CHADEMA 2015 Tanzania ndicho chama tawala

JOSE KASANO

Senior Member
Apr 23, 2013
120
93
Habari wana JF.
Mimi ni Mtanzania kwa kuzaliwa, nimezaliwa, kukua, kusoma na kuishi Tanzania huku kwa umri wangu mdogo nikishuhudia mambo mengi yanatendeka katika Taifa letu lijulikanalo kama Taifa lenye amani Duniani kote.Huku tukihubiri amani, dhana yenyewe amani inaonekana kutofahamika kwa watanzania walio wengi; amani wakati watu wanakufa njaa; amani wakati raslimali za Taifa zinataifishwa na watu waliopewa dhamana ya kuzilinda na kuzipeleka nje kwa manufaa yao; amani wakati wananchi walio wengi wanashindwa kusomesha watoto wao shule nzuri; amani wakati vyombo vya ulinzi na usalama vinatumiwa na watawala wa kisiasa kuzima sauti za wananchi kwa kuwazuia kufanya mikutano , maandamano na hoja zenye maslahi kwa Taifa.

Yapo mambo mengi sana yanayoendelea kufanyika katika Taifa letu kupitia mgongo wa kuwadanganya watanzania eti ni nchi ya amani huku wachache wakitumia turufu hii ya tulinde na kudumisha amani ya Tanzania wakionekana wazi kabisa kuwa kujinufaisha na raslimali zetu tena bila huruma.

Nimezichambua sera za Chama tawala kwa hivi sasa Tanzania, utekelezaji wa sera hizo, muelekeo wa chama hicho, aina ya viongozi wanaoendelea kukiongoza na wanaoteuliwa kupewa nyadhifa mbalimbali nikagundua kuwa chama tawala Tanzania kilichopo kwa sasa mwisho wake huenda ni 2015 na kinawezakana kisiongoze hata kambi ya upinzani Bungeni.

Lakini pia nimechambua sera, utekelezaji na uwajibikaji, aina ya viongozi na namna viongozi wanavyowajibika kwa maslahi ya wananchi kwa kuvichunguza vyama vya upinzani vilivyoko hapa Tanzania na kugundua kuwa tayari vyama vingine vimebeba kofia ya upinzani lakini si vyama vya upinzani hata kidogo.Mfano, CUF ni chama ambacho kimeunda serikali ya mseto huko Tanzania visiwani lakini eti kikija huku Bara ni chama ya upinzani, katibu wake mkuu ndiye makamu wa Rais Zanzibar kwa maana hiyo huku Bara kikijadiri jambo kama chama cha upinzani basi habari na mikakati yote lazima awe nayo mh.makamu wa Rais huko Zanzibar.Kwa maana hiyo tayari kimepoteza taswira,lakini chama hiki kiliwahi kushika mashiko katika nchi hii kabla ya ccm kukishikilia bango kuwa ni chama cha waislamu na magaidi hivyo kukidhoofisha kabisa. NCCR-MAGEUZI nacho ni chama kilichoonekana kuwa na machachari kidogo chini yake Mh.James Mbatia kama mwenyekiti na kuwa na wabunge ambao kimsingi tunawaona wakijali maslahi ya Taifa lakini kitendo cha Mh.James Mbatia kuteuliwa mbunge la Rais wa ccm kilimuondolea baadhi ya element licha ya kwamba mh.Mbatia ni mtu anayeonekana kuwa na uzalendo wa Taifa hili mbali na itikadi za vyama na mambo mengine.Tunfahamu kazi nzuri anayofanya bwana Mbatia bungeni na hata nje ya Bunge ila tunashuhudia baadhi ya hoja zake zikikejeliwa na wabunge hata mawaziri wa ccm kwa kuwa na dhana ya kuwa kateuliwa na Rais ambaye ndiye mwenyekiti wa ccm.Mfano siku moja waziri alikuwa akijibu swali la mh.Mbatia bungeni na kusema,'mh.Spika, naomba kujibu swali la mh.James Mbatia, mbunge aliyeteuliwa na Rais wetu na mwenyekiti wetu wa ccm kama ifuatavyo'.Maelezo ya waziri huyu ilikuwa ni kumdisvalue bwana Mbati.

