CCM yawaita watanzania ni VIBAKA?

CCM yawaita watanzania ni VIBAKA?

johnthebaptist

JF-Expert Member
Joined
May 27, 2014
Posts
104,319
Reaction score
183,522
Chama cha Mapinduzi kupitia gazeti lake la Uhuru toleo la leo 11/8/2015 kimesema umati wa watanzania waliomsindikiza Lowasa NEC kuchukua fomu jana ni vibaka.

CCM imedai vibaka hao waliokodiwa na ukawa walifanya uporaji wa mali katikati ya jiji. Ninachojiuliza je ccm ni wasemaji wa polisi? watanzania hawa wameikosea nini CCM kustahili kuitwa vibaka?

Mungu na azidi kutuhurumia!!
attachment.php

 

Attachments

  • uhuru1.jpeg
    uhuru1.jpeg
    43.5 KB · Views: 1,744
Washajiona wamebaki peke yao Jana wameumbuka saana...tutaambiwa mengi sana tusubiri
 
Hili gazeti ka Uhuru na lile la Mazalendo bado yanachapishwa? Vanguard papers !
 
Yani wakubwa wa ccm mnazidi kukiumiza chama kwa kuwaita watz bila kujal kama wa ccm-oil chafu,makapi,vibaka..haya bwana
 
Chama cha Mapinduzi kupitia gazeti lake la Uhuru toleo la leo 11/8/2015 kimesema umati wa watanzania waliomsindikiza Lowasa NEC kuchukua fomu jana ni vibaka. ccm imedai vibaka hao waliokodiwa na ukawa walifanya uporaji wa mali katikati ya jiji. Ninachojiuliza je ccm ni wasemaji wa polisi? watanzania hawa wameikosea nini CCM kustahili kuitwa vibaka? Mungu na azidi kutuhurumia!!

muda mfupi uhuru litaanza kutukana matusi kwenye habari zake .baadala ya kumnadi Magufuli linahangaika na EDO
 
ihi habari hata mimi nimeiona kwenye gazeti la uhuru,

kwa kweli imenishangaza sana, kweli ccm leo inawaita watanzania vibaka?

Kwa hiyo wale wanaokwenda kwenye mikutano ya ccm ndio sio vibaka? Amakweli hakuna ugonjwa mbaya kama ugonjwa wa kulewa madaraka,

chama cha mapinduzi kilitakiwa kijifunze kwa vyama tawala vilivyo ondolewa madarakani kwa kulewa madaraka,

hawa hawa leo wanao waita vibaka ndio hawa hawa walimpa jk kura zao kwa kulaghaiwa (maisha bora kwa kila mtanzania)

sasa tujiulize aliye sababisha kuzalisha vibaka ni nani???

Ama kweli sikio la kufa halina dawa na dawa yake vijana wote wa nchi ihi wataonyesha hasira zao kwenye sanduku la kura oct 25

na hasubui hasubui ccm bye bye ikajifunze nini maana ya uongozi nje ya serikali,
 
Habari hii hata mie nilitaka niruke nayo. Pamoja na Polisi kutoripoti tukio hata moja la kihalifu kutokana na utulivu wa aina yake ulioonyeshwa na idadi ile kubwa ya watu, bado CCM imeamua kuwatukana watu wa Dar kuwa ni vibaka.
Watu wa DSM mpo! Kama mnaitwa vibaka jee mtaipa adhabu gani CCM iliyowatusi?
Ni wazi kwamba kama mkusanyiko huu ni wa vibaka basi jiji la Dar litakuwa linaongoza dunia nzima kwa kuwa na vibaka wengi sana.
 
Dalili za mfa maji washajuwa mwisho wao umefika!!
 
Watakuwa wanajinanga wenyewe kwa serikali yao iliyokuwa madarakani kwa miaka 50+ na imeweza kuzaliksha vibaka na mafisadi. Shame!
 
Hawa wanatakiwa watolewe kabisa madarakani ili wawe upinzani kabisa.
 
Inaonekana Dar ina vijana vibaka na walevi walevi wengi sana nchini.
 
Chama cha Mapinduzi kupitia gazeti lake la Uhuru toleo la leo 11/8/2015 kimesema umati wa watanzania waliomsindikiza Lowasa NEC kuchukua fomu jana ni vibaka. ccm imedai vibaka hao waliokodiwa na ukawa walifanya uporaji wa mali katikati ya jiji. Ninachojiuliza je ccm ni wasemaji wa polisi? watanzania hawa wameikosea nini CCM kustahili kuitwa vibaka? Mungu na azidi kutuhurumia!!

Wamesahau yaliyompata aliyekuwa katibu wao makamba alikwenda TARIME akawambia vijana vibaka na jimbo likachukuliwa na vibaka hao!!
 
Wacha waendelee kujitoa ufahamu,hao wanaowaita vibaka watawahukumu oct 25.
 
Hizi kauli zitawacost saana! By the way hatukutarajia muongee mazuri juu ya mafuriko ila tulitegemea ukimya kama ishara ya kukubali matokeo sio matusi. Inawapa sheeda sana!
 
Walituahidi maisha bora Leo wanatuita vibaka dahh?! Kweli CCM wamesharidhika, hatuna cha kuwafanya zaidi ya kuwaadabisha kwa kura,UKAWA TUMAINI LETU
 
Back
Top Bottom