CECAFA Challenge Cup | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

CECAFA Challenge Cup

Discussion in 'Sports' started by Mfumwa, Dec 30, 2008.

 1. M

  Mfumwa JF-Expert Member

  #1
  Dec 30, 2008
  Joined: Aug 29, 2008
  Messages: 1,456
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Uganda prepares for Cecafa

  Ten nations will compete for the East and Central Africa Senior Challenge Cup (Cecafa Cup) which starts in Uganda on Wednesday.

  The hosts, who have won the event a record nine times, are seeking their first triumph in five years and are in Group A with Tanzania, Rwanda, Zanzibar and Somalia.

  Uganda finished third in last year's event in Tanzania, behind Sudan and Rwanda.

  Defending champions Sudan are in Group B alongside Kenya, Burundi, Djibouti and guests Zambia with the top two sides in each group qualifying for the semi-finals

  The opening games of the tournament are in Group B with Zambia playing minnows Djibouti and Sudan facing Kenya.


  Zambia will participate as guests, after being invited to replace Eritrea, who withdrew from the two-week tournament.

  The Zambians won the tournament in 2006 in Addis Ababa, having also been invited as guests then.

  Kalusha Bwalya, the president of the Zambia Football Association, has said the tournament will be ideal preparation for the year ahead.

  "We're very happy the Cecafa executive invited us to this regional tournament because it will help our team prepare better for both the African Nations Championship (CHAN) and the 2010 World Cup and African Cup of Nations qualifyiers," he said.

  Kenya, Rwanda and Sudan go into the tournament on a high as East Africa's representatives in the final phase of the World Cup and Africa Cup of Nations qualifiers, which begin in March.

  Tanzania will also be using the event as a warm-up for the first ever finals of the CHAN, which kick off in the Ivory Coast on 22 February.

  The Tanzanians already have a psychological advantage over 2007 Cecafa champions Sudan, having only recently knocked them out of the CHAN qualifiers.

  Kenya coach Francis Kimanzi has said he is giving the tournament the same respect as the World Cup qualifiers.

  Burundi have yet to win the event, with their best showing coming as runners-up to Ethiopia in 2004.

  Ethiopia are prevented from taking part as they are serving a Fifa suspension.

  Source: BBC SPORT | Football | African | Uganda prepares for Cecafa
   
 2. B

  Babuji Senior Member

  #2
  Dec 30, 2008
  Joined: Nov 27, 2008
  Messages: 198
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  [​IMG]
  Kocha Mkuu wa timu ya Kilimanjaro Stars, Marcio Maximo, akizungumza na wachezaji wa timu hiyo mara baada ya mazoezi yao kwenye Uwanja wa Karume Dar es Salaam leo asubuhi, kwa ajili ya kujiandaa na michuano ya Chalange inayofanyika nchini Uganda inayoanza kesho.


  [​IMG]
  Wachezaji wa timu ya Tanzania Kilimanjaro Stars, wakiwa kwenye mazoezi Uwanja wa Karume Dar es Salaam, kujiandaa na michuano ya Chalange inayoanza kesho nchini Uganda.

  source: NIFAHAMISHE Tanzania news portal
   
 3. M

  Mfumwa JF-Expert Member

  #3
  Dec 31, 2008
  Joined: Aug 29, 2008
  Messages: 1,456
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Tunakwenda kufanya vizuri-Maximo

  William Mjema
  Daily News; Tuesday,December 30, 2008 @21:15

  Timu ya Kilimanjaro Stars ikiwa inaondoka leo, Kocha Marcio Maximo amesema ana imani kikosi chake kitafanya vizuri katika michuano ya Kombe la Chalenji inayotarajia kuanza leo. Michuano ya Kombe la Chalenji inayotarajia kuanza kutimua vumbi leo inatarajia kufikia tamati yake Januari 13, Kampala, Uganda na inashirikisha nchi 11.

