Teknolojia ni Yetu sote
JF-Expert Member
- Apr 28, 2020
- 1,246
- 2,498
Katika Maendeleo ya Teknolojia Tanzania sasa tutaona Mabadiliko mbalimbali kwenye sekta hiyo ambayo baadhi ya nchi mbalimbali ulimwenguni zimepiga hatua kubwa kwenye uwekezaji wa kutumia Roboti katika shughuli mbalimbali.
Jana kwenye mkutano wa Ccm kulikua na Mambo mengi waliongelea kuhusu na chama chao lakini Kubwa zaidi ni kuhusu Roboti ambaye alitengenezwa maalum kwa ajili ya kuwapokea Wageni mbalimbali watakao wasili kwenye mkutano.
Ni mkutano maalum wa Ccm Taifa, lilikua kivutio kwa watu kutokana na kila mtu kutaka kupigana naye picha,
wasanii mbalimbali waliweza kusogea karibu yake na kupiga naye picha chakushangaza zaidi Roboti naye aliwachangamkia wageni.