CDM kuingia madarakani? Vunja nguzo hiz za CCM, otherwise ni ndoto | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

CDM kuingia madarakani? Vunja nguzo hiz za CCM, otherwise ni ndoto

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by NYAMKANG'ILI, Sep 17, 2012.

 1. N

  NYAMKANG'ILI JF-Expert Member

  #1
  Sep 17, 2012
  Joined: Apr 1, 2012
  Messages: 223
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Prof Shivji aliwahi kusema nguzo za KATIBA TANZANIA, na hivyo nguzo za utawala wa CCM ni: (1) chama kimoja CCM; (2) MUUNGANO TZ na ZANZ; na (3) urais wa kifalme (imperial presidency). HAYA yalikuwa ya kale, yaliwahi kuwapo na zilikuwa nguzo za kweli za CCM.

  Kwa sasa nguzo za CCM za kuvunja ili kuingia ikulu CDM ni hizi: (1) urais wa kifalme ambao umempatia RAIS mamalaka makubwa ya uteuzi wa watu lukuki ktk nafasi za madaraka, huu umefanya watendaji wa serikali wasitumikie wananchi na nchi kwa ujumla wake na badala yake wanatumikia RAIS, na kwa kuwa RAIS ni m/kiti wa CCM basi wanatumikia CCM badala ya kutumikia wananchi. Watu wanajipendekeza ili wateuliwe au wasiondolewe kwenye nafasi walizopewa; (2) ufisadi kama wa EPA, MEREMETA, DEEPGREEN nk ambao unaipatia CCM pesa chafu za kufanyia siasa ambazo vyama vingine havina. Mfumo wa ufisadi unatumiwa sana kukandamiza wapinzani kwani CCM inawaambia watumishi kuwa iwapo kitatoka madarakani CDM kitawanyang'anya mali zote walizopata kupitia ufisadi, kinawatia hofu ya mabadiliko na kuahidi kuwalinda na mali zao za wizi; (3) vyombo vya habari ambavyo vingi vinamilikiwa na mafisadi wa CCM, vyombo hivi vinatumika kuhakikisha hakuna ajenda ya maana inayopita na kuwafikia wananchi; NA (4) vyombo vya mabavu kama polisi, TISS, PCCB na JWTZ ambavyo makamanda wake wote ni CCM damu na baada ya kustaafu wanakwenda kugombea ubunge kupitia CCM, na wengine hata wanagombea wakiwa bado kazini mfano mzuri ni maafisa wa PCCB 5 waliogombea ubunge 2010 kupitia CCM na mmoja wao aligombea (kura za maoni CCM) jimbo la mzee MZINDAKAYA na waliposhindwa walirudi kazini, hawa wanapambana kuhakikisha CCM inabaki. Kamati ya MKAMA iliyochunguza kwa nini CCM ilipata matokeo mabaya uchaguzi 2010, pamoja na mambo mengine, iliinyoshea kidole PCCB kwamba ni moja ya sababu ikidai kuwa inakamata watu wao na kuitangaza CCM kuwa ni ya mafisadi, hii inajibu swali kwa nini mwaka huu 2012 kwenye chaguzi za CCM zinazoendelea PCCB haijaonekana mpaka sasa, inatii maelekezo ya CCM.
   
 2. M

  Mindi JF-Expert Member

  #2
  Sep 17, 2012
  Joined: Apr 5, 2008
  Messages: 1,393
  Likes Received: 945
  Trophy Points: 280
  Nadhani ishu siyo CHADEMA kuachiwa peke yake kazi ya kuing'oa CCM kwenye madaraka, bali wananchi walala hoi walio wengi kuamua kwamba sasa basi, watumie haki yao ya kimsingi kukataa kuendelea kunyonywa katika mfumo huu uliodumu mpaka sasa. hapa nazungumzia mkulima ambaye Wasira kamtangazia kwamba Serikali ya CCM haiwezi kumpigania, ila inaweza kufidia makampuni yanapopata hasara kutokana na kuyumba kwa bei ya Pamba katika soko la dunia, nazungumzia mfanyakazi anayenyonywa kwa kukatwa kodi kubwa ya PAYE wakati makampuni makubwa yanakwepa kodi, na hata ule wigo wa kodi ni finyu mno kiasi kwamba ni wachache tu wameachiwa mzigo wa kulipa kodi. nazungumzia vijana ambao wamesahaulika kabisa. unachosema ni kweli kwamba CHADEMA bila kujizatiti haiwezi kufanikisha azma ya ukombozi wa mtanzania - lakini ninachosema ni kwamba hao watanzania wasikae tu kusubiri mechi kati ya CHADEMA na CCM, bali wao wenyewe waingie uwanjani na wapiganie kile wanachokiamini kwamba ni haki yao. ni wajibu wa CHADEMa kuendelea kutoa elimu na uhamasishaji, lakini ni wajibu wetu sisi sote kuitikia na kila mtu kwa nafasi yake kufanya kitu, hata kama ni kuanza kwa kupiga kelele za kutoridhishwa na hali ilivyo, na tusiishie kupiga kelele tu.
   
 3. M

  MIRIJA IKATWE Senior Member

  #3
  Sep 17, 2012
  Joined: Oct 21, 2011
  Messages: 136
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mshikamano na uadilifu ndiyo kitakacho waondoa hawa magamba madarakani
   
 4. Chenge

  Chenge JF-Expert Member

  #4
  Sep 17, 2012
  Joined: Oct 5, 2011
  Messages: 1,077
  Likes Received: 39
  Trophy Points: 145
  mkuu mikakati ya CDM hii hapa

  [​IMG]
   
 5. N

  NYAMKANG'ILI JF-Expert Member

  #5
  Sep 17, 2012
  Joined: Apr 1, 2012
  Messages: 223
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  MIRIJA, mwana jamvi hoja yake haiko kwenye MBINU za kutumia kuing'oa CCM, bali nguzo ambazo utawala wa CCM umejengwa ambazo ndizo za kuvunja la sivyo hakuna kitu. Je, unakubaliana nami kuwa hizo ndizo nguzo za utawala wa CCM au kuna nyingine? Na hizo nyingine ni zipi? Hii ndo hoja ...
   
 6. N

  NYAMKANG'ILI JF-Expert Member

  #6
  Sep 17, 2012
  Joined: Apr 1, 2012
  Messages: 223
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Hoja si mikakati, soma kwa makin hoja: hoja ni nguzo zipi za utawala huu ambazo zinapaswa kuvunjwa, bila ya kujua hizo nguzo basi adai atashambuliwa KIVULI chake badala ya kichwa ...
   
Loading...