CHADEMA Bunda Mjini 2015, Kama anguko CCM Iringa Mjini 2010

Ngurudoto

JF-Expert Member
Mar 13, 2008
208
26
Chadema Bunda yabomoka vibaya

-Robo tatu ya viongozi wa kamati tendaji wajihudhuru nyadhifa zao
-Wasema chanzo ni Esther Bulaya kubebwa na viongozi wa juu wa chama hicho
-Wasema wamekitumikia chama hicho na kuwekwa ndani lakini sasa hawathaminiwi


Na Ahmed Makongo, Bund | Mtanzania | Agosti 20, 2015

CHAMA cha Demokrasia na maendeleo (Chadema) katika Wilaya ya Bunda, kimepata mpasuko mkubwa kutokana na jana karibu robo tatu ya viongozi wake kujihudhuru nafasi zao, akiwemo katibu mwenezi wa Chadema jimbo la Bunda Emmanuel Malibwa, mwenyekiti wa jimbo hilo Samwel Alfred na katibu wa Chadema Wilaya Rita Itandilo.

Baadhi ya viongozi hao pamoja na baadhi ya wanachama wa chama hicho walisema kuwa sasa hivi watamuunga mkono mgombea wa CCM katika jimbo la Bunda Stephen Wassira, kwa sababu viongozi wao wamejichanganya sana, kwa kuwafanyia maamuzi ambayo siyo sahihi.

Habari zinasema kuwa chanzo cha viongozi hao kujihudhuru nafasi zao ni aliyekuwa mbunge wa viti maalumu kundi la vijana kutoka mkoani Mara, kupitia tiketi ya CCM Esther Bulaya, aliyejiunga na chama hicho hivi karibuni na kuteuliwa kuwa mgombea wa ubunge katika jimbo la Bunda mjini kupitia tiketi ya Chadema, huku aliyeshinda kura za maoni Pius Masururi akikatwa jina lake.

Viongozi hao walisema kuwa kwa mjibu wa katiba uteuzi wa mbunge huko kwenye kamati kuu, lakini walivyowaletea Esther Bulaya yeye alikuja na uongozi wake bila ya kuwashirikisha viongozi waliokuwepo na kwamba kwa jinsi hiyo wameamua kujihudhuru nafasi zao na kumwachia viongozi aliokuja nao.

Viongozi hao pamoja na wa kamati tendaji na baadhi ya walinzi, wakifuatana na wananchama wa kawaida zaidi ya 70, wamejihudhuru nafasi zao kwa kile walichodai kuwa viongozi wa chama hicho wakiwemo wa ngazi ya juu wameivunja katiba ya chama hicho kwa makusudi.

Wakizungumza na waandishi wa habari jana katika hoteli ya Green Guden, mjini Bunda viongozi hao walisema kuwa wameamua kujihudhuru nafasi zao na kubakia wanachama wa kawaida kwa sababu viongozi wao wa Mkoa, kanda na Taifa wamekiuka katiba ya chama hicho.

"Kwa kile kilichotokea kupitia uongozi wetu wa mkoa, kupitia katibu wetu wa Chama Mkoa Chacha Heche na mwenyekiti wetu wa Mkoa wameshindwa kujua jimbo la Bunda msemaji wa chama au Mkoa ni nani wao badala ya kufuata katiba wameshindwa kujua katiba inasemaje kuhusu malalamiko yoyote.

"Wao badala ya kuona katiba inasemaje na kanuni za chama zinasemaje na taratibu zinasemaje kuhusu malalamiko yoyote kama yalikuweo ili waweze kuyafanyia kazi, lakini kilichofanyika ni udhalilishaji na maamuzi ambayo kamati tendaji ina mamlka ya kuyafanyia kazi, kupitia viongozi hawa ambao leo wanatoa matamko, mimi huwa sikubali kutokuonyesha msimamo.

"Mimi siku zote huwa napenda kuwa muwazi leo nafikia kuchukuwa maamuzi haya magumu, mimi ni mwanchama mwaminifu wa Chadema nimekitumikia chama kwa kipindi cha miaka zaidi ya kumi, lakini leo Bunda imekuwa shamba la bibi, maamuzi ya mtu ndiyo yanayokuja kulitengeneza jimbo la Bunda, kamati tendaji ya jimbo la Bunda ilifanya uteuzi wake wa awali kupitia kura za maoni.