CHAMA CHA DEMOKRASIA NA MAENDELEO(CHADEMA) ndicho chama pekee cha upinzani kilichobakia Tanzania kwa hivi sasa na ndicho chama kinachoonekana kukubalika zaidi kwa wananchi kila uchwao.Chama hiki kinazo sera, mikakati ya kuongoza nchi na viongozi wanaokubalika katika jamii wanaojulikana kama watetezi wa wanyonge na ndio maana mikutano ama maandamano yoyote yanayoitishwa na CHADEMA lazima wananchi waitikie kwa nguvu zao zote hata michango wananchi hukichangia chama hiki bila hiyana yoyote huku wakiwa na imani kabisa myoyoni mwao kuwa chama hiki chaweza kuwaletea matumani yao yaliyopotea.Ni kwa kufahamu hili cham cha mapinduzi chama hiki cha CHADEMA wanakiona sumu kwao, tishio kuliko maelezo, kinakubalika kuliko chenyewe chama tawala, kinaendelea kupewa misaada kutoka ndani na nje; ni kwa kufahamu hilo ndipo hujuma mbalimbali zilianza kutolewa kwa CHADEMA kwamba ni chama cha kikabila yaani wachaga(hoja iliishiwa nguvu), kuwa ni chama cha udini(hoja ilipuuzwa), ni chama cha marafiki(hoja iliishiwa mashiko), ni cham cha magaidi (HOJA ILIYOSHIKILIWA BANGO NA MAKADA WA CCM KAMA KETE YAO YA KUKIMALIZA CHADEMA, LAKINI WAMEANGUKIA PUA NA SASA VINYWA VYAO NVI WAZI WANADUWAA WAFANYE NINI MAANA CHAMA CHAO KINAWAFIA MIKONONI).

Ni kwa nini chama cha Demokrasia na maendeleo(CHADEMA) kinapewa kete ya kutawala nchi hii 2015? Hoja ni nyingi mno na sababu ziko wazi kabisa.Hii ni kutokana na Watanzania kuchoshwa na dhuluma za viongozi wa ccm na serikali kwa ujumla kushindwa kutekeleza wajibu wao wa kuwaletea maendeleo na kuanza kujinufaisha wao wenyewe na vizazi vyao.BAADHI YA MAMBO AMBAYO YANAWADSIVALUE CCM NA KUWAVALUE CHADEMA NI KAMA IFUTATAVYO:

1.UCHAGUZI WA SPIKA WA BAADA YA CHAGUZI MKUU WA 2010.
Hakuna mtanzania ambaye hakuona dhuluma iliyofanyika ya kumuondoa mh.Sitta kugombea Uspika.Hizi zilikuwa ni mbinu chafu zilizofanywa na viongozi wa ccm wa juu na serikali kuhakikisha kuwa Bwana Sita hapati uspika maana alionekana kucheza kete zake vizuri bungeni kwa kuwapa haki sawa wabunge kujenga hoja huku wapinzani wakionekana kuichachafya serikali hadi kufikia kuiwajibisha pale waziri mkuu kwa wakti huo Mh.Lowasaa alipolazimika kujiuzulu kwa kashfa ya RICHMOND. Hivyo walilazimika kuweka mtu ambaye atakahikisha kuwa analinda cham tawala kwa kuwaziba midomo wapinzani na hii ndiyo tunashuhudia maana Anna Makinda na Timu yake ya kina Ndugai inaonekana wazi namna inavyolinda serikali na ccm badala ya kufanya kazi ya kuwatumikia watanzani kuhakikisha wanaisimamia serikali.Wabunge wa ccm sasa hivi wanafanya kazi ya kuijibia hoja serikali na kuishauri, wajibu ambao ni wa mawaziri.Pale wapinzani wanapochachamaa juu ya serikali kutotimiza wajibu wake kwa wananchi tumeshuhudia wakipewa rungu kali na kiti cha spika, mambo haya huwapa credit CHADEMA huku nje ya Bunge kwa kutathmini kazi nzuri wanayofanya.

2.SERA YA CCM YA MAISHA BORA KWA KILA MTANZANIA.
Baada ya serikali ya ccm kuingia madarakani kwa kete ya kuleta maisha bora kwa kila mtanzania, sasa imebainika kuwa ccm walikuwa wanomba kuingia madarakni ili kuleta maisha duni kwa kila mtanzania.Badala ya maisha bora kwa kila mtanzani kwa hivi sasa maisha yamekuwa magumu kuliko hata ya miaka iliyotangulia.Viongozi wa serikali na ccm wanashuhudiwa waziwazi wakijihusisha na vitendo vya ufisadi vya kuhujumu Taifa, wengine wanafanya biashara ya meno ya Tembo huko ulaya bila Taifa kunufaika na chochote(Mfano kwa mujibu wa hotuba ya kambi ya upinzani iliyowasilishwa na waziri kivuli mh.Mchungaji Msigwa ilimtuhumu Kinana ambaye ni katibu wa ccm Taifa kuhusika na ujangili wa nyara za Taifa letu huku serikali ikitoa majibu mepesi). Watanzania wanaona na wamechoka sana kuendelea kukitumika ccm na ndio maana wako tayari kukiweka CHADEMA madarakani 2015.

