini sasa uhitaji kuwa na dar.Halafu unasikia kauli kuwa watu wa kaskazini hawatashika nchi nahakuna anayekuja kemea au kuomba radhi hadharani?
Nakumbuka those days primary school tuliongea sana hiyo mambo ktk honest discussion za kitoto.Tulipokuwa tunakosa nafasi za kusoma Kilimanjaro, wakati wazazi wetu wamechangisha fedha, rasilimali kma mawe,mbao na nguvu ili kujenga shule wakati wengine wanacheza ngoma na bao.Halafu suala la shule tunaambiwa kuna quota.So majimbo nimore natural, kwani jimbo litakalo laza damu litaomba msaada ktk federal government na ikiwa mara nyingi then jitihada maalumu zifanyike.
Off course nilikuja kuwa brainwashed na elimu ya magamba na kuzikubali siasa za kivivu na za upendeleo.ndio maana ukinagalia kwa makini mali za huyo mnene wa magogoni utaona kuwa, pamoja na kuwa madarakani miaka kibao,utagundua kuwa hakuweza tengeneza hela nyingi km alivyopata miaka hii 10 aliyokuwepo na si kwa uwekezaji makini ktk uchumi binafsi.Kaskazini watu wanatengeneza hela popote kuanzia uza pua za ng`ombe mpaka baishara rasmi.