CECAFA Challenge Cup

Full time score tumeshinda 3-2 sasa macho yetu yote ni mwezi ujao kule CHAN Ivory Coast mimi napendekeza Striking patners wawe 7. Mrisho Ngasa 9. Dany Mrwanda 10. Jerry Tegete hapa lazima upate mabao umesikia Maximo na maandalizi tuanze mapemaaaa
 
Your are right kuhusu hiyo combination lakini mrwanda hata weza kucheza kwani yeye anahesabika anacheza soka nje ya nchi, then he has to find some one to take mrwas position. Hukuliona hilo au ndo mrwanda kasha rudi kama Nizal?
 
Hongra sana vijana wetu, afadhali mmetufuta machozi. Ila kuna kitu nimekigundua kuhusu kili/taifa stars. TUNA MATATIZO KTK DEFENCE SYSTEM. Why kila mechi ndani ya dk 45 za mwanzo lazima tupigwe? Refer somalia, znz, Uganda, Kenya, na Burundi games. Wadau wa Soka mnalionaje hili?

Thanx!!!

Aljuniortz
 
Unajua kuchambua na kuanalyse performance ya timu, kuna uwezakano mkubwa, lakini inaweza changiwa na viungo wa kati kutokuwa wazuri kiasi kwamba wanawapa mabeki mzigo mkubwa na pia washambuliaji, mimi nafikiri Maximo aweke viungo wa kati sawa, kwani uhai wa timu upo kwa viungo , sijui kama nimekosea lakini hiki ndicho nachofikiria mimi, hatuwezi shinda katu kama viungo ni wabovu. Mnielimishe wenye kujua vizuri.
 
Mkuu hapa umeegemea upande mmoja..tukumbuke CHAN wanaenda Taifa Stars (The Blues of Africa) na si Kilimanjaro Stars..

Kili Stars = Taifa Stars - (Abdi Kassim; Nadir Haroub & Ali Bushiri tu!). Kwa hiyo kuitakia kila la heri Kili Stars ni sawa tu na kuitakia kila la heri Taifa Stars
 
Hongra sana vijana wetu, afadhali mmetufuta machozi. Ila kuna kitu nimekigundua kuhusu kili/taifa stars. TUNA MATATIZO KTK DEFENCE SYSTEM. Why kila mechi ndani ya dk 45 za mwanzo lazima tupigwe? Refer somalia, znz, Uganda, Kenya, na Burundi games. Wadau wa Soka mnalionaje hili?

Thanx!!!

Aljuniortz

Nafikiri sasa kuna haja ya Maximo kumsamehe Kaseja. Inasemekana tatizo letu kule Uganda lililikuwa ni moja tu: Golkipa! Kulingana na maelezo ya wadau, tungekuwa na kipa mzuri tungechukua kombe!
 
Kasja bwana anafaaa, lakini sijui tatizo na maximo ni nini kiasi kwamba jamaa kakomaa hamsamehi utafikiri jamaa alikua anamchukulia mkewe!!!!
Lakini inabidi atafute golikipa kama kaseja.
 
Kilimanjaro Stars yawafariji Watanzania
Uganda mabingwa wa Chalenji 2009

Michael Momburi,Kampala

KILIMANJARO Stars jana jioni iliwafariji Watanzania baada ya kuifunga Burundi mabao 3-2 huku ikicheza soka lisilovutia na kuchukua ushindi wa tatu wa Kombe la Chalenji.

Stars ambayo ilikuwa na wachezaji wake wote tegemeo kama Shadrack Nsajigwa na Kelvin Yondani waliokosekana katika mechi iliyopita dhidi ya Kenya, ilicheza soka la kuonekana dakika 30 za mwisho.

Kiwango hicho kilionekana kupanda haswa baada ya kuingia kwa Nizar Khalfan na Mussa Hassan pamoja na kupata bao la kusawazisha na la ushindi.

Burundi ambayo ilikuwa ikishangiliwa sana na mashabiki wa Uganda ilitawala idara zote kwa takribani dakika 60 za mchezo huku wakipiga pasi nyingi kadri wanavyotaka.

Stars ambayo beki wake wa kushoto Juma Jabu alicheza chini ya kiwango, iliitumia dakika mbili kupata bao la kuongoza lililofungwa na Mrisho Ngassa ambaye aliunasa mpira na kuwachomoka mabeki wa Burundi waliokuwa wakijipanga.

Mpira huyo ulianza kwa kasi ya kawaida, lakini dakika ya nne Henry Joseph alizidiwa ujanja na kumkwatua mshambuliaji wa Burundi, Nahimana Claude na kusababisha penalti ambao ilifungwa kirahisi na Irambona Abdallah dakika ya tano.

Stars ambayo haikuwa ikipandisha mashambulizi ya haraka kama katika mchezo dhidi ya Rwanda na Zanzibar, ilitengeneza nafasi nzuri dakika tisa, lakini Mrwanda aliponasa pasi ya Henry Joseph akakokota na kupaisha.

Burundi ambao bado walionekana kutulia na kupanga mashabulizi ya hatari kimahesabu, walikuwa wakimiliki mpira kwa kiasi kikubwa lakini Nsajigwa aliwaponyoka dakika ya 16 na kupandisha shambulizi kali lakini shuti lake likapaa.

Warundi hao wakimtegemea zaidi mshambuliaji wao Nahimaha Claude mwenye mabao matatu, waliivamia ngome Stars mara kadhaa na kuitoa kijasho.

