CHADEMA 2015 Tanzania ndicho chama tawala

CHADEMA 2015 Tanzania ndicho chama tawala

Nchi haifanyiwi majalibio mnaongoza halmashauri mbona hatuoni mabadiliko kisha tuwape nchi nyie oteni mngalimacho
 
Kama uko baa na unakunywa bia ya eagle ile ya buku Lazima akili zielekee kwny mawazo haya
 
Maccm yakiiba kura je?

Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums

Mkuu haibiwi mtu; Itumie haki yako ya kupiga kura vizuri, "Piga kura yako, itetee kura yako, na ilinde kura yako"; Hiyo ndo siri ya mafanikio.
 
Kwa sie wenye huduma bora za mawasiliano ujumbe wako tumeupata,je watu wa vijijini uliko mtaji mkubwa wa ccm unawasaidiaje kuwafikishia ujumbe huu?

Tushirikiane mimi na wewe kuwakishia ujumbe huu kwa wakati muafaka.
 
Lakini jaman kama uchaguzi ukifanyika leo Chadema itapata majimbo mengi na si kuongoza nchi maana bado hawajafika chini kwenye ngazi ya vijij mfano me niko huku masasi mtwara yaan chadema hamna kabisa napata kaz sana kutafuta wanachama ila bado sana

JEMEDARI. H., wewe tayari ni CHADEMA; anza kazi huko Mkuu.
 
Uze mrefu sana ntarudi baadae kuumalizia kusoma
 
Dunia ipo kwenye kipindi cha mabadiliko,ndio maana Amerika wameweza kumchagua Rais mweusi bwana Obama.
Hivyo hata, watanzania walio wengi wanaonyesha kuhitaji mabadiliko ya dhati ambayo inawabidi kufanya maamuzi magumu lakini yaliyo ndani ya uwezo kwenye sanduku la kura.
"Time will tell"
 
Kama kuna watu kijijini kwako bado wanajishebedua kwa CCM basi huko propaganda za kidini zitakuwa zimewakaa. Kijijini kwanguu ni tofauti. CCM ni jina tu yaani nyoka wa shaba. Hivi ni mara ngapi umesikia wananchi wanaomba M4C itembelee maeneo yao? Hiyo inatosha kukuonyesha kuwa CHADEMA imeshika. Binafsi kama CDM hawachukui nchi 2015 basi nitaacha kazi ili kuwa mwasiasa, mwanaharakati.
 
Bado kabisa kiosheni chama chenu kwanza na sifa za fujo udini na ukabila ndio tutazungumza kushika madaraka TZ
Watanzania ni waangalifu sana linapokuja suala la uongozi wa nchi
Mfano jamii forum kwa kiasi kikubwa inajulikana ni kigoda cha Chadema na hutumika kuonesha sera za CDM
Lakini chombo hichi kwa matusi kwa waislamu uislamu na Mitume yao ni jambo la kawaida na mfumo mzima huwa unashambulia uislam kwa kutukana bila ya mada kufutwa au kupigwa ban kwa mtukanaji
Waislam wengi pia ni memba wa mtandao huu wanaona hali ilivo
Hivo huu ni uchafu unatakiwa kuoshwa
Japo Zito alilisemea suala la udini na kuonesha kwamba CUF walasingiziwa na sasa ni CDM lakin Zito huwa ni mchangiaji humu na hajawahi kuwakemea wana chadema kujipesha na chuki za kidini humui mtandaoni
Wala si kiongozi yoyote wa CDM amewahi kukemea tabia ya kuonesha chuki na matusi kwa vijana wa CDM ndani ya mtandao huu
Jee itawezekana kweli kuingia ikulu kutegemea kundi moja hapa tanzania? HAIWEZEKANI
Muda upo utumieni kujisafisha na kujenga imani na kuwashirikisha waislam nao kujiunga CDM wawezesheni washike nafasi isiwe waislam ni zito na familia yake tu na Arfi
Inahitajika nia safi na ari ya kujenga Taasisi ya kisiasa isiyo kuwa na ubaguzi hivo mujiuluze jee tunayo nia hio ?
Ushawishi wa CDM na CUF unafanana kwa sababu Inakua vigumu kwa wasomi wa kikristo kujiunga na CUF kwa hisia za kidini na pia inakua vigumu kwa wasomi wa kiislam kuingia CDM huu ndio ukweli na ndio hapa pa kujisafisha kuleta matumaini kinyume chake ni CCM tu ndio inayo faidika

Sent from my BlackBerry 9700 using JamiiForums

Ndugu,hayo yote ulosema yameasisiwa na CCM, we hukumbuki propaganda hiz za udin,ukabila na ukanda? Wanachokifanya vijana wa Chadema,Lema na Slaa kwa kutaja wachache,wanawakumbusha ccm kit walichokiasisi sasa matokeo yake yameanza kutokea,sa hiz wameanza kuasisi ugaidi matokeo yake huwez kuyaona sa hiz ni mpaka baada ya miaka kadhaa! Masuala haya ndio yaloiua Cuf. Hapa wanachokifanya Chadema si udin bali wanakumbusha! Na Waislamu wote wanatakiwa waelewe na wang'amue na hata Wakristu pia ili nchi isonge.
N:B Tafadhali mi sifungamani na chama chochote cha kisiasa!
 
hiyo ndio hapari ya sasa....na ndio ukweli utaki kufa ili usijionee
 
Bange zingine msiwe mnavutia chooni huwa zinakuwa kali zaidi
 
Back
Top Bottom