yegella
JF-Expert Member
- Nov 18, 2010
- 3,113
- 1,102
Chama cha Mabwepande kimezidi kuumbuka safari hii ni kwenye mgomo wa wasafirishaji mkoani Kilimanjaro. Jisomee mwenyewe
Wana bodi asalaam aleykum
Tangu juzi Ijumaa Mji wa Msohi umekumbwa na kadhia ya Wasafirishaji kugoma kusafirisha abiria kati ya mji wa moshi na Arusha pamoja na sehemu zingine za mkoa wa Kilimanjaro.
Hali ni mbaya sana kwani abiria wanalazimika kupanda magari binafsi aina ya Noah. Na magari hayo kupambwa kwa maua kama vile wanaenda Msibani. kwani kuna vijana wamepangwa Njia ya panda Himo,Barabara ya Kibosho kwa ajili ya kupopoa mawe mabasi ambayo yanakaidi mgomo.
Pia nimejaribu kuongea na baadhi ya makundi ya vijana wapopoaji kuhusu theme ya mgomo wao. Cha kwanza kabisa waliniuliza itikadi yangu nikaawaambia mimi ni mwana CDM. Duh. Namshukuru mwenyezi mungu kwa kunijalia Mbio.
Nilichokugundua kuwa Umoja wa Vijana wa CCM wilaya ya Moshi na Mkoa wanachochea mgogoro huu ili kuchonganisha wananchi wa Moshi na Halmashuri ya Mji wa Moshi ambayo inaongozwa na Chadema. Kuna magari ambayo yanapeperusha bendera za CCM yanabeba abiria bila kikwazo chochote. aliyepo moshi aende barabara inayoenda TPC/Kahe atayaona vizuri tu.
Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana Mkoa wa Kilimanjaro Godliving Moshi. ambaye kimsingi ni mpiga debe wa magari ya Marangu/Holili chini ya mwavuli wa Akiboa ndiye aliyepanga vijana maeneo yote hayo yenye vurugu. Pia warusha mawe hao ni wale vijana wa CCM waliopiga wagonjwa Hospital ya KCMC mwaka 2010
NAOMBA KUWASILISHA