Eliphaz the Temanite
JF-Expert Member
- Jan 19, 2010
- 3,018
- 1,149
Miezi michache iliyopita nilitaka mkopo kwenye kitaasisi hiki ambacho kiko sinza kijiweni karibu na Delux, maelezo niliyotoa mwanzo na aina yangu ya biashara yalitosha kabisa kuni disqualify kuendelea na mchakato, besides licha ya kupendekeza kusitisha mchakato baada ya kusoma masharti yao bado Mkurugenzi wake bwana Shumbi alisisitiza niendelee na mchakato. Mchakato ule ulunigharimu pesa tasisilim kama ada ya mkopo, muda, fuel ⛽, ukiacha mbali wadhamini na picha na masharti mengi yasiyo na tija ONLY to be told si qualify licha ya kuweka dhamana ya gari langu lenye thamani ya zaidi ya ml 20 eti kwa sababu aina ya biashara yangu is not qualified to be loaned! Nikauliza what about maelezo yangu ya awali? What about my suggestion kusitisha mchakato?? They never answered me!! Rai yangu ni kwamba kuna watu wangapi wanatapeliwa kwa ujanja ujanja huu, unatoza fee kwa ajili ya kuevaluate zaidi ya elf 50 mwisho wa siku unaambiwa bodi imeamua hutopata mkopo?? Jamaa akifanya hivyo kwa watu 20 kwa mwezi ana zaidi ya mil 1.Niliwahi kumpigia simu huyo shumbi kumweleza my feeling hakupokea simu. Mimi nilidhani fee inalipwa pale ambapo mteja atatoa maelezo ya kuridhisha kwamba anakidhi masharti ya dhamana, vielelezo anavyo na wakaguzi wanapokuja wanakuja kuthibitisha kile alichoeleza mteja na kwamba kama atadanganya basi asipewe, au kama hana vielelezo basi asipate. Kwangu mimi ilikuwa tofauti dhamana nilikidhi, vielelezo vyote nilukuwa navyo, kama shida ni hii aina ya biashara ningeambiwa mapema licha ya kudhidhi masharti!!
Asomae na afaham
Asomae na afaham