"Walimaliza kura za maoni wakaenda kwenye kamati tendaj,i mimi kama katibu wa Wilaya naletewa mapendekezo ya kamati tendaji ndiyo ninayAfanyia maamuzi, nilichukuwa majina ya wsagombea nikayapeleka kwenye tume kwenda kuyawatambulisha, lakini kilichotokea Mkoa na Kanda na Naibu Katibu mkuu wakatoa maelekezo mengine mbadala, akaletwa mtu ndani ya ofisi yangu bila kunishirikisha wala hata kupewa barua ya kunitambuliusha.

"Lakini kilichofanyika huyo aliyeletwa akaanza kunielekeza lakini mimi kama katibu wa Wilaya ninayejua utaratibu nilikataa, lakini kilichotokea nikiingia ofisini kwangu pale naonekana kama mimi ni mgeni au mtuanayehitaji huduma pale, na kilichotokea wakachonga mhuri mwingine wakatengeneza mhuri ndani ya mhuri mwingine.

"Ndicho kilichopelekea leo hii nimeamua kuchukuwa maamuzi magumu kama mwanamke na nimeamua kujihudhuru nafasi hii ya katibu wa wilaya Chadema nitabaki kama mwanachama wa kawaida isije ikaonekana mimi ndiye nimesababisha chama kushindwa"alisema.

Naye mwenyekiti wa jimbo la Bunda, Samwel Alfred, alisema kuwa "mimi kama mwenyekiti wa Chadema jimbo nimeamua kujihuduhuru uenyekiti wangu wa jimbo la Bunda na nimeamua kujihudhuru uenyekiti wangu wa mtaa, kwa sababu kuna vitu vilivyonikera baada ya kuona kuna watu wanavunja katiba.

"Cha kwanza tulipiga kura za maoni wakapatikana washindi watatu wakiwemo wawili ambao waamekitumikia chama, lakini cha ajabu wakarudisha jina la mshindi wa tatu (Esther Bulaya), hawakuvunja katiba, lakini cha ajabu aliyerudishwa hakuonyesha ushrikiano na viongozi waliokuwepo, kwa kuhofia kuwa walikuwa kambi nyingine kwamba watasababisha ashindwe." Alisema.

Aliongeza kuwa pia kwa upande wa wagombea udiwani wagombea waliopendezwa na kamati tendaji pia majina yao yalibadilishwa na viongozi wa mkoa, kanda pamoja na Naibu katibu mkuu Zanzibar Salum Mwalimu, ambapo yaliletwa majina ya wagombea wengine na kuondolewa wale waliokuwa wameshinda na kupitishwa na kamati tendaji ya jimbo.

"Mimi kama kiongozi niliyepigania chama hiki niliyepata kesi nyingi nimekaa magereza, nimenyanyaswa nimepigwa na nimedhalishwasana, leo hii nimeamua kujihudhuru lakini siyo kwamba naondoka peke yangu naondoka na makamanda wakiwemo wajumbe wa kamati tendaji na katibu wa Bavicha, kwa hiyo robo tatu ya kamati tendeji yote tumejihudhuru.

"Hata wenyeviti wa kata, viongozi wa vijiji, vitongoji wote wameamua kujihuduhuru, najua makamanda wataumia sana maana wanakitaka sana Chadema, lakini kiongozi aliyeletwa kugombea ameshindwa kutambua mchango wa viongozi hawa waliokipigania chama na kufikia hatua hii sisi tumeamua tumpishe ili ashinde salama' alisema.

Katibu mwenezi wa Chadema jimbo la Bunda, Malibwa alisema " Mimi kama katibu mwenezi wa Chadema jimbo la Bunda natangaza rasmi kuwa nimejihuduru nafasi yangu hiyo ya uenezi, na wafuasi wangu wote ambao niliwashawishi wakaingia Chadema leo watambuwe kuwa nimejihudhuru nafasi hiyo nitabaki kuwa mwanachama wakawaida tu.

"'Na sijaondoka peke yangu kama mnavyoona hapa ndugu waandishi wa habari tunao viongozi wote wa kata 20 za jimbo la Bunda, wakiwemo wenyeviti wa kata, makatibu wa kata, kwa ujumla kamati tendaji ya watu 17, mimi mwenezi, mwenyekiti wangu na wajumbe wengine tumeondoka imebaki na watu watatu tu" alisema.

