SI KWELI Cetirizine Inabana Uke?

SI KWELI Cetirizine Inabana Uke?

Baada ya kuitathmini taarifa hii, tumebaini kuwa si ya kweli.
Source #1
View Source #1
Source #2
View Source #2
Madai yamekuwa yakisambaa kwenye mitandao ya kijamii yakisema kuwa dawa ya allergy aina ya cetirizine inaweza kutumika “kubana uke”, huku baadhi ya wanawake wakishauriwa hata kuingiza vidonge hivyo ndani ya uke.

Madai hayo yameenea kwa kasi kiasi cha kuripotiwa kuongezeka kwa mahitaji ya cetirizine katika baadhi ya maduka ya dawa nchini.

Lakini je, cetirizine kweli inaweza kubana uke?
eastleighvoice-co-ke-2026-november-04-162413.webp
 
Tunachokijua
Cetirizine ni dawa ya antihistamine inayotumika kutibu dalili za allergy, ikiwemo kupiga chafya, mafua ya mzio, macho kuwasha, ngozi kuwasha na hives. Dawa hiyo imetengenezwa kumezwa, si kuingizwa ndani ya uke.

Pharmaceutical Society of Kenya (PSK) imesema hakuna ushahidi wa kitabibu unaoonyesha kuwa cetirizine inaweza kubana uke au kuimarisha misuli ya uke.

Chanzo cha madai hayo kinaonekana kuhusishwa na ukweli kwamba antihistamines zinaweza kusababisha ukavu kama moja ya madhara yake kwa baadhi ya watumiaji.

Lakini wataalamu wanasema ukavu wa uke si sawa na uke kubana.

Kupungua kwa lubrication hakubadilishi muundo wa uke wala kuimarisha misuli yake. Badala yake, ukavu unaweza kuongeza msuguano, maumivu na uwezekano wa kujeruhi tishu nyeti wakati wa tendo la ndoa.

Je, kuingiza cetirizine ukeni ni salama?

Hapana.

Pharmacy and Poisons Board (PPB) imesema cetirizine haijaidhinishwa wala kufanyiwa majaribio kwa matumizi ya uke.

Kuingiza kidonge hicho ndani ya uke kunaweza kusababisha kuungua, kuwasha, maumivu, soreness na irritation. Pia kunaweza kuvuruga mazingira ya kawaida yanayolinda uke na kuongeza hatari ya maambukizi.

PSK pia imewataka watu ambao tayari wamejaribu njia hiyo kuacha, na kutafuta matibabu iwapo watapata maumivu, damu, kuungua, kuwasha, discharge isiyo ya kawaida au homa.

Serikali imesema nini?

Wizara ya Afya imeonya dhidi ya matumizi mabaya ya cetirizine baada ya madai hayo kusambaa mtandaoni.

Principal Secretary for Medical Services Ouma Oluga alisema mijadala ya mitandaoni inaweza kuwashawishi watu kutumia dawa kwa njia ambazo hazijaidhinishwa, na akasisitiza umuhimu wa kufuatilia matumizi salama ya dawa.

PSK pia imeripoti kuongezeka kwa mahitaji, bei na hata upungufu wa cetirizine katika baadhi ya maduka ya dawa, jambo linaloweza kuathiri wagonjwa wanaohitaji dawa hiyo kwa matumizi yake halisi ya kutibu allergy.


HUKUMU: Fake News


Dai kwamba cetirizine inabana uke halina ushahidi wa kisayansi.

Cetirizine inaweza kusababisha ukavu kwa baadhi ya watu kama side effect, lakini ukavu si kubana uke na haumaanishi misuli ya uke imeimarika au anatomy yake imebadilika.

Zaidi ya hayo, kuingiza cetirizine ndani ya uke si matumizi yaliyoidhinishwa na kunaweza kusababisha madhara.
Back
Top Bottom