3.MATUMIZI MABAYA YA VYOMBO VYA DOLA.
Hili ni suala ambalo limekera si watanzania tu bali hata watu wa Mataifa ya nje.Tanzania inayomatumizi mabaya ya vyombo vya kwani tumeshihudia vyombo vya ulinzi na usalama vikifanya kazi ya kukilinda ccm kwa hali yoyote ile kwa kuwadhibiti wapinzani na wananchi kwa ujumla wasijumuike kujadili mambo ambayo yanahusu mustakabali wa Taifa letu.Vyombo hivyo vimefikia hatua ya kukiuka haki za binadamu kwa kuwaua baadhi ya watu wasio na hati Mf. maauji ya huko Arusha, Morogoro, MWANDISHI WA Habari MAREHEMU MWANGOSI ambaye aliuawa na jeshi la polisi kule Nyororo bila huruma huku tukio hilo likishuhudiwa na kamanda nduli na fashist KAMUHANDA wa mkoa wa Iringa huku serikali ya ccm ikijigamba kupitia kwa waziri wa mambo ya ndani Bwana NCHIMBI na waziri LUKUVI kuwa kamanda KAMUHANDA ni kiongozi shupavu anastahili pongezi kwa kuwadhibiti wapinzani kufanya mikutano.Watanzania walifadhaishwa na kifo cha Mwangosi na utekaji na utesaji wa mwenyekiti wa madaktari Dr.Ulimboka ambaye aliteswa sana lakini alipopata nafuu aliwataja wahusika wakiongozwa na maoisa wa IKULU ya Kikwete huku serikali ikibaki kimya juu ya Unyama huo.Watanzania wamekasirishwa na hali hiyo ya vyombo vya dola kuendelea kuwaziba midomo watu wanaoikosoa serikali ili kuhakikisha ccm kinaendelea kutawala hata kwa mabavu, wananchi wameamua 2015 CHADEMA ndicho chama kitachoongoza taifa hili ili kuliletea ukombozi dhidi ya watu wanaoendelea manyanyaso kwa raia wake tena bila huruma.

4.RAIA KUBAMBIKIZWA KESI NA VIONGOZI WA SERIKALI.
Serikali mahali popote pale ilipo duniani lengo lake ni kulinda utu, mali na haki za kila raia wake.Hali hii ni tofauti kabisa kwa Tanzania maana wimbi la viongozi wa serikali wakisaidiwa na vyombo vya dola la kuwabambikizia kesi za mauaji, ugaidi, ubakaji, rushwa tena kwa manufaa ya ccm limeshamiri.Waziri Nchimbi alilazimika kuwaondoa madarakani baadhi ya polisi waliokuwa wakiwabambikizia kesi wananchi kwa makosa ambayo hawajanfanya ili kujinufaisha lakini waziri hajua kwamba huo ni mtandao mrefu yani kuanzia chini mpaka juu serkali hivyo bado tatizo linaendelea.Mkurugenzi wa Ulinzi na usalam wa CHADEMA Mh.Lwakatare alibambikiziwa kesi ya UGAIDI na mafisadi wa ccm wakiongozwa na Mwigulu njemba ambaye anajifanya mzalendo kumbe ni fisadi mkubwa sana katika Taifa let kwa kuendesha siasa za kipumbavu ambazo hazina tija kwa Taifa letu.Ukweli umebainika Lwakate makosa ya Ugaidi kafutiwa na mahakama huku vyombo vya usalama ambavyo vilifanya kazi kubwa kuandaa ushahidi wa kupika wakihaibika.Vilevile baadhi ya polisi Morogoro wanashikiliwa wakiwa na kichwa cha binadamu ambacho walikuwa wanakwenda kumbambikizia mfanyabishara mmoja ili wamuombe rushwa kwamba wamemkata na kicha cha mtu mungu alisaidia wakatiwa mbaroni.Hali ni mbaya sana kama viongozi walinda amani ndio wanafanya uharamia huu wananchi wakimbilie wapi tofauti na kuiondoa serikali ambayo imeshindwa kuwajibika wa raia? CHADEMA NDO MBADALA 2015 kuondoa dhuluma hizi.

5.RUSHWA ILIYOKITHIRI, HUDUMA MBOVU ZA KIJAMIINA MIPANGO ISIYOTEKELEZEKA NA KUONGEZA UMASKINI.
Katika zama hizi za serikali inayoongozwa na ccm suala la Rushwa limeishaonekana kuwa ni huduma maana hata wabunge wa ccm walishataka kupisha sheria eti ni takrima.Huwezi kupata huduma popote pale mpaka utobolewe mifuko yako,Vituo vya polisi, mahakamani, mahospitalini ,mashuleni, maofisini rukshwa imeshamiri na hakuna juhudi za makusudu kukomesha tatizo maana hata TAKUKURU ni wala rushwa wakubwa sana.

Elimu yetu imeishaonekana si chochote wa lolote.Wanafunzi wamefanya mitihani kidato cha nne zaidi ya nusu walipata 0 baadaye serikali ya ccm kifuta matokeo na kuanza kuchakachuaa matokeo mapya hivi sasa tunasubiri uchakachuzi huo ukamilike tuone jipya ni lipi, swali ni je hata mwaka kesho watachakachua?

Kimsingi mambo ni mengi LAKINI KIKUBWA NI KWAMBA WANANCHI WAMEISHAJIPANGA 2015 LKUKIWEKA MADARAKANI CHADEMA ILI KUNUSURU TAIFA HILI NA HAWA WAFEDHURI WACHAHCHE.
 
