CCM yatoa tamko juu ya mauaji ya Daudi Mwangosi

Sualla la sensa lisichukuliwe kisingizio cha kuidumaza CHADEMA. Kwani sensa imekamilika nchi nzima isipokuwa mkoa wa Iringa?
 
Issue hapa si scuffels btn police and the people,issue hapa ni "was the excess force" justifiable?

Hata kama mwananchi alimtukana polisi,ama hata kama mwananchi hakutii amri ya polisi,hiyo siyo issue kwenye utawala wa demokrasia,issue ni je bomu la machozi kuelekezwa tumboni kwa ukaribu kabisa na kwa kukusudia,ni justifiable?Nyingine zote blah blah tu.

Issue siyo kwamba amri ya rais,IGP ama mkuu wa kituo na hata RPC kwamba hazikufuatwa na wananchi,issue hapa ni je askari walikuwa trained kuuwa raia asiye na silaha?Askari wana mamlaka ya kuuwa hata kama maisha yao hayako hatarini?

Issue hapa siyo kuvunja sheria za nchi,maana hata kama that was the case,basi mahakama zipo,issue hapa ni je polisi wana mamlaka ya kujichukulia sheria mkononi na kuuwa raia asiyekuwa na silaha ama raia ambaye walikuwa tayari wameshamkamata na yuko chini ya ulinzi wao?

Jibu ni hapana,kwahiyo msiwasikilize kina Nape,what we want here is for justice to prevail.Period!
 
Kumbe waliambiwa wasitishe mikutano yao mpaka sensa iishe?

Wanaleta fujo na machafuko halafu wanakuja humu JF kujidai wameonewa? hawa wana matatizo makubwa sana na wakiendelea kuachwa wataitumbukiza shimoni hii nchi, wadhibitiwe mapema sana, hatua nzuri ni kukifuta tu hiki chama.

Pambanua fumbo sababu inayotolewa kwa CDