CCM yawageukia Chenge, mawaziri yawataka watoe ushirikiano kwa vyombo vya dola

Kichakoro

JF-Expert Member
Sep 10, 2008
2,557
2,000
Ningekuwa mimi CHENGE, kwanza ningejiuzulu nafasi zote za uongozi bungeni na kwenye chama kisha nabaki mwanachama wa ccm na mbunge.

Kisha namwendea mwenyekiti kwa ushauri je ajiondoe chamani? Kama mwenyekiti akisema ndio, amuulize je 2022 rais ajaye akimuuliza kuhusu nyumba zilizouzwa atakua na majibu?

Weka heshima Mtemi Chenge
 
msem

JF-Expert Member
Nov 7, 2015
1,810
2,000
Inatakiwa wakamatwe na kuwekwa ndani ndiyo waanze kuhojiwa kama inavyofanyikaga kwa watuhumiwa wengine
Hili ni muhimu kwa namna kama mbili hivi
mosi;wasje wakatoroka,pili kwa usalama wao,manake kwa tuhuma walizonazo naona kama wananchi wana hasira nao sana huko mtaani na pia kuna uwezekano mmoja wao ana ushahidi wa kuwaimplicate wengine wasiomo hao wasiomo wakaplan jambo baya kwa mtu kama huyo, mfano kama mimi kwa sasa sijatajwa na ninajua kuwa mtuhumiwa flani "x" iwapo atahojiwa itakuwa si salama kwangu naweza kushawishika kumdhuru ili asihojiwe,nadhani hawa jamaa kwa sasa ni watu muhimu sana kwa hiyo wanastahili ulinzi mkali,kwa kuwa ni ngumu kuwapa ulinzi mkali mmoja mmoja huku kila mtu yuko kwake wangewekwa sehem moja tulivu na salama (behind the bars and walls) ili wawe salama.
 
Bowie

JF-Expert Member
Sep 17, 2016
4,231
2,000
Hayo ndio yanayotakiwa l think Nguo za kijani haitakuwa chaka la mafisadi.
 
Ngangari

Member
Sep 6, 2013
43
125
Hili ni muhimu kwa namna kama mbili hivi
mosi;wasje wakatoroka,pili kwa usalama wao,manake kwa tuhuma walizonazo naona kama wananchi wana hasira nao sana huko mtaani na pia kuna uwezekano mmoja wao ana ushahidi wa kuwaimplicate wengine wasiomo hao wasiomo wakaplan jambo baya kwa mtu kama huyo, mfano kama mimi kwa sasa sijatajwa na ninajua kuwa mtuhumiwa flani "x" iwapo atahojiwa itakuwa si salama kwangu naweza kushawishika kumdhuru ili asihojiwe,nadhani hawa jamaa kwa sasa ni watu muhimu sana kwa hiyo wanastahili ulinzi mkali,kwa kuwa ni ngumu kuwapa ulinzi mkali mmoja mmoja huku kila mtu yuko kwake wangewekwa sehem moja tulivu na salama (behind the bars and walls) ili wawe salama.
Mawazo mfu. Mnacheza na maisha ya watu ninyi, Mungu anawaona. Uwaweke ndani kwa kosa lipi hasa? JPM ameonyesha njia, wengi waliohusika hawajatajwa. Huwezi kuangamiza mchwa bila kushughulika na malkia. Kazi nzuri hii ya JPM itaharibika kwa kubangaika na chenge, tukomae na barrick ndio kwenye manufaa.
 
kabombe

JF-Expert Member
Feb 11, 2011
26,064
2,000
Inatakiwa wakamatwe na kuwekwa ndani ndiyo waanze kuhojiwa kama inavyofanyikaga kwa watuhumiwa wengine
hiyo ndio maana yake,ukiitwa uende na wadhamini kabisa.
Hata kwa kina Mramba na Yona ilianza hivi kuhojiwa lete hiki,lete kile mwisho bang!
 
wasumu

JF-Expert Member
Oct 28, 2015
2,008
2,000

Wako wa kunikamata ila wakunifunga Hakuna.

Nanukuu :
Nilitia sahihi kweli kama ripoti inavyodai ila kwa maagizo ya boss wangu sasa tatizo liko wapi kwangu?

Aliyetuagiza sisi kutia sahihi ndiye boss huyo huyo aliyemwagiza yeye kuuza nyumba za umma na kama ni kesi zinafanana.

Am not a stupid to sign agreement without a security.

