marcoveratti
JF-Expert Member
- Sep 21, 2017
- 1,091
- 1,915
“Ujobless si kilema – ni hali ya mpito, lakini pia ni cheche ya mabadiliko.”
Katika kona za vijiwe vyetu vya kahawa, mitandao ya kijamii, na hata kwenye foleni za usafiri, sauti moja imeanza kusikika – sauti ya matumaini lakini pia yenye mzigo mzito wa ukweli. Sauti hii inaitwa CCMJless – Chama Cha Ma Jobless.
Ndiyo, nipo mbioni kuanzisha chama hiki kipya cha siasa. Sio chama cha kawaida, bali ni mwamko mpya wa kisera, kwa ajili ya kizazi kilichosahaulika: kizazi cha wasomi waliomaliza shule na kubaki na vyeti mifukoni na ndoto kichwani. Kizazi cha walioambiwa “elimu ni ufunguo wa maisha” lakini wakajikuta wamekuta milango yote unafunguka kwa fingerprint.
Sera Kuu ya CCMJless: "Ujobless si Kilema"
Hii ndiyo falsafa ya msingi. Tunatambua kuwa kukosa ajira si kosa. Ni hali, si hukumu. Katika hali hiyo ndipo tunaona fursa.
Siasa kwa sasa ndiyo “ajira isiyo na CV”. Huhitaji uzoefu, wala transcript ya GPA, bali kuwa mjanja, mwenye mdomo mrefu na ahadi tamu. Na sisi tuna sifa hizo.
Chama hiki kitakuwa jukwaa la wale walionyimwa majukwaa. Vijana waliotoka kusoma chuo kwa mikopo, wakarudi kijijini na degree za BSc in Engineering, lakini kazi zao zikiwa “winga”.
Tunasema hapana , kama siasa ndiyo biashara inayolipa, basi nasi tunahitaji tawi letu sokoni.
Kwa Nini CCMJless?
CCMJless ni kivuli cha kisiasa, lakini pia ni kioo cha jamii. Tunaiga, tunabeza, na kisha tunatengeneza nafasi yetu.
Kama wapo wanaoitwa Waheshimiwa kwa kula posho bungeni wakiwa kimya, sisi tunataka kuitwa Waheshimiwa.
Kama wao wanapitisha sheria, basi sisi tutapitisha mashairi, na ubunifu unaochoma.
Na kama wao wanavaa suti bungeni, sisi tutavaa T-shirt za maandiko: “Degree Bila Ajira – Piga Kura CCMJless!”
Kikundi cha Kwanza – Vijana Wasomi Waliopigwa Chenga
Hiki ndicho kikosi cha kwanza cha CCMJless – mabingwa wa kutuma maombi 1,000 bila response, wamiliki wa vyeti vilivyokaushwa kwenye kabati, na wale waliogeuzwa mema ya elimu kuwa mzigo wa kisaikolojia.
Tunajua, siasa yetu sasa ni michezo ya kuigiza – basi sisi tumeamua kuwa waigizaji bora zaidi.
Hitimisho: Cheka Lakini Tafakari
CCMJless ni zaidi ya jina. Ni harakati. Ni wimbo wa waliochoka kuhesabiwa kama mzigo, wakaamua kuhesabu wenyewe hatua zao. Ni njia ya kusema kuwa kama kazi haipo, basi tunatafuta mamlaka. Kama ajira haziji, basi tunaomba kura.
Kwa hiyo, kama wewe ni kijana mwenye ndoto nzito lakini mfuko mwepesi, mwenye elimu kubwa lakini heshima ndogo, karibu CCMJless – chama cha kesho, kinachozaliwa kwa kejeli lakini kina ujumbe mzito kuliko sera za bajeti.
Karibu kwenye siasa ya kahawa – CCMJless, siasa yenye ladha ya ukweli na uchungu.
---
Ukicheka, ujue tumekufikia. Ukitafakari, ujue sasa tumeanza kushinda.
# CCMJless2025
“Jobless but not Hopeless.”