CHADEMA acheni kukopi na kupest toka CCM | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

CHADEMA acheni kukopi na kupest toka CCM

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by kilombero yetu, May 27, 2011.

 1. k

  kilombero yetu JF-Expert Member

  #1
  May 27, 2011
  Joined: May 6, 2011
  Messages: 1,007
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Kamati kuu, ilani, kamati ya maadili na mengine mengi na sasa mnataka kufungua tawi eti UK kisa CCM nao wamefungua. Udokta wenu uko wapi mnashindwa kuja na mfumo mwingine tofaut kabisa? Ndio maana mm nimehama CHADEMA koz hapo juu kuna watu watatu chama wanafanya kama kampuni yao.

  Nafasi zakusomesha vjana wao ndowana kauli ya mwisho mfano kimemo alichokuja nacho puye toka kwa mkubwa akapewa cheki wakati kuna vijana kibao wapiganaji hawapewi hata vocha kuwasaidia vyuoni. Majina ya nafasi ya BAVICHA tayari mlishasema eti yeyote mwenye harufu ya Ztto, Mpendazoe, Wangwe na Dk Safari jina alitakubaliwa.

  Nakwambia kwa ninayoyajua toka CHADEMA hamtafika mbali, kumbuka Dk Slaa wakati wamjadala wakatiba Karimjee pale nyuma ya gari yako ulikuwa ukiongea nini kuhusu Zitto na Mbowe kwa simu wakati unaongea na Lema kuhusu mgombea urais wa CHADEMA 2015.

  Acheni kuwahadaa watz eti mnatetea haki na kwambieni kama si hekima za mzee Baregu hapo nikundi la walafi tu linalowaonea wivu CCM nalo likitaka kwenda likale tu.
   
 2. Kachanchabuseta

  Kachanchabuseta JF-Expert Member

  #2
  May 27, 2011
  Joined: Mar 8, 2010
  Messages: 7,290
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 135
  [​IMG]
   
 3. o

  olng'ojine Senior Member

  #3
  May 27, 2011
  Joined: Dec 2, 2010
  Messages: 119
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Na bado..mpaka magamba yawatoke.
   
 4. Augustine Moshi

  Augustine Moshi JF-Expert Member

  #4
  May 27, 2011
  Joined: Apr 22, 2006
  Messages: 2,214
  Likes Received: 316
  Trophy Points: 180
  Yaani "Tumaini Letu" unataka CDM isitumie hata maneno ya Kiswahili kama "ilani", eti kwa vile yametumiwa na CCM. Kwani "Kamati Kuu", "Kamati ya Maadili", etc ni vitu mimevumbuliwa na CCM? Warusi, Wachina, etc nao wamekuwa na hizo kamati (kwa lugha zao).

  Zamani kulikwa na Chama kimoja tu, na neno CHAMA maanake ilikuwa ni CCM. Kwa logic yako, CDM hawatakiwi kutumia neno chama kwa sababu watakuwa wamenakili toka CCM!

  Naona utakuwa mmojawapo wa wale waliotumwa siku za karibuni kuja hapa baada ya CCM kulalamika JF inakimaliza. Huvui kitu hapa!
   
 5. Matola

  Matola JF-Expert Member

  #5
  May 27, 2011
  Joined: Oct 18, 2010
  Messages: 36,045
  Likes Received: 13,277
  Trophy Points: 280
  CCM itapona kwa kuiga CHADEMA?
  [​IMG]

  Ansbert Ngurumo

  SINA ugomvi na kaulimbiu ya zamani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) – "zidumu fikra za mwenyekiti."

  Katika maisha ya sasa ya CCM hii inayoporomoka, inayotapatapa, inayojivua gamba na inayoishi kwenye kivuli cha kauli ya hayati Horace Kolimba kwamba "haina dira wala mwelekeo," kaulimbiu ile ina maana sana.

  CCM ya sasa imeishiwa fikra. Haina tanuri la kuzalisha mawazo mapya. Lakini imeweza kuzalisha na kutunza mitambo ya makombora ya fitina za kisiasa.
  CCM hii legelege, iliyozaa serikali goigoi, kwa muda sasa imejigeuza chama cha wanachama wanaokulana wao kwa wao.

  Kama alivyowahi kusema mtu mmoja mahali fulani, CCM hii imekuwa mithili ya dume zee la ng'ombe linalopenda kupanda madume badala ya majike.
  Wafugaji wanaelewa dume la namna hiyo linapokataa jike, na likakosa dume la kupanda, hujigeukia na kujifanyia mzaha gani!

  CCM isiyo na mawazo mapya, inashindwa hata kunakili au kuboresha fikra ilizoachiwa na waasisi wake. Kwanza imeziua, na sasa imeanza kurukia na kudandia fikra na mipango ya wapinzani wake. Hii ni CCM inayojimaliza.

  Si hilo tu. Hata vile inavyoviiga kwa wapinzani, inavitekeleza kwa kubabia, bila umakini na weredi wa kuviboresha.

  Nitatoa mifano michache. Baada ya kusikia Rais Jakaya Kikwete anazindua Bodi ya Taasisi ya Uongozi, wiki hii kwenye Hoteli ya Movenpick, Dar es Salaam, kumbukumbu zangu zilinipeleka hadi Desemba 10, 2010.

  Siku hiyo, katika Hoteli ya Kilimanjaro Kempiski, Dar es Salaam, Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe, kwa niaba ya uongozi wa CHADEMA, alitangaza nia yao ya kujenga Chuo cha Mafunzo ya Uongozi, kama njia ya utekelezaji wa azima yao ya kuondoa ombwe la uongozi nchini. Si chuo cha viongozi wa CHADEMA, bali cha kitaifa. CHADEMA walikuwa waasisi tu wa wazo, ambalo walilitangaza siku hiyo.

  Katika kuenzi mchango wa mwana CCM mmoja ambaye amejipambanua kwa kuchangia ukuaji wa upinzani, kupitia CHADEMA, Mustafa Sabodo, wakaamua kuita chuo hicho The Mustafa Sabodo Academy of Leadership and Excellence.

  Mustafa Sabodo mwenyewe alikuwapo. Alikubali jina lake litumiwe, na alichanga kianzio cha sh milioni 150 papo hapo kwa ajili ya ujenzi wa chuo hicho.

  Nia ya CHADEMA, kama ilivyotangazwa na Mbowe, ni kukabiliana na ombwe la uongozi kwa kuandaa viongozi werevu na waadilifu kwa ajili ya uongozi wa taifa hili na taasisi nyingine za kitaifa na kimataifa.

  Siku hiyo hiyo, CHADEMA walimtunuku Sabodo medali ya ujasiri na nia njema; maana
  si kawaida kwa mwana CCM kuchangia upinzani. Sabodo alikuwa ameichangia CHADEMA sh milioni 200 wakati wa kampeni za mwaka jana.

  Walimshukuru na kumpongeza kwa kuunga mkono harakati za mabadiliko chanya katika siasa za Tanzania, na kwa ujasiri wa kujitokeza, tofauti na wafanyabiashara wengi wanaotumika kuhujumu harakati za mabadiliko.

  Miezi mitano baadaye, Mei 18, 2011, Rais Jakaya Kikwete amezindua Bodi ya Taasisi ya Uongozi, inayotarajiwa kuwa kituo cha maendeleo ya uongozi.

  Ni wazo zuri, lakini nani anaamini uwezo wa serikali hii katika kuanzisha na kusimamia taasisi makini ya viwango hivi, kama watawala wale wale wameua, na wameshindwa kusimamia taasisi ndogo ndogo zilizokuwapo?

  Inawezekana wameibuka upya kwa sababu ya wazo la CHADEMA? Je, kwa kuiga huku wataweza kulitekeleza kwa ufanisi? Nguvu hii ya rais na serikali isingefaa kuunganishwa na walioasisi wazo la awali ili kuleta ufanisi mkubwa zaidi katika chuo kimoja chenye hadhi na umakini?

  Wasiwasi wangu ni huu: watawala wale wale walioasisi ombwe lile lile, wakiachiwa peke yako kujenga vyuo vya namna hii, wanaweza wakatumia fursa hii kujenga misingi ya kusimika na kutaasisisha ombwe la uongozi. Maana walioshindwa uongozi hawawezi kusimamia taasisi ya uongozi.

  Kuiga si kosa, kama wanaoiga wanaweza kulikuza na kuliboresha wazo la awali. Je, hawa wana uwezo huo? Kama wameanzisha taasisi hii kwa nia njema, si kuipiku CHADEMA, basi, waifanye taasisi ya taifa, si ya serikali, si ya CCM.

  Na waijenge pole pole, isije kuwa mithili ya shule za kata zinazojivunia wingi wa watoto na idadi kubwa ya sifuri katika mitihani ya taifa.

  Upo mfano mwingine. Katika kampeni za uchaguzi mkuu mwaka 2010, ilani ya CHADEMA ilisema wazi kwamba kama kingepata ridhaa ya kuunda serikali, kingefumua mfumo wa uongozi na kuufuma upya.

  Kwa kuanzia, ndani ya siku 100 za kwanza, kingeanzisha mchakato wa mabadiliko ya katiba, ili ipatikane katiba inayoendana na matakwa ya sasa kisiasa, kijamii na kiuchumi, hasa kwa kuzingatia kuwa mabadiliko ya mfumo yanajikita katika muundo wa katiba.

  CCM ilikejeli azimio hilo la kuunda katiba mpya. Hata baada ya uchaguzi, CHADEMA iliposhinikiza serikali ianzishe mchakato wa kuandika katiba mpya, serikali ilisema hakuna haja.

  Waziri wa Sheria na Katiba, Celina Kombani, alikataa katakata, akaisifia katiba iliyopo; akawakejeli wanaodai katiba mpya, akasisitiza haiwezekani. Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Jaji Frederick Werema, naye akaunga mkono hoja ya Kombani, kwamba hakuna haja ya katiba mpya.

  Baada ya shinikizo la umma kutaka katiba mpya, Waziri Mkuu Mizengo Pinda, na Rais Jakaya Kikwete wakaamua kutekeleza madai ya wanamageuzi.

  Rais Kikwete akakiri kwamba baada ya miaka 50, Tanzania inastahili kuwa na katiba mpya. Akaamuru serikali ianzishe na kusimamia mchakato huo.

  Matokeo ya kuiga bila kujipa muda wa kujifunza tumeyaona. Mchakato wenyewe umeanza vibaya kwa serikali kuandaa muswada wa sheria wenye kasoro zile zile zinazosababisha madai ya katiba mpya.

  Wasiwasi wangu ni huu: CCM inaiga mipango ya wapinzani bila kujiandaa vema. Na kuiga huku kunaanza kuwafanya wananchi wahoji: kama CHADEMA wana mawazo mazuri hivi hadi CCM inayaiga, hata kuacha kutekeleza ilani yake ya awali, ni nani anaongoza nchi hii?

  Tusisahau kwamba CHADEMA ndicho kiliasisi mpango uitwao ‘Operesheni Sangara' kwa ajili ya kujijenga na kuinua hamasa ya siasa za upinzani vijijini. Mkakati huo umekiwezesha kukua kwa asilimia 400 kwa muda mfupi.

  Matunda ya awali ya Operesheni Sangara yalionekana kwenye uchaguzi mdogo wa Busanda, Biharamulo na Tarime. Uchaguzi Mkuu uliopita ni ushahidi mwingine wa matokeo ya Operesheni Sangara.

  Nguvu hiyo ya Operesheni Sangara ndiyo ilivifanya vyama vingine navyo viige mkakati kama huo na kuupa majina yanayoshabihiana nao.

  Kwa mfano, CUF waliibuka na Operesheni Zinduka. CCM nao wakaiga, wakatengeneza kitu kinachoitwa Operesheni Chakaza! Kama CCM imekosa ubunifu kwa viwango hivi, si ni dhahiri kwamba hawakuwa na makosa kuimba zidumu fikra za mwenyekiti? Maana sasa tumegundua kwamba ndiye pekee aliyekuwa anasumbua kichwa chake kufikiri na kuweka dira na mipango mkakati ya chama.

  Mwaka 2005, CHADEMA walibuni utaratibu mpya wa kufanya kampeni kwa kutumia helikopta. CCM wakadhihaki, wakasema ni matumizi mabaya ya pesa.
  Lakini CCM walilazimika kulamba matapishi yao wenyewe katika uchaguzi mdogo wa Tarime, na baadaye katika uchaguzi mkuu wa 2010.

  Badala ya helikopta moja, wakakodi tatu na kubwa kuliko za CHADEMA. Kumbe CHADEMA waliona mbali?

  Tukumbushane pia, kwamba hata Chuo Kikuu cha Dodoma, kimetokana na wazo la CHADEMA. Mwaka 2005, mgombea urais kupitia CHADEMA, Mbowe, alitoa matamko mawili makubwa yaliyonakiliwa na CCM baada ya uchaguzi.

  Akiwa katika mji wa Merererani (Mkoa wa Arusha wakati huo), Mbowe alisema kama CHADEMA kingeingia madarakani, kingepitia upya mikataba ya madini nchini, ili kuondoa unyonyaji unaofanywa na serikali na wawekezaji dhidi ya wananchi maskini.

  Mwaka 2008, serikali ilipobanwa vilivyo, ikaamua kuunda Tume ya Bomani kwa lengo lile lile la kupitia sheria na sera ya madini. CCM ikaanza kujitapa kwamba ni sehemu ya ilani yake.

  Lakini hakuna popote katika ilani yake paliposema kwamba wangepitia upya mikataba ya madini. Waliiga wazo la CHADEMA ili kuwanyamazisha kisiasa, lakini hawakuwa wamejifunza kwao jinsi walivyodhamiria kulitekeleza.

  Tamko jingine muhimu la CHADEMA lilitolewa na Mbowe katika Uwanja wa Jamhuri Dodoma. Akasema CCM inawahadaa wananchi kuhusu serikali kuhamisha makao makuu kutoka Dar es Salaam kwenda Dodoma.

  Akasema CHADEMA haina sababu ya kudanganya wananchi. Akasema sera ya CHADEMA si kuufanya makao makuu ya serikali, bali kuufanya Dodoma uwe mji wa wasomi – kwa kujenga vyuo vingi vya elimu ya juu. Akatoa faida nyingi za kuufanya mji wa wasomi; mojawapo ikiwa ni ongezeko la mzunguko wa pesa, hivyo kuinua uchumi wa Dodoma.

  Mara baada ya uchaguzi, Rais Kikwete akanakili wazo hilo; akatangaza uanzishwaji wa Chuo Kikuu cha Dodoma, ambacho kilianzishwa rasmi Machi 2007, bila maandalizi ya kutosha.

  Katika mkutano wao wa mwaka 2010, CHADEMA walitangaza ubinifu wao wa kuchangisha wananchi kwa kupitia ujumbe mfupi wa simu za mkononi.

  Katika hali iliyodhihirisha wivu na fitina za kisiasa, CCM, kupitia serikali, ilitisha makampuni ya simu yasiwezeshe mfumo huu kwa CHADEMA hadi wao watakapokuwa wameutumia.

  Nilishuhudia viongozi na maofisa wa CHADEMA wakivutana na watendaji wa makampuni hayo kuhusu utekelezaji wa mpango huo.

  Baada ya miezi kadhaa, CCM nayo ikazindua kwa kishindo mpango huo huo kwa kutumia makampuni yale yale. Woga, wivu, fitina!

  Haya ni maeneo machache ambayo CCM imeiga waziwazi kutoka CHADEMA. Na huu ni
  ushahidi mwingine kuwa CCM inaanza kupoteza taratibu uhalali wa kutawala.

  Ni kielelezo cha kauli iliyomponza aliyekuwa Katibu Mkuu wa CCM, hayati Horace Kolimba, kwamba: "CCM haina dira wala mwelekeo," iliyosisitizwa upya na mzee Joseph Butiku, wiki chache zilizopita.

  Hii ndiyo CCM inayojitahidi kujitambua, ingawa haipo tayari kujikubali; CCM inayojivunia miaka 50 madarakani, lakini inadhani njia pekee ya kudumu madarakani ni kuiga mikakati na mipango ya CHADEMA. Kwa mbinu hii, itapona?  [​IMG]
   
 6. Ellyson

  Ellyson JF-Expert Member

  #6
  May 27, 2011
  Joined: Nov 13, 2010
  Messages: 1,717
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  Pole nilidhani kuwa u mzima kumbe nawe pia ni mfu? Nenda kawashauri wafu wenzio akina Dovutwa & CCM company.
   
 7. The Finest

  The Finest JF-Expert Member

  #7
  May 27, 2011
  Joined: Jul 14, 2010
  Messages: 21,709
  Likes Received: 44
  Trophy Points: 145
  GROAN GROAN GROAN

  Luck is merely an illusion, trusted by the ignorant and chased by the foolish
   
 8. F

  FJM JF-Expert Member

  #8
  May 27, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 8,088
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 145

  Mtoto wa nyoka ni nyoka. Tumaini limekufa
   
 9. k

  kizazi kipya JF-Expert Member

  #9
  May 27, 2011
  Joined: Jul 21, 2010
  Messages: 329
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  ndio wale wanaotumiwa na nape...sio yeye bali ni njaa zinaomfanya ajidhalilishe...pole sana mchumia tumbo..
   
 10. k

  kakini Senior Member

  #10
  May 27, 2011
  Joined: Mar 31, 2011
  Messages: 197
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0

  nadhani mtoto wa darasa la 7 akisoma hii atacheka sana
   
 11. CAMARADERIE

  CAMARADERIE JF-Expert Member

  #11
  May 27, 2011
  Joined: Mar 3, 2011
  Messages: 4,427
  Likes Received: 158
  Trophy Points: 160
  Kwa hiyo unaafiki kuwa CCM wanakula sio?
   
 12. k

  kilombero yetu JF-Expert Member

  #12
  May 29, 2011
  Joined: May 6, 2011
  Messages: 1,007
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  mbowe awataka bavicha kuhakikisha chadema inatawala nilizan anataka chadema iongoze
   
 13. Lunyungu

  Lunyungu JF-Expert Member

  #13
  May 29, 2011
  Joined: Aug 7, 2006
  Messages: 8,836
  Likes Received: 75
  Trophy Points: 145
  A Moshi mwache huyu Tumaini yeye huwa hana moja bali vioja . Mwacheni kumjiu tuendelee na hoja za maana .Yeye yuko kwa hao anao watetea miaka yote hana jipya
   
 14. kipindupindu

  kipindupindu JF-Expert Member

  #14
  May 29, 2011
  Joined: Dec 16, 2010
  Messages: 1,051
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Tumaini letu kubali kushindwa!
   
 15. Shaycas

  Shaycas JF-Expert Member

  #15
  Jun 6, 2011
  Joined: Feb 13, 2009
  Messages: 899
  Likes Received: 34
  Trophy Points: 45
  Lets wait and see
   
 16. Memo

  Memo JF-Expert Member

  #16
  Jun 6, 2011
  Joined: Jan 17, 2011
  Messages: 2,147
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  Yaani "Tumaini Letu" unataka CDM isitumie hata maneno ya Kiswahili kama "ilani", eti kwa vile yametumiwa na CCM. Kwani "Kamati Kuu", "Kamati ya Maadili", etc ni vitu mimevumbuliwa na CCM? Warusi, Wachina, etc nao wamekuwa na hizo kamati (kwa lugha zao).

  Zamani kulikwa na Chama kimoja tu, na neno CHAMA maanake ilikuwa ni CCM. Kwa logic yako, CDM hawatakiwi kutumia neno chama kwa sababu watakuwa wamenakili toka CCM!

  Naona utakuwa mmojawapo wa wale waliotumwa siku za karibuni kuja hapa baada ya CCM kulalamika JF inakimaliza. Huvui kitu hapa!
  You like this.
   
 17. Memo

  Memo JF-Expert Member

  #17
  Jun 6, 2011
  Joined: Jan 17, 2011
  Messages: 2,147
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  The Following 3 Users Say Thank You to Augustine Moshi For This Useful Post:

  Memo (Today), mfukunyunzi (27th May 2011), Mtumishi Wetu (27th May 2011) ​
   
 18. F

  FJM JF-Expert Member

  #18
  Jun 6, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 8,088
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 145
  Kilichofikisha ccm hapo ilipo ni majungu na fitna kama hizi ulizoandika hapa. Watu wazima wanapa kulinda na kutetea katiba lakini kila uchwao ni majungu na fitna. Na sasa matokeo yake ndio hayo - za mwizi arobaini. Mmezungukana mpaka kwenye kope za macho, na ndio maana mnashindwa kupeana zile barua. Ila kinachohuzunisha ni kuwa mtoto kama wewe Tumaini letu unaonekana kurithi huu umaaluni. But again, mtoto wa nyoka ni nyoka.
   
 19. kichomiz

  kichomiz JF-Expert Member

  #19
  Jun 6, 2011
  Joined: Feb 28, 2011
  Messages: 12,015
  Likes Received: 2,667
  Trophy Points: 280
  Unajitutumua kopotosha weee lakini wapi,watu wanakuona kama mwendawazimu fulani hivi,unatapa tapa tu huna jipya wewe,kawapotoshe nduguzo huko kwenu sio hapa.
   
 20. K

  Kakalende JF-Expert Member

  #20
  Jun 6, 2011
  Joined: Dec 1, 2006
  Messages: 3,259
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 135

  Huu ndio mfano halisi wa 'COPY & PASTE' !?? wakati mwingine muwe makini kidogo!
   
Loading...