✍✍✍

Shikamoo Mzee Chenge

Mingoi

JF-Expert Member
Jul 21, 2012
11,615
2,000
CCM hawana kabisa msamiati wa samaki mkunje angali mbichi, leo wanapomuomba Chenge atoe ushirikiano tayari ameshabobea katika masuala ya kupindisha
 
Scale

JF-Expert Member
Apr 6, 2014
1,877
2,000
Chenge ni chuma cha reli! Mnasemaga hivyo hata akitaka uspika mtasema Ndiyoooooo! Huyu ana akili kuwazidi wote CCM! Atahojiwa na kuachwa alivyo! Subirini!
 
minyoo

JF-Expert Member
May 25, 2013
21,527
2,000
Dar es Salaam. Chama Cha Mapinduzi (CCM), kimewataka wote waliotajwa katika ripoti ya kamati ya pili iliyochunguza makontena 277 ya mchanga wa madini, kutoa ushirikiano kwa vyombo vya dola vitakavyowahoji.

View attachment 524440

Waliotajwa katika ripoti ya pili ni aliyewahi kuwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG), Andrew Chenge, waliokuwa mawaziri wa Nishati na Madini, William Ngeleja, Profesa Sospeter Muhongo na na Nazir Karamagi.

Akizungumza na wanahabari leo (Alhamisi) katika ofisi za Lumumba, Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Humphrey Polepole amesema ili vyombo vya dola viweze kufanya kazi yake kwa haraka na ufanisi, waliotajwa wanapaswa kutoa ushirikiano.

Polepole amesema chama hicho chenye Serikali kinaviagiza vyombo vya dola kuwahoji waliohusika kwa haraka ili Watanzania wajue ukweli wa yaliyotokea.

Amempongeza Rais John Magufuli kwa kuthubutu kudai rasilimali ambazo zimekuwa zikiibiwa.

Pia, amewataka wananchi kumuunga mkono Rais Magufuli kwa kazi anayoifanya badala ya kugawanyika.

Chanzo: Mwananchi
Amri zote zilitolewa na Mkapa na kikwete iweje waandamwe ambao walipokea Amri zao, kama wanataka kuendelea kuwahukumu watu kienyeji wajiandae kukabili hali zote
 
minyoo

JF-Expert Member
May 25, 2013
21,527
2,000
Hili ni muhimu kwa namna kama mbili hivi
mosi;wasje wakatoroka,pili kwa usalama wao,manake kwa tuhuma walizonazo naona kama wananchi wana hasira nao sana huko mtaani na pia kuna uwezekano mmoja wao ana ushahidi wa kuwaimplicate wengine wasiomo hao wasiomo wakaplan jambo baya kwa mtu kama huyo, mfano kama mimi kwa sasa sijatajwa na ninajua kuwa mtuhumiwa flani "x" iwapo atahojiwa itakuwa si salama kwangu naweza kushawishika kumdhuru ili asihojiwe,nadhani hawa jamaa kwa sasa ni watu muhimu sana kwa hiyo wanastahili ulinzi mkali,kwa kuwa ni ngumu kuwapa ulinzi mkali mmoja mmoja huku kila mtu yuko kwake wangewekwa sehem moja tulivu na salama (behind the bars and walls) ili wawe salama.
Ulinzi gani wapewe? Kwani mtu akiamua kuwaua ulinzi hauwezi kuzuia mauaji yao kule kibiti polisi waliuawa wakiwa na bunduki zao hata kule Uganda msemaji wa Polisi aliuawa na walinzi wake , cha Msingi ni kuwahoji Mkapa na kikwete pekee kwani wao ndiyo walikuwa wakitoa Amri wanapokea na kutekeleza.
 
Kingdavi.ii

JF-Expert Member
Jul 29, 2015
1,180
2,000
Chenge ni chuma cha reli! Mnasemaga hivyo hata akitaka uspika mtasema Ndiyoooooo! Huyu ana akili kuwazidi wote CCM! Atahojiwa na kuachwa alivyo! Subirini!
Hakuna wa kumhoji may be wafanye maigizo , mbona kamati ya maadili aliigomea kuwa haina mamlaka na ika-surender (kuhusu escrow)
Na serkali gaina uwezo wa kwenda mahakamani kwani ni marufuku kuwataja au kuwagusa wahusika wakuu ambao wana kinga na ndiyo maana gazeti la mawio limefungiwa kwa kuugusa mzizi wa tatizo.
 
finyango

JF-Expert Member
Aug 11, 2016
2,026
2,000
waende tu maana majibu watakayojibu ni rahisi
wote watajibu walitekeleza maamuzi ya mabosi wao
wakienda kwa mabosi wameshaambiwa wasiguswe waachwe walale usingizi na biashara inaishia hapo hapo
Sio biashara,ni hadithi ndipo inapoishia
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom