Cdm tv asap

Dr-of-three-Phd

JF-Expert Member
Oct 20, 2010
202
30
Wandugu wapendwa nimeonelea niliseme hili kwa CDM kwani habari zinaminywa sana kwa wananchi uhuru wa habari wa kupata habari kwa mwananchi pale anapotaka yeye kuzipata kikatiba umeminywa sana.

CDM wamekuwa na mkakati unaoonekana dhahiri shahiri unamanufaa kwa nchi na wananchi wake hasa ukizingatia chama kinachotawala kwa sasa kinatumia malalamiko ya CDM kujirekebisha na hata kuwanufaisha wananchi kwa kutumia taarifa hizo.

Sasa kama kweli CDM inafanya yaliyo mema kiasi hiki kwanini vyombo vya habari hususani Televisheni za umma ambazo ni mali ya umma wa Tanganyika na Zanzibar (TBC na TVZ) za kodi za wanannchi waliokwenye kila chama, wanaokatwa kodi za nyumba bidhaa, viwanja, biashara, mafuta, chakula, mishahara (payee) yao visioneshe kile kinachofanyika huko kwenye misafara ya CDM watu wajue na waone kinachoendelea kilichokuwa kinatakiwa kifanyike na chama cha serikali ya chama Tawala.

Badala yake habari zinatolewa visivyo, zikiwa zimechakachuliwa! wananchi wanaanza kuamini yasiyo ya kweli...

Hivi huu umuhimu hauonekani? CDM hebu tuambieni nini kinashindikana, je kuna urasmu wa kupata masafa ya mawasiliano (mafupi au marefu au ya setelite) au leseni au ni mtaji au ni ninii?

Kama kuna wa kujibu na kulielezea hili kutoka CDM nitashukuru sana.

Na nabakia kurekebishwa pale nitakapokuwa nimeleza vile nisivyo jua na hali halisi na mipango ya CDM.

Aluta continue
 
Back
Top Bottom