  Maximo alisema kuwa wachezaji wake wamefanya mazoezi ya kutosha na kuahidi kuonyesha ushindani wa hali ya juu. “Siku zote mimi si mtu wa kutoa ahadi, ila tunakwenda tukiwa na lengo moja la kushinda, wachezaji wangu wako katika hali nzuri na wako tayari kufanya kila wawezalo ili kuwa na matokeo mazuri,” alisema Maximo.

  “Tumejiandaa vizuri, na ninajua kuwa mechi itakayokuwa ngumu kwetu ni ile dhidi ya Zanzibar kwa sababu hawa ni ndugu zetu na tunajuana kwani kuna baadhi ya vijana wangu wako huko,” alisema. Naye Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Abbas Kandoro ameitaka timu ya Kilimanjaro Stars kushuka dimbani wakijua kuwa wanatakiwa kurudi nyumbani na ushindi wa michuano hiyo ya 33 ya Kombe la Chalenji.

  Kandoro alitoa wito huo, jana baada ya kukabidhi bendera ya taifa kwa nahodha Henry Joseph wakati wa hafla ya kuwaaga. Kilimanjaro Stars inatarajia kuondoka leo jioni kwenda Kampala, Uganda tayari kwa mashindano ya michuano hiyo. “Hivi sasa Tanzania ni miongoni mwa timu nzuri katika kanda hii, hivyo mnahitajika kucheza kwa juhudi ili kuendeleza rekodi.

  Nina imani mmefanya mazoezi ya nguvu na imani yangu kuwa mtatufanya tujisikie ufahari kwa kurudi na kombe,” alisema Kandoro. Naye Makamu wa Kwanza wa Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Athumani Nyamulani amewashauri wachezaji kutumia mashindano hayo kuonyesha vipaji vyao kutokana na kuwa mashindano hayo yanatarajia kuwakutanisha mawakala kutoka sehemu mbalimbali.

  “Macho yote ya wadau wa soka yataelekezwa Uganda kwa wiki mbili, hivyo ni nafasi yenu ya kujitangaza na kupata soko la kucheza soka ya kulipwa,” alisema. Aidha, Nyamlani alisema: “Mapokezi waliyoyapata Taifa Stars kwa Waziri (Muhammed) Seif Khatib (Waziri Ofisi ya Rais-Muungano) kuzunguka na wachezaji kwenye gari la wazi yatakuwa madogo, kwani ninyi mkirudi na kombe basi Mkuu wa Mkoa (Abbas) Kandoro atatembea na mkokoteni".

  Kilimanjaro Stars imepangwa kundi A ikiwa pamoja na timu za Somalia, Zanzibar, Rwanda na wenyeji Uganda. Tanzania inarusha karata yake ya kwanza Jumamosi kwa kumenyana na Somalia na siku mbili baadaye inatarajia kucheza na ndugu zao wa Zanzibar. Januari 7 mwakani, Kilimanjaro Stars itaumana na Rwanda ambayo katika michuano iliyopita ilifika hatua ya fainali na inatarajia kumaliza hatua ya makundi ya michuano hiyo kwa kuonyeshana kazi na Uganda, Januari 9.

  Kikosi cha Maximo kinatarajia kutumia michuano hiyo inayojumuisha nchi 11 za Afrika Mashariki na Kati kujiandaa na fainali za Mataifa ya Afrika kwa wachezaji wanao cheza Ligi ya Ndani (Chan) inayotarajia kuanza Februari 22 hadi Machi 8 mwakani, Abidjan, Ivory Coast. Katika michuano hiyo Stars inatarajia kuanza na Senegal.

  Wachezaji anaotarajia kuondoka leo ni Shaban Dihile, Deo Mushi, Shadrack Nsajigwa, Kelvin Yondani, Amir Maftah, Salum Swed, Juma Jabu, Geoffrey Bonny, Athuman Idd na Nurdin Bakari. Wengine ni Kigi Makasi, Henry Joseph, Haruna Moshi, Musa Hassan ‘Mgosi’, Mrisho Ngasa, Jerry Tegete na Danny Mrwanda. Viongozi ni Maximo na msaidizi wake Marcos Tinoco, timu Meneja Leopold Mukebezi, Meneja wa vifaa Fred Chimila na daktari Juma Sufian.
   