Nahimana alikokota mpira na kumvuka Henry Joseph na Kelvin Yondani, mashabiki wote wa Tanzania wakaweka mikono kichwani lakini kipa Shabaan Dihile akauwahi miguu kwa mchezaji huyo.

Burundi chini ya kocha wake Gilbert Younde ambae juzi alisema Tanzania haiponi, ilipata bao la pili dakika ya 42 kupitia kwa Jafari Jumapili aliyeunganisha krosi ya Nahimana.

Kipindi cha pili kilianza kwa Burundi kuingia kwa kasi na kukosa nafasitatu za wazi, lakini Stars ilijipanga na kusawazisha dakika 68 kupitia kwa Jerry Tegete ambae alipokea krosi Shadrack Nsajigwa,mchezaji mwenye umri mkubwa kwenye kikosi cha Stars.

Tanzania ilionyesha uhai baada ya kupata bao hilo ambapo walitulia na kupiga pasi fupi fupi huku Burundi wakiwa wamerudi kujilinda lakini wakawa wanapanga mashambulizi ya kushtukiza ambayo yalikuwa yakiwaweka kwenye wakati mgumu Yondani na Jabu.

Dakika ya 76 Danny Mrwanda ambae alikuwa akicheza huku akihisi maumivu kwenye enka ya kulia, aliifungia Stars bao la ushindi kwa shuti baada kunasa pande la Ngassa.

Mrwanda ambaye alifikisha mabao matatu katika mchezo huo, alionekana kuichachafya safu ulinzi ya Burundi sambamba na Ngassa lakini viungo walikuwa wakiwapandishia mipira ya juu ambayo mara nyingi haikuwa na madhara kwa Burundi.

Katika mchezo huo Burundi ilionekana kujiamini zaidi huku kocha wake Younde akiwa amesimama kwa dakika zote tisini kuhamasisha vijana wake ambao walilala uwanjani baada ya kipyenga cha mwisho cha mwamuzi Issa Kagambo wa Rwanda.

Kocha wa Stars, Marcio Maximo alisema vijana wake walipigana kufa kupona kusaka ushindi huo kwani Burundi ilimiliki sana hususani kipindi cha kwanza.

"Tulijipanga vizuri na wachezaji wangu wamecheza mpira mzuri kipindi cha pili, michezo hii imetusaidia kuelewa zaidi timu na ni maandalizi mazuri kwa michuano ya CHAN."

Kocha wa Burundi, Younde alilaumu safu yake ya ulinzi kwa kushindwa kulinda ushindi huku washambuliaji wakiwa na papara walipokuwa wakikaribia lango la Tanzania.

Kwa ushindi huo Stars imejinyakulia dola 10,000 tofauti na awali ilivyotuwa jijini hapa ambapo mashabiki walikuwa wakiipa nafasin kubwa ya kutwaa ubingwa.

Stars; Shabaan Dihile,Shadrack Nsajigwa, Juma Jabu, Kelvin Yondani, Henry Joseph, Kiggi Makasi/Nizar Khalfan, Nurdin Bakar/Jerry Tegete, Danny Mrwanda/Mussa Mgosi, Mrisho Ngassa na Athuman Iddi.

Source: Mwananchi Read News
 
RESULT
Uganda 1-0 Kenya

THIRD PLACE MATCH

Tanzania 3-2 Burundi

ROLL OF HONOUR TITLES
1- Uganda 10
2-Kenya 5
3-Sudan 3
4-Malawi 3
5-Ethiopia 2
6-Tanzania 2
7-Zambia 2

Pedigree does matter in football after all. The Uganda Cranes yesterday cemented their reputation as the most feared team in Cecafa Senior Challenge Cup history when they beat Kenya’s Harambee Stars 1-0 in the final to capture their tenth trophy.

Cranes player hold the Cecafa Senior Challenge Cup aloft. It was the Cranes’ tenth trophy in the history of the competition. PHOTO BY EDDIE CHICCO.


Fufa Footballer of the Year Brian Umwony netted the all important goal to confirm his status as the rising star of Ugandan football. It was his fifth goal of the tournament, giving him the Golden Boot, ahead of Kenyan Francis Ouma.

Kenya were quicker out of the blocks with their front pair, Ouma and Mike Baraza troubling the Cranes back four with their slick movement. The tide of the game however shifted 15 minutes into the game. First, Tony Mawejje blasted wide after being set up by Steven Bengo. Then came the goal. Francis Kimanzi’s well drilled Stars failed to clear a short corner between Bengo and Vincent Kayizzi, allowing Umwony to use his goal poaching instincts to devatating effect.

Two minutes later, Geoffrey Massa broke, only to be stopped in his tracks by George Owino. The resulting Habib Kavuma free kick was saved by Kenya’s custodian Duncan Ochieng.

Harambee Stars continued to probe, but they found the Cranes back four, marshalled by skipper Andy Mwesigwa and Edward Ssali in uncompromising mood. Joseph Shikokoti and Eric Ochieng were booked in quick succession soon after the break, for illegally stopping Massa, whose pace continued to trouble the back four.

Coach Bobby Williamson replaced the tired Vincent Kayizzi and Steven Bengo with Dan Wagaluka and Robert Kimuli respectively. But once again, it was Umwony who headed against the cross bar five minutes to full time, before Kimuli drew a save from Ochieng two minutes later. “I congratulate my players. It was magnificent for them to bring so much joy to Ugandans,” Williamson said.
Kimanzi attributed Cranes’ victory to luck.
 

Attachments

  • cecafa-cranes-victory.jpg
    cecafa-cranes-victory.jpg
    28.5 KB · Views: 45

Similar Discussions

Back
Top Bottom