Mwenye macho haambiwi tazama. Mateso waliyoyapata Watanzania kwa takribani miaka 50 ya utawala wa CCM yako wazi. Sasa hivi ni suala la muda tu watanzania waamue mustakabali wa nchi yao kwa manufaa ya nchi na watu wote si kwa wateule wachache tu.
Itafika siku watanzania watakuwa na ujasiri wa kusema basi inatosha.
 
Lakini jaman kama uchaguzi ukifanyika leo Chadema itapata majimbo mengi na si kuongoza nchi maana bado hawajafika chini kwenye ngazi ya vijij mfano me niko huku masasi mtwara yaan chadema hamna kabisa napata kaz sana kutafuta wanachama ila bado sana
 
Of course yes! This has no further discussion.......tzns are aware now they don't listen to magambaz outdated propagandaz...they all focus for the future nation without ccm and all ccm and government corrupt leaders starting from kikwete himself
 
Bado kabisa kiosheni chama chenu kwanza na sifa za fujo udini na ukabila ndio tutazungumza kushika madaraka TZ
Watanzania ni waangalifu sana linapokuja suala la uongozi wa nchi
Mfano jamii forum kwa kiasi kikubwa inajulikana ni kigoda cha Chadema na hutumika kuonesha sera za CDM
Lakini chombo hichi kwa matusi kwa waislamu uislamu na Mitume yao ni jambo la kawaida na mfumo mzima huwa unashambulia uislam kwa kutukana bila ya mada kufutwa au kupigwa ban kwa mtukanaji
Waislam wengi pia ni memba wa mtandao huu wanaona hali ilivo
Hivo huu ni uchafu unatakiwa kuoshwa
Japo Zito alilisemea suala la udini na kuonesha kwamba CUF walasingiziwa na sasa ni CDM lakin Zito huwa ni mchangiaji humu na hajawahi kuwakemea wana chadema kujipesha na chuki za kidini humui mtandaoni
Wala si kiongozi yoyote wa CDM amewahi kukemea tabia ya kuonesha chuki na matusi kwa vijana wa CDM ndani ya mtandao huu
Jee itawezekana kweli kuingia ikulu kutegemea kundi moja hapa tanzania? HAIWEZEKANI
Muda upo utumieni kujisafisha na kujenga imani na kuwashirikisha waislam nao kujiunga CDM wawezesheni washike nafasi isiwe waislam ni zito na familia yake tu na Arfi
Inahitajika nia safi na ari ya kujenga Taasisi ya kisiasa isiyo kuwa na ubaguzi hivo mujiuluze jee tunayo nia hio ?
Ushawishi wa CDM na CUF unafanana kwa sababu Inakua vigumu kwa wasomi wa kikristo kujiunga na CUF kwa hisia za kidini na pia inakua vigumu kwa wasomi wa kiislam kuingia CDM huu ndio ukweli na ndio hapa pa kujisafisha kuleta matumaini kinyume chake ni CCM tu ndio inayo faidika

Sent from my BlackBerry 9700 using JamiiForums
 
Wana CDM bado nazidi kutoa mchango wangu juu ya kutorelax, kwa kutizama wimbi kubwa la wahudhuriaji wa mikutano ya kisiasa. Kama mlivyoshuhudia wakati wa ziara ya katibu mkuu wa CCM mikoani huwaambia wanachama wao waonyeshe kadi za uanachama kwanza, Hivyo ni muda wa kuhakiki wanachama pia kuzidi kujiimarisha zaidi tena kwa kasi kubwa kuliko hata hii iliyopo sasa, Ambayo nayo kwa hali ya hewa tungekuwa na vipimo vya majanga labda wangeshatangaza kuwa muda si mwingi harakati hizo zitazimwa kama mkaa kwa maji "Resonance yeke fanya jaribio usikie mlio wa mkaa, lakini moto huzima pamoja na kutokea athari za kutapakaa kwa maji chini kitu ambacho hakikutarajiwa".

Pia kikubwa zaidi, kuna mwanajamvi mmoja liyewahi kutoa michango yake hapa akisema "CCM is a dying horse na anarusha mateke vibaya kiasi kwamba usipojihadhari unaweza kudhuriwa vibaya" Hivyo ni kuzidi kuangalia uelekeo wa mateke yake ambaye hakuna asiyekubalina hapa kuwa ni kuzidi kulinda uhalali wa kuwepo madarakani. Chukulia Mfano wa Kwa jirani zetu hapo ukikatiza Namanga, Mkuu aliyekabidhi juzi uongozi huku akionyesha hajawahi kuongea chochote cha kuunga au kutounga mkono chama chochote aliingiaje madarakani mhula wa pili? na sherehe yake ya kuapishwa ilikuwaje?. Rudi hapa kwetu mwenyekiti wa chama alishakiri katika moja ya vikao vya juu kuwa yeye hawezi kukabidhi uongozi upinzani na atahakikisha anakabidhi uongozi kwa mwanachama wa chama chake, bear in mind mchakato wa katiba mpya unavyoendelea huku ukifocus matumizi ya vyombo vya dola kwa sasa yanavyonekana. Rudi nyuma kidogo uchaguzi wa 2010 pale ambapo matokeo yalikuwa yanarushwwa moja kwa moja na vyombo vya habari siku ya pili tu tulishuhudia kizuizi kikubwa cha kurusha matokeo bila matamshi wa wasimamizi na hapo ukiingia zaidi Kuna kauli ilitoka kwa kiongozi mkuu kupitia chama kuwa hakuna matokeo yatakayotangazwa ya ubunge au uraisi bila yeye kusema (kauli ilikuwa ni ya siri) na watanzania tukaanza kushuhudia masanduku ya kura kuchelewa kufika vituo vikuu kwa kisingizio cha miundombinu "Hata Dar yalionekana kuchelewa kuliko maeneo ya vijijini, Katika jimbo nililokuwa mimi Kituo kimoja kilichopo mita kama 400 toka wilayani sanduku lilifika siku ya Tatu tena bila sanabu".

Hata hivyo kuna tetezi zilizojitokeza juu ya kura zenye kemikali kutumika enzi za kuiua CUF kauli iliyotolewa na Lipumba pamoja na ndugu Mrema kudai hata kura yake moja tu mpaka mahakama za juu aliyopiga kupotelea kusikojulikana. vile vile tumeona wabunge kadhaa wakirudishiwa ubunge na mahakama kuu pamoja na kwamba chaguzi zilikithiri kwa Rushwa kitu ambacho hakikubaliki kisheria.

Baada ya kujitathmini kwa yote hayo, CDM imejiandaaje kukabiliana na tatizo hilo la kiongozi kuja kutangazwa bila kujali masanduku ya kura yalisemaje au kulikuwa na usanii gani katika kura na ulinzi ukaimarishwa vya kutosha? Rejea hapo visiwa vya Zanzbar hawakutoka ndani karibu wiki nzima huku mabomu ya machozi na makatazo ya kutotoka nje yakishamiri kama okjeni vile kabla ya CUF kukubali ndoa.
 
Maccm yakiiba kura je?

Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums
 
Salaam kwenu wazalendo!
Niliwasilisha mada hapa kwamba chama cha Demokrasia na maendeleo ndicho cha tawala Tanzania mwaka 2015, baada ya kuwasilisha mada hiyo, kuna baadhi ya maoni yalipostiwa na baadhi ya watu wengine wakiunga mkono huku wengine wakionesha wasiwasi kwamba CHADEMA 2015 hakiwezi kushika dola kwa sababu hakijajijenga mpaka ngazi za chini za vitongoji na kwamba hakina wanachama wengi kama kilivyo chama cha CCM a.k.a CHAMA CHA KUJIVUA GAMBA(Gamba ambalo lilishindikana kuvuliwa), kwa taarifa yenu kitimoto huwa hakichunwi ngozi, ukikichuna ngozi huo huwa ndio mwisho wa maisha yake vilevile ukiona umepiga mbwa akabweka, ujue hajaumia lakini ukiona umepiga mbwa na akakunja mkia wake ndani na kutimua mbio, jua fika kabisa kwamba mbwa huyo kaumia vibaya sana na akikuona popote pale atakuwa anabweka kisha kutimua mbio na kutokomea(falsafa ya gamba);

Nawashukuru wale wanaoona mbali juu ya mwenendo wa Taifa letu maana tunapaswa kuiangalia Tanzania angalau miaka 50 ijayo itakuwa wapi kwa kutazama tunakotoka na tulipo sasa hivi.Kama una upeo wa kutosha, ukichunguza unakotoka na ulipo sasa inatosha kujua unakoelekea, lakini kama hujui unatoka wapi na uko wapi ni vigumu kujua unakoelekea.

Kwanza niwafahamishe watu wenye mashaka kwamba CHADEMA kinaweza kushindwa kushika dola 2015 kwa sababu hakina wanachama wengi, viongozi wa CHADEMA hii ni kazi yenu kuhakikisha mnaeneza sera za chama hadi ngazi za chini za vitongoji LAKINI WATAKAOKIWEKA CHAMA CHA CHADEMA MADARAKANI MWAKA 2015 SIO WANACHAMA WA CHADEMA NDUGU ZANGU BALI NI WATANZANIA WOTE WAKIWEMO WANACCM, CUF, TLP, NCCR-MAGEUZI, SAU n.k na wale wote wasio na itikadi za vyama ila wanaitakia mema nchi yetu.Hata kama CHADEMA hawa kwa hivi sasa hawana viongozi ngazi hizo za chini ukweli ni kwamba wale viongozi mnaowaona wamevaa mavazi ya kijani huko vitongojini ndani ya nyoyo zao kuna CHADEMA, msiwe na wasiwasi na hilo, watanzania wote hata hao wa magamba wamechoka na maisha magumu yanayosababishwa na ccm.

