Hizo siyo aina za cement!
Hizo ni grades za cement, na hiyo N inamaanisha Normal strength, R ikiwa na maana ya rapid strength!
Aina za cement zipo nyingi tu, mfano ni kama hizi:-
Ordinary Portland Cement (OPC),Portland Pozzolana Cement (PPC), Rapid Hardening Cement, Extra Rapid Hardening Cement, Low Heat Cement, Sulfates Resisting Cement, Quick Setting Cement, Blast Furnace Slag Cement...n.k!
Kwa Tz aina kuu ya cement inayozalishwa na kutumika zaidi ni OPC na hata PPC, ambazo huwa zinazalishwa grades
32.5N/ 32.5R,(Cement daraja la chini)
42.5N /42.5R.(cement daraja la juu)
Lakini pia ipo 52.5N/52.5R (ambayoni cement daraja la juu zaidi, kwa tz hii bado haipo).
Cement ambayo ni grade 32.5N/32.5R hii inafaa zaidi kwa matumizi ya plaster na kazi ndogo ndogo ambazo hazihitaji kuhimili uzito mkubwa!
Cement ambayo ni grade 42.5N/42.5 au daraja la juu zaidi inafaa zaidi kwa kazi za zege kama nguzo, bimu, slabu, madaraja n.k kutokana na uimara wake kuwa mkubwa zaidi.
Maana ya herufi N, kama nilivyoeleza ni normal strengh, hii ina maana ili kufikia ubora wake baada ya matumizi huchukua muda kidogo tofauti na cement ambayo ni R-rapid strenght ambayo hii huwahi zaidi kufikia ubora wake baada ya matumizi! Kawaida ubora wake hufikiwa kuanzia siku 2-7.
Hivyo naamini kwa maelezo haya mafupi unaweza kuamua utumie cement yenye grades zipi kwa matumizi gani!