CCM yazindua Roboti kwenye Mkutano wake Dodoma

CCM yazindua Roboti kwenye Mkutano wake Dodoma



Katika Maendeleo ya Teknolojia Tanzania sasa tutaona Mabadiliko mbalimbali kwenye sekta hiyo ambayo baadhi ya nchi mbalimbali ulimwenguni zimepiga hatua kubwa kwenye uwekezaji wa kutumia Roboti katika shughuli mbalimbali.


Jana kwenye mkutano wa Ccm kulikua na Mambo mengi waliongelea kuhusu na chama chao lakini Kubwa zaidi ni kuhusu Roboti ambaye alitengenezwa maalum kwa ajili ya kuwapokea Wageni mbalimbali watakao wasili kwenye mkutano.


Ni mkutano maalum wa Ccm Taifa, lilikua kivutio kwa watu kutokana na kila mtu kutaka kupigana naye picha,


wasanii mbalimbali waliweza kusogea karibu yake na kupiga naye picha chakushangaza zaidi Roboti naye aliwachangamkia wageni.
Anaitwa nani?
 
Wanasiasa bana, shida yetu Watanganyika siyo Roboti,,,
  • sambazeni maji mlioahidi kutoka Ziwa Nyanza,
  • sambazeni mashamba ya umwagiliaji,
  • tieni mkazo Kilimo cha Biashara kwa mazao kulingana na mazingira husika...
  • fufueni viwanda mlivyofilisi
 
hii nchi sina uhakika kama kuna chuo kikuu kinafundisha robotics. sasa huyu roboti anatofauti na yule wa zape?
 
Back
Top Bottom