CHADEMA Arusha kwatifuka

Crashwise

JF-Expert Member
Oct 23, 2007
22,227
8,735
Wafuasi wa madiwani wanaounga mkono mwafaka wafunga ofisi ya CHADEMA ARUSHA...picha na video zinakuja
 
Last edited by a moderator:
Niliona maandamano yao leo maeneo ya kaloleni na mabango makubwa, ya kukashifu chama. hali siyo hali, sikujua walikoelekea, nilipita na mkebe changu yaani ujumbe ulikuwa mzito kweli
 
Hii trick ya kununua madiwani wa CHADEMA itafutiwe dawa mapema
naona inakula sana, hapa magamba wameshika pabaya watu wana njaa
kuna tatizo sehemu tena kubwa madiwa wachunguzwa mienendo yao
wabunge mko wapi?
 
Niliona maandamano yao leo maeneo ya kaloleni na mabango makubwa, ya kukashifu chama. hali siyo hali, sikujua walikoelekea, nilipita na mkebe changu yaani ujumbe ulikuwa mzito kweli

Mkuu, kwani wananchi wengi katika jiji la Arusha wapo upande gani upande wa madiwani au upande wa chama?
 
wakuu sitawe kutuma picha wala video kwa leo ila nitafanya hivyo kesho kama ngereja ataniruhusu maana leo wakati jaribu ku-upload kwenye youtube ngereja akafanya kazi yake..maandamano yalihusisha pikipiki nne na gari moja la jamaa moja majengo ya juu kwajina ni mbuya huyu ni mtu wa bayo na katibu wakata ya kaloleni
 
hii trick ya kununua madiwani wa CHADEMA itafutiwe dawa mapema
naona inakula sana, hapa magamba wameshika pabaya watu wana njaa
kuna tatizo sehemu tena kubwa madiwa wachunguzwa mienendo yao
wabunge mko wapi?

Hebu tuwe wakweli haya ni matokeo ya viongozi cdm kulewa madaraka ya nguvu ya umma inyohitaji zaidi maamuzi ya pamoja/kwa maslahi ya wengi, badala ya kujiona wao <viongozi> ndiyo wenye maono< hawataki kitu kinaitwa Collective decision< kuamini maamuzi ya wengine> hapo hakuna mchawi> wala mnunuzi> wala mteja> kwani hiyo ndiyo gharama ya mgema akisifiwa kutia maji siku zote.
 
Huwa kila siku nasema,
Upinzani Tanzania badoo kabisa!
Tuendelee kujenga umoja wetu na CCM yetu! Hawa wanaoenda upinzani siyo kwamba wanapenda sana maslai ya TZ but ni kutokana na uchu wao wa madaraka hasa baada ya kuenguliwa CCM!
 
wakati wakitoka kufunga ofisi zilizoko kwenye jengo la namvua plaza huku wakibandika mabango yenye maneo ya kuutaka uongozi wa chadema mkoa uachie ngazi na lingine likisomeka taizo la Arusha ni Mh lema bila kufafanua.

Baada ya hapo wafuasi wa upande wanaopinga walianza kumiminika kuona hivyo waasi hao walikimbia huku moja akiacha gari lake na dereva kuna watu walitaka kulichoma moto ndipo dereva alipo liondoa sehemu hiyo
 
Chadema msihangaike na hao walio nunuliwa, wala wasiwa sumbue ni mbaki na madiwani wachache wasio lubunika kuliko kuwa na mizigo ambayo haina maana ktk chama.
 
Mkuu, kwani wananchi wengi katika jiji la Arusha wapo upande gani upande wa madiwani au upande wa chama?
Idadi yao ilikuwa haizidi 30, nadhani ni wale walioshiriki sherehe ya kupongezana pale ukumbi wa manispaa. In fact 98% wanapinga muafaka wa kichina
 
  • Thanks
Reactions: FJM
Huwa kila siku nasema,
Upinzani Tanzania badoo kabisa!
Tuendelee kujenga umoja wetu na CCM yetu! Hawa wanaoenda upinzani siyo kwamba wanapenda sana maslai ya TZ but ni kutokana na uchu wao wa madaraka hasa baada ya kuenguliwa CCM!
Acha zako na wewe kwani UVCCM Arusha hawakuandamana na kutaka kuchoma moto jengo la CCM Mkoa kutaka kumtoa Mary kitanda.
 
Saa hizi ni usiku unataka ofisi ziachwe wazi acha wafunge watafungua asubuhi.
kwa tarifa nilizo zipata baadhi wamesha kamatwa mbaya zaidi wengi wao hana hata kadi yaani si wanachama..
 
Back
Top Bottom