 4. Bubu Msemaovyo

  Bubu Msemaovyo JF-Expert Member

  #4
  Dec 31, 2008
  Joined: May 9, 2007
  Messages: 3,436
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 145
  Halafu leo alfajiri nikiwa nasikiliza BBC nilisikia kwamba timu ya Zambia imealikwa kushiriki mashindano hayo nilikuwa usingizini sikusikia vizuri mwenye taarifa muafaka anijulishe niwe na uhakika.
   
 5. M

  Mfumwa JF-Expert Member

  #5
  Dec 31, 2008
  Joined: Aug 29, 2008
  Messages: 1,456
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Bubu Msemaovyo, ni kweli timu ya Zambia imealikwa kuchukua nafasi ya Eritrea ambayo ilijitoa.
   
 6. Belo

  Belo JF-Expert Member

  #6
  Dec 31, 2008
  Joined: Jun 11, 2007
  Messages: 11,274
  Likes Received: 4,259
  Trophy Points: 280
  Mods hizi topic za CECAFA ziko 2 mziunganishe
   
 7. M

  Mfumwa JF-Expert Member

  #7
  Jan 1, 2009
  Joined: Aug 29, 2008
  Messages: 1,456
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Zambia yarejea Chalenji kwa ushindi
  Michael Momburi, Jinja

  MICHUANO ya Kombe la Chalenji imeanza mjini hapa kwa kushuhudia Zambia ikiilaza Djibouti mabao 3-0 na Kenya na Sudan zikigawana pointi baada ya kushindwa kufungana.


  Lakini, hali ya uwanja wa michezo wa Bugembe mjini hapa ambako ufunguzi ulifanyika ilizua malalamiko kutoka kwa timu zinazoshiriki michuano hiyo kuwa haufai na hauna hadhi inayolingana na michezo yenyewe.


  Awali, Zambia 'Chipolopolo' ilianza vizuri baada ya kuitandika Djibouti mabao 3-0 katika machezo wa ufunguzi uliofanyika katika Uwanja wa Bugembe uliopo, Jinja, kilometa 80 kutoka Kampala.


  Zambia iliyoingia katika michuano hiyo kama mwalikwa baada ya Eritrea kujitoa, ilianza kupata bao katika dakika ya 25 lililofungwa na Given Singuluma.


  Singuluma aliyonekana mwiba kwa timu ya Djibouti, aliongeza bao la pili kwa timu yake katika dakika ya 32.


  Wakati kila shabiki akiamini kuwa timu hizo zitakwenda mapumziko kwa matokeo hayo, Jonas Kakuhawa aliiandikia Zambia bao la tatu.


  Kipindi cha pili kilianza kwa kasi na kila timu ikitaka ama kuongeza bao au kusawazisha, lakini milango ilikuwa ni migumu na mabekiwa timu zote walikuwa makini kuondoa hatari zilizoekekezwa kwao.


  Baada ya mchezo huo, kocha mkuu wa Zambia, Herne Renald alilalamika uwanja wa Bugembe kuwa ni mbovu na mkavu akiulinganisha na ule wa Chuo Kikuu cha Zambia.


  Nazo Kenya na Sudan zilishindwa kutambiana baada ya kutoka suluhu 0-0 katika mchezo wa pili wa Kombe la Chalenji uliofanyika kwenye uwanja huo mkavu wa Bugembe.


  Katika mchezo huo, Harambee Stars hawakucheza soka ya kuvutia ikilinganishwa na Sudan ambayo ilikuwa na wachezaji sita waliocheza dhidi ya Taifa Stars. Kenya iliwachezesha wakali wa Yanga, John Baraza na John Njoroge, lakini haikuonyesha umakini.