Sasa naomba nianze kuwasilisha ushahidi wangu kwenu:

1. Dr.aliwataja mafisadi 11 hapa nchini bila kumung'unya maneno kwamba ndio wametafuna nchi yetu Tanzania.Baada ya hapo magamba walirukaruka hapa na pale eti wanakwenda mahakamani wamekashifiwa, Dr.(ninaposema Dr.nadhani unamfahamu Dr. wa ukweli sio yule ambaye aligawiwa u Dr. bila kuandika hata paper moja) aliwambie njia ya kwenda mahakamani ni nyeupe nendeni tuje tuwavue nguo.Baadaye wakasema hatutakwenda mahakamani kwa sababu Dr.mzushi tu!(MPO HAPO?).Nani anaweza kukashifiwa halafu aseme wewe ni mzushi tu nakupuuza? Watanzanie waliona na wanajua ukweli wa Dr. na wanafahamu kwamba mafisadi hayo ndo yanaangamiza Taifa letu pendwa.

2. MIKUTANO NA MAANDAMANO.
Naomba mchunguze wenyewe ushahidi huu, CCM wakifanya mikutano ya hadhara mahali popote pale ni lazima waandae magari mengi kwa ajili ya kusomba watu kuhudhuria mikutano hiyo,hongo na rushwa kwa ajili ya kuwarubuni wananchi wahamie kwenye chama hicho, fedha ya walipa kodi ndo hutumika kufanya mambo yote badala ya kuipangia miradi ya maendeleo wananchi. LAKINI CHADEMA WAKIFANYA MIKUTANO YA HADHARA, WANANCHI WENYEWE HUJISAFIRISHA KWA GHARAMA ZAO TENA KUTOKA KONA MBALIMBALI ILI WAJUE MUSTAKABALI WA TAIFA LAO, WANANCHI HAO HUTOA MICHANGO YAO YA HIARI KWA AJILI YA KUKUZA NA KUENDELEZA CHAMA, HUJIUNGA NA CHAMA BILA HONGO YOYOTE NA KADI HULIPIA WENYEWE WAKATI ZA KADI ZA CCM WANACHAMA HUDHAMINIWA NA VIONGOZI.(Je, huko sio kukubalika? au mnataka ushahidi gani?)

3.MIJADALA KATIKA VIKAO VYA BUNGE:
Naomba mchunguze wenyewe mijadala inayojengwa katika vikao vya bunge, akisimama mbunge yeyote wa CHADEMA wananchi huku mitaani wote huacha shughuli zao na kukaa kwenye runinga ili waweze kusikiliza hoja zenye mashiko na maana, zinazoongelea juu ya kutatua kero za wananchi, zinazobana wezi na mafisadi wanaohujumu rasilimali za Taifa letu, hoja ambazo huwafanya watu wajisikie nyoyo zao zisuhuzike licha ya matatizo waliyonayo LAKINI akisimama mbunge wa CCM! utasikia wananchi wakisema,' aahhhhhhhhh!' halafu huondoka kwa maana ya kwamba hawatarajii hoja zenye maana kutoka kwa wabunge hao.Na mfano wa hili ni kwamba akisimama mbunge wa ccm kujenga hoja hufanya mambo yafuatayo: Kwanza; huazan kwa kutoa shukrani kwa rais, mawaziri, kiti cha spika kuendeleza ubabe,wananchi wake kwa ujinga wao kumpeleka bungeni, pili; huunga mkono hoja hata kabla hajaijadili, tatu; huanza kuponda wapinzani na kuwatukana matusi ya nguoni kwa ukweli wao wanaosema kwa wananchi bila kujua kwamba huwa wanatukana wananchi moja kwa moja, nne; huanza kuituhumu serikali na kuilalamikia wakati ameishaipongeza na kuitetea, tano; anashukuru tena kiti cha spika halafu anakaa.Ndio maana wananchi huwa hawapendi kuwaangalia wabunge wa ccm wakijega hoja bungeni maana hawaoni jipya kwa mustakabali wa maisha yao, sita; spika anasimama au akiwa amekaa anampongeza mbunge huyo kwa hoja nzuri(kama huamini fuatilia vikao vya bunge upate ukweli).

4.(i) KATIKA VYUO VIKUU.
Nenda vyuo vikuu vyote kote nchini hapa ambako wanapatikana wasomi na wachambuzi wa masuala ya kijamii na kitaifa uone kama utapata wafuasi wa ccm, ukweli ni kwamba hakuna! hata wanaoonekana kuiunga mkono ccm ni wale wenye njaa ili waweze kujaza matumbo yao na kupata udhamini wa masomo lakini ndani ya nyoyo zao ni CHADEMA pure.

(ii) KATIKA VYUO VYA STASHAHADA NA ASTASHAHADA.
Nenda katika vyuo hivyo utapata ukweli huo maana hata waomi hao wote hawana sprit tena ya ccm kama huamini nenda kueneza sera za ccm katika vyuo hivyo huone kama hutapondwa mawe, wamechoka na hao ndio wasomi wanosambaza elimu na sera za CHADEMA kote nchini.

