CCM yaunga mkono Maridhiano ya kisiasa

CCM yaunga mkono Maridhiano ya kisiasa

.. Hii style alikuwa anaitumia zaidi JK. Iko hivi wameona hakuna haja ya kuangaika na watu wasio na madhara,sana sana ni kuleta attention kwa wafadhili wazungu bila sababu ya msingi. Hii style ilitumika sana kipindi cha JK. Na watakaofaidi hayo mnayoyaita maridhiano ni Mbowe na waliomzunguka.. FULL STOP. Ila mwananchi wa Tandahimba na Nyangulukulu mfuasi wa CHADEMA hayatamuhusu hata kidogo. Ukitaka kuamini hilo,hata akina Mdee watakaa bungeni hadi 2025 na story ya katiba mpya ndo imefika mwisho. Hakuna mkate mgumu mbele ya chai, ila mwisho wa movie watakaoathirika kisaikolojia ni wafuasi wa vyama wanaochukulia siasa kama ushabiki wa Simba na Yanga.
Jiwe hakuwa na hii akili?
 
Hata CUF walishawahi kuwa kwenye maridhiano bila kusahau ACT wazalendo . Daima CCM ataendelea kuwa mtawala
 
Chama cha Mapinduzi (CCM) , kimetangaza kuunga Mkono Mazungumzo yanayoendelea kati ya Mwenyekiti wao na viongozi wa Chadema , yenye lengo la kuleta usawa wa KIDEMOKRASIA na HAKI , kwa MASLAHI MAPANA YA TAIFA.

Kauli hii nzuri imetangazwa hadharani na Shaka Hamdu Shaka , ambaye ni Katibu wa Uenezi na Itikadi wa Chama hicho , alipoongea na Waandishi wa Habari .
Ni jambo jema sana. Na sisi wapenda Haki amani na maendeleo tunasubiri utekelezaji wa vitendo
 
Hivi yule Bia yetu aliondoka na korona, nini? Au alizikwa na mfalme Zumeradi kandokando ya ziwa Nyanza? Baada ya Mahera kumtangaza yule mkuu wa malaika wa shetani kuwa kashinda uchaguzi, akapotea JF!! Ama anasubiri uchaguzi 2025 ndio aanze tena propaganda za CCM. CCM inawatumia kama mipira. Uchaguzi ukishaa wanatupwa!

View attachment 2236038
Hawa wote sahizi wako na ID mpya wana majonzi na fedheha
 
Kuweni makini... ccm na wanachama wake akina Paskali hawaridhishwi na kinachoendelea!
Wana CCM walio wengi, hofu yao iko kwenye kupoteza fursa 2025, walizozipata kutokana na uchafuzi wa 2020. Demokrasia ikitamalaki, ni wazi wengi watapoteza matonge..... Hakutakua na haja ya kuwatengeneza Covid 19, wabunge wa upinzani watakuwepo.
 
Hivi yule Bia yetu aliondoka na korona, nini? Au alizikwa na mfalme Zumeradi kandokando ya ziwa Nyanza? Baada ya Mahera kumtangaza yule mkuu wa malaika wa shetani kuwa kashinda uchaguzi, akapotea JF!! Ama anasubiri uchaguzi 2025 ndio aanze tena propaganda za CCM. CCM inawatumia kama mipira. Uchaguzi ukishaa wanatupwa!

View attachment 2236038
Last seen date ya Bia yetu ni 28/10/2020..
Inasemekana hii ilikuwa I'd ya jiwe!
 
Walivyo wapuuzi MaCHADEMA yanaomba maridhiano wakati yenyewe yanadhulumu wanawake. Yafanye maridhiano pia
Wanadhulumu wanawake?!!!
Kwani huyu Kibamia ni CDM au ccm?
 
.. Hii style alikuwa anaitumia zaidi JK. Iko hivi wameona hakuna haja ya kuangaika na watu wasio na madhara,sana sana ni kuleta attention kwa wafadhili wazungu bila sababu ya msingi. Hii style ilitumika sana kipindi cha JK. Na watakaofaidi hayo mnayoyaita maridhiano ni Mbowe na waliomzunguka.. FULL STOP. Ila mwananchi wa Tandahimba na Nyangulukulu mfuasi wa CHADEMA hayatamuhusu hata kidogo. Ukitaka kuamini hilo,hata akina Mdee watakaa bungeni hadi 2025 na story ya katiba mpya ndo imefika mwisho. Hakuna mkate mgumu mbele ya chai, ila mwisho wa movie watakaoathirika kisaikolojia ni wafuasi wa vyama wanaochukulia siasa kama ushabiki wa Simba na Yanga.
Hizi shule za siku hizi sijui walimu wanafundisha nini....
 
Dr. Charles Mahera hastahili kuendelea kuwepo ofisi ya tume ya taifa ya uchaguzi. Huyu alichangia sana uchafuzi wa 2020 na upelekaji wa Covid 19 bungeni.
Natabiri Mahera atafungwa
 
Sasa CCM inaongizwa na wenye akili.

Wote, sasa tunapata uhakika kuwa kichaa mmoja ana uwezo wa kuharibu kila kitu, kama ilivyo mwenye hekima mmoja anaweza kuleta amani mioyoni mwa watu.

Angalia, mtu mmoja tu, Magufuli, alivyoweza kuvuriga na kuharibu nchi, kiasi cha kuiona CCM kuwa chama cha kishetani, kumve shetani alikuwa mmoja tu!!
 
Back
Top Bottom