  Baraza, George Owno , wote wa Yanga hawakuonyesha viwango vyao, Joseph Shikokoti alikuwa benchi. Kocha alimtoa Baraza katolewa kaingia Francis Ochieng.


  Lakini, wachezaji wa pande hizo walidai hawakuweza soka la kuvutia kutokana na ubovu wa uwanja.


  Mkurugenzi wa ufundi wa Sudan, Ahmed Babiker aliulalamikia uwanja, akisema umechangia kuwaathiri na kuongeza kuwa wao wanatengeneza timu mpya.


  Kocha wa Kenya, Francis Kimanzi aligoma kuzungumza mchezo huo, lakini Owino na wenzake walionekana wakimzonga mwamuzi Ally Kalyango wa Uganda.


  Wakati huo huo, Uganda Cranes imewatema wachezaji Simon Senkuruma, Benjamin Ochan, Derick Warurya, Owen Kasule, Yuda Mugalu, Jimmy Mukubya, Ema Okwu, God Walusimbi kwa madai kuwa hawapo fiti kwa mchezo dhidi ya Zanzibar Heroes leo.


  Katika hatua nyingine, waumini wa Kikrsito 'walokole' zaidi ya 3,000 kutoka mikoa yote ya Uganda wamekusanyika katika Uwanja wa Mandela ulioko Namboole mjini hapa kwa mkesha wa mwaka mpya jana wakisali ikiwa ni siku mbili kabla ya Kilimanjaro Stars haijacheza na Somalia uwanjani hapo .


  Mgeni rasmi katika mchezo wa Uganda na Zanzibar atakuwa Janet Museveni, mbunge na mke wa Rais Yoweri Museveni.


  Kilimanjaro Stars iliyotarajiwa hapa jana usiku iliandaliwa mapokezi yaliyoongozwa na kocha Frank Anyau 'Video' akiwa na jukumu la kusimamia kila kitu . Kocha huyo ni mmoja kati ya watu walioko karibu sana na benchi la ufundi la Uganda. Kwa Uganda, wanamuita Kocha wa 'Reserve'.


  Uganda wameahidiwa asilimia 50 ya zawadi ya ubingwa, msemaji wa Rais wa Fufa (Shirikisho la Soka Uganda), Lawrance Mulindwa alieleza.


  Katika tukio jingine, timu ya Kenya, Harambee Stars ikiwa na wachezaji wa Yanga, Joseph Shikokoti, John Baraza juzi ililala njaa Jumatatu ilipokwenda Jinja kwenye hoteli ya Triangle kwa kuwa hakukuwa na taarifa kwa uongozi wa hoteli.
   
 8. N

  Nurujamii JF-Expert Member

  #8
  Jan 1, 2009
  Joined: Jun 14, 2007
  Messages: 414
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Zanzibar yaifunga Somalia 2-0
   
 9. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #9
  Jan 1, 2009
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,606
  Likes Received: 82,181
  Trophy Points: 280
  Zambia na Malawi si ziliwahi kushiriki Challenge cup miaka ya nyuma?

  Nakumbuka nusu fainali kama sikosei ya mwaka 79 ambapo Tanzania na malawi zilicheza dakika 120 kwa siku mbili bila kupata mshindi na hatimaye kuamuliwa kwa miguu 12 ya mtu mzima mwenye akili timamu ambapo tulitolewa. Mechi zote mbili zilikuwa ni kali sana na kandanda lilionyeshwa na timu zote mbili lilikuwa la hali ya juu.
   
 10. M

  Mfumwa JF-Expert Member

  #10
  Jan 2, 2009
  Joined: Aug 29, 2008
  Messages: 1,456
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Uganda yaiadhibu Rwanda 4-0. Sasa tusubiri timu yetu Jumamosi itakapofungua dimba na Somalia.
   
 11. M

  Mfumwa JF-Expert Member

  #11
  Jan 2, 2009
  Joined: Aug 29, 2008
  Messages: 1,456
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Burundi 4 - Djibout 0
  Zambia 0 - Kenya 0
   
 12. M

  Mfumwa JF-Expert Member

  #12
  Jan 3, 2009
  Joined: Aug 29, 2008
  Messages: 1,456
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
 13. Belo

  Belo JF-Expert Member

  #13
  Jan 3, 2009
  Joined: Jun 11, 2007
  Messages: 11,274
  Likes Received: 4,259
  Trophy Points: 280
 14. M

  Mfumwa JF-Expert Member

  #14
  Jan 3, 2009
  Joined: Aug 29, 2008
  Messages: 1,456
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Gemu imeisha.
   
 15. Nyambala

  Nyambala JF-Expert Member

  #15
  Jan 3, 2009
  Joined: Oct 10, 2007
  Messages: 4,470
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Du tunafungwa mpaka na Somalia????? kweli mzee ruksa hakukosea
   
 16. Shadow

  Shadow JF-Expert Member

  #16
  Jan 3, 2009
  Joined: May 19, 2008
  Messages: 2,908
  Likes Received: 71
  Trophy Points: 145
  Tanzania imefungwa leo na Somalia bao 1-0. Bao lililofungwa na mchezaji wa Zamani wa Simba, Bushiri. Somalia walifungwa kwenye mechi yao ya Kwanza na Zanzibar bao mbili kwa tairi. Bao la Somalia lilifungwa katika kipindi cha kwanza. Mtunange huo ulipigwa katika dimba la Nakivubo

  Tanzania hiko kwenye nafasi finyu ya kwenda raundi ya pili.
   
 17. share

  share JF-Expert Member

  #17
  Jan 3, 2009
  Joined: Nov 22, 2008
  Messages: 2,293
  Likes Received: 2,277
  Trophy Points: 280
  Kushabikia mpira wa Tanzania inahitaji uwe na moyo kama wa mwendawazimu. La sivyo, ni rahisi kuwa chizi au kupandisha presha. Timu inayofuata kucheza nayo ni jamaa zetu wa Zenji. Nasikia wazenji wameapa ni afadhali wafungwe na timu zote lakini si Kilimanjaro stars. Kazi ipo bara!
   
 18. Shadow

  Shadow JF-Expert Member

  #18
  Jan 3, 2009
  Joined: May 19, 2008
  Messages: 2,908
  Likes Received: 71
  Trophy Points: 145
  sipati picha maximo atakuja na stori gani? Naona ze kilimanjaro ni kama arsenal siku hizi!!
   
 19. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #19
  Jan 3, 2009
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,606
  Likes Received: 82,181
  Trophy Points: 280
  Yaani hii ni aibu ya hali ya juu. Tunafungwa na Somalia kweli nchi ambayo haina serikali na wanauana kila kukicha sijui hata kama timu yao ilikaa kambini!!! maana nchi nzima imejaa vita vya wenyewe kwa wenyewe!!! Duh! hatuna consistency yeyote katika uchezaji wetu maana tunaweza kufungwa na timu ambazo hazistahili hata kutufunga!!!! Wana kazi ngumu sana ya kuendelea na mashindano hayo maana inabidi washinde mechi zote walizobakisha tena kwa magoli mengi na timu nyingine nzuri kwenye kundi lao kufanya vibaya. Yaani mimi nilidhani tutavuna kapu la magoli kumbe bado ni kichwa cha mwendawazimu!!!!!
   
 20. Shadow

  Shadow JF-Expert Member

  #20
  Jan 3, 2009
  Joined: May 19, 2008
  Messages: 2,908
  Likes Received: 71
  Trophy Points: 145

  Bubu ataka kusema, mwezi huko bado mchanga mwendawazimu hupata nafuu mwezi hukiwa full!
   
Loading...