(iii)KATIKA SHULE ZA SEKONDARI:
Nenda katika shule za sekondari ukweli utaupata ndugu yangu kwamba CHADEMA ndo cha PENDWA na hakuna chama kingine.Wanafunzi wamechoka sana na udhalimu wa serikali ya ccm, hawana vitabu, madarasa hakuna , maabara hakuna, walimu hakuna, mitihani inatungwa na kufutwafutwa yaani kila kitu hakieleweki, serikali imeishapoteza muelekeo.Hawa wote wameishaona CHADEMA ndio MWAROBAINI wa matatizo yote.

(iv) WAHOJI WALIMU.
Walimu ndio watumishi walio wengi kati ya watumishi wa serikali maana ni zaidi ya nusu ya wafanyakazi wa serikali; wote wamekata tamaa na serikali ya ccm maana mishahara yao kila siku ni kilio, hujaribu kugoma ili kuona kama serikali ya ccm inaweza kuwajali lakini huambulia kupelekwa mahakamani, kufukuzwa kazi na vitisho kibao.Walimu wote kwa hivi wamechoka na ahadi za uongo za serikali ya ccm na wote kwa pamoja 2015 kura zao ni kwa CHADEMA, haki ya nani nawambie mtaona labda wenye sumu wainywe mapema.

(v) MADAKTARI NA WAUGUZI:

Nenda kawahoji wataalamu hawa watakueleza walivyochoshwa utawala wa serikali ya ccm lakini watakueleza msimamo wao kwa CHADEMA kwani serikali ya ccm imewadhulumu mangapi? Hadi daktari kufikia hatua ya kugoma sio kitu cha kawaida maana maadili yake hayaruhusu lakini madaktari wa Tanzania walifikia hatua hiyo maana wamechoshwa na dhuluma, wafanye nini? wakisema wanapuuzwa! wote hawa 2015 kura ni kwa CHADEMA wala sifanyi kampeni hapa naeleze facts.

(vi) POLISI:
Waulize polisi, watakuleza namna ambavyo wamechoka kutumiwa na serikali ya ccm kisiasa maana wameishachukiwa na wananchi huku mitaani, polisi sio rafiki wa mwananchi tena ni maadui kwani wananchi wameishachoshwa na dhuluma zifanywazo na polisi kuwanyima haki zao kwa maslahi ya ccm;polisi wanalaumiwa bure maana kazi yao wakiambiwa piga wao ni kutekeleza tu,jeshin hakuna jibu la hapana unapoulizwa na bwana mkubwa lakin ki ukweli polisi wa Tanzania nao wanaganga njaa na ndio maan wengi wao wameona kula rushwa ndo mkombozi kwao, wamechoka sana maana 2015 kura zao zote lazima waziweke CHADEMA ili kujikomboa na udhalimu wa CCM.

(vii) WAKULIMA.

Waulizeni wakulima wa Tanzania walioko huko vijijini watakuelezeni watakachofanya 2015.Wakulima katika nchi hii wamekosa matumaini ya kuishi kabisa yaani wengine hawajui kama serikali ipo, wanalima masoko hakuna, michango kibao tena ambayo haina tija na mapato na matumizi hakuna, mfano fuatilia wakulima wa korosho huko kusini mwa Tanzania, wakulima wa kahawa, pamba, tumbaku, katani na mengine watakuleza jinsi walivyojipanga 2015 watakavyokipigia kura CHADEMA tena wameishajipanga kujiandikisha kwa wingi na wote kupiga kura na sio kupuuzia kama walivyofanya 2010 maana wengi walisema hawakupiga kura kwa sababu wamekata tamaa , sasa wamegundua kuwa kutopiga kura ni ujinga; piga kura kisha zilinde zisiporwe na magamba.Iwapo huamini hili zungukia wananchi mitaani watakuleza matumaini waliyo nayo kwa CHADEMA na siyo kwa chama chochote.

(viii) WAFANYA BIASHARA.

Waulize wafanya biashara watakwambia jinsi walivyochoshwa na utawala wa serikali ya ccm kwa kuwatoza kodi nyingi na kuwapa masharti magumu ya kibiashara kwa manufaa ya wachache.Wafanya biashara wanalipa kodi nyingi sana lakini badala ya matumizi ya kodo hizo kuwarudia huwanufaisha wachache, nenda mahospitalini madawa hakuna na wataalamu hakuna mpaka unde hospitali za watu binafsi, shule za serikali hakuna taaluma bora hivyo huwalazimu kuwapeleka watoto wao shule za binafsi kwa gharama kubwa ili kuona kama watoto wao wanaweza kupata taaluma bora, wamechoka kwa pamoja 2015 kura ni kwa CHADEMA ili waweze kuondokana na kadhia hizi(kawaulizeni wafanyabiashara watakuelezeni vizuri).

(ix) WATUMISHI WA MAHAKAMA.
Waulizeni watumishi wa mahakam watakuelezeni namna walivyochoka kutumiwa na serikali ccm kushinikiza kufanya maamuzi kwa matakwa yao lakini kwa kiasi fulani mahakama zetu bado zinaonekana kusimama kidete kutetea mhimili wale licha ya kwamba unaingiliwa na serikali(hawa wote 2015, kura ni kwa CHADEMA ili kuondoa kuingiliwa ovyoovyo na serikali, wataweka serikali yenye nidhamu)

(x) WANAJESHI NA ASKARI WOTE KWA UJUMLA)
Hawa wote wamechoka sana na wako tayari 2015 kukiweka CHADEMA madarakani ili waweze kupumua kwa kufanya utekelezaji wa majukumu yao bila kuingiliwa na siasa za magamba.