Alisema kuwa yeye pia alikuwa ni mgombea udiwani wa kata ya Nyamakokoto na alikuwa tayari amechukuwa fomu katika ofisi ya Tume, lakini sasa hatarudisha fomu hizo na kwamba kutokana na utaratibu huo kuvunjwa na viongozi wao kwenye baadhi ya kata kuna wagombea wawili wa Chadema ambao tayari wameshachukuwa fomu za Tume kuwania nafasi hiyo.
Viongozi hao walisema kuwa pamoja na kujihudhuru watapiga kura zao katika uchaguzi mkuu ujao.

Wakati viongozi hao wakisema wamejihudhuru nyadhifa zao viongozi wa Chadema, akiwemo mmoja kwa niaba ya katibu mkuu wa Wilaya Kaunya Yohana, alisema kuwa viongozi hao wapatao kumi na moja hawajajihudhuru kama walivyodai bali wamesimamishwa uongozi kwa sababu mbalimbali, ikiwemo kupandikiza wagombea bila taratibu, rushwa na kukiuka maadili na kanuni za chama hicho.

Source: Gazeti la Mtanzania 21/08/2015

View attachment 278672
View attachment 278673
image.jpg
 
Bunda bila wasimbe inawezekana! Pius ndiyo alikuwa Chagua la Mungu, Esther Bulaya Musimbe
 
utakuwa chizi km utafananisha ccm ya iringa mjini na chadema ya bunda mjini!..,chadema inatafuta jimbo bunda hailitetei
 
Mamluki kutoka CCM watatuulia Chama tuwe makini na mtandao wa stven wassira jamani. Tumepata mkombozi halafu tunahadaika please tutulie makamanda
 
Aliyekuwa mshindi wa kura za maoni Bunda Mjini wa CHADEMA, Pius Masururi ametangaza kukihama chama hicho na kujiunga CCM huku mwenyekiti wa jimbo hilo, Samuel Imanani na wanachama 50 wakiwamo viongozi wakijivua uanachama.

Masururi, aliyepata kura 65 mbele ya wapinzani wake wa karibu, Magembe Makoye (40) na Ester Bulaya (37) katika kura za maoni zilizopigwa Julai 29 mwaka huu, ametangaza uamuzi wake huo jana kupitia kituo cha redio cha Mazingira FM cha mjini Bunda.

Masururi amesema ameamua kukihama chama hicho baada ya kutofurahiswa na kitendo cha Kamati Kuu ya CHADEMA kupuuza uamuzi wa wanachama kwa kukata jina la aliyeshinda kura za maoni.

Katika jimbo la Bunda Mjini, CHADEMA imebadilisha matokeo na kumteua mshindi wa tatu, Ester Bulaya kupeperusha bendera ya chama hicho, jambo lililowaudhi baadhi ya makada wake.

Baadhi ya wanachama walioongozwa na mwenyekiti wa jimbo hilo, Samuel Imanani wamesema kitendo cha makao makuu ya CHADEMA kutengua uamuzi wa kura zao za maoni ni udhalilishaji mkubwa, hivyo hawana budi kukihama chama hicho.

"Tumeamua kuuachia uongozi wa makao makuu uendeshe mambo yote, nasi tusiwe tena wanachama maana hautusikilizwi," alisema Mashaka Kipili mmoja wa wanachama hao.

Chanzo: Radio Mizingira Bunda.

 
Duh ! Habari ya tangu jana hapa JF, wewe unaileta leo saa tano halafu unaiita breaking news !.
 
Na katibu CHADEMA Wilaya ya Bunda nae nilimsikia Clouds FM, kaachia nafasi yake na kubaki kuwa mwanachama wa kawaida.
 
Tupo na Ester Bulaya 2015✌✌hao wengine ni njaa tu....

Sasa kweli Nani mwenye Njaa..Hii picha ya Bulaya Ktk ofisi ya CHADEMA Bunda ni kama picha ya Hofu na Msiba Fulani....atakuwa anajuta "hivi huku nimekuja kufanya nini kustaili aibu Hii"
 
Back
Top Bottom