Ndugu zangu sijui mnataka niwape ushahidi gani ili muweze kuamini kwamba ccm 2015 kitakuwa ni chama cha upinzani bungeni tena hakitaongoza hata kambi ya upinzani, wao wenyewe wanaamini na wanalijua hilo wewe kwa nini usiamini? Katika wao ccm kulijua hilo ndo maana sasa hivi wanahaha kuhakikisha kuwa wananchi hawarushiwi matangazo ya moja kwa moja ya mijadala ya bunge ili kuficha madudu pale wanapozidiwa hoja na wapinzani bungeni eti kwa kigezo kwamba wapinzani wanapata credit, mko tayari kudanganyika na upuuzo huo? Wamefikia wakati wa kuwafukuza wabunge, majembe ya CHADEMA kwa hoja zao nzito na zenye ukweli kwa sababu wamewachachafya vibaya mno matokeo yake wamejilaumu wenyewwe na kukilaumu kiti cha spika kwamba kimewaongezea pointi CHADEMA maana walipotoka wananchi waliwapokea kama mashujaa watokao vitani na ushindi; Wanaandaa mkakati kuhakikisha mikutano ya CHADEMA kwa wananchi haiendelei kwa kuwatumia polisi kuzuia mikutano na maandamano.

Kama bado watu hawaani kwamba ccm inakufa muda si mrefu, baada ya katibu wao mkuu wa chama (kinana) kutuhumiwa kumiliki kampuni inayosafirisha meno ya tembo huko Uchina, ni hoja gani za msingi zemeletwa ili wananchi wapime ukweli ama uongo huo, tunashuhudia majibu ya kupwayapwaya.
Mtiririko wa kuwabambikizia kesi na kuwafunga wananchi ni dalili kwamba serikali ya ccm haina sera tena za kutekeleza tofauti na kuanza kuwafunga wananchi wake kwa kesi za kutengeneza. CCM wanmtegemea mtu kama Mwigulu ambaye kimsingi alishaonekana kwa wananchi kama mtu asiye na busara wala weledi wowote, kazi yake kubwa kutumia fedha ya walipa kodi na kuwahonga wenye njaa kujiunga na chama na kutengeneza video ambazo hazina mashiko wala tija yoyote kwa umma, leo anatwambia kamrekodi LWAKATARE na ugaidi mbona hajatuwekea video ile ya mshua iliyomuonyesha akitendwa na kwa nini hajatwambia kama ilikuwa ya kweli au ya kutengenezwa? SHAME TO HIM UNROCOGNIZED MEMBER OF FAMILY LIKE NAPE. Wote hawa wanaweza kujiua watakapopigwa mweleka 2015 wanahitaji ushauri mapema kabla ya tukio.

Nimalizie kwa kusema kwamba kama bado kuna watu hamjaamini kwamba 2015 CHADEMA itatawala nchi hii, mnasubiri kufufuka kwa Hayati baba wa Taifa Mwalimu Nyerere ili awaeleze ukweli maana hata nafsi yake huko alipo ahera inamuonyesha namna chama chake alichoacha madarakani kinavyoendelea kutafunwa na watu ambao awali alishawatilia mashaka kama wana uwezo wa kuongoza nchi ama la! NAWASILISHA.Ukipenda comment usipopenda acha ila nafsi yako itakwambia ukweli wa kilichoko hapo juu.
 
Kwa sie wenye huduma bora za mawasiliano ujumbe wako tumeupata,je watu wa vijijini uliko mtaji mkubwa wa ccm unawasaidiaje kuwafikishia ujumbe huu?
 
Mkuu shaka ondoa CCM wanajua kuwa mwisho wao umefika ndo maana wakagawana Nyumba za Serikali, Ndiyo maana wanaingia mikataba ya miaka 99, Ndiyo maana deni la Taifa linapaa... Haya yote ni sehemu ya maandalizi ya kuachia dola wakuu...
 
Wakati umefika wa mabadiriko wananchi wenyewe wameamua hakuna kurudi nyuma
 
kusema kweli muda umefika sasa kwa ruzuku inayotolewa kuelekezwa vijijini ili kuishinda na kusambaratisha adui ccm kwani huko ndipo mtaji wao wa kuvuna kura nyingi mkuu tumaini makene hili jambo tumeliongea sana ebu tufanya kwa vitendo na kwa hakika tutaweza kushinda kwa kura nyingi.


"kazi ni msingi wa maisha ya mwanadamu". mwl nyerere.
 
Hata mimi nina ndoto......

Nitawasilisha next time.....

Mmmmmh....ssssio kama ile ya babu Ambi wa Samunge.....Lakini zinashabihiana.
 
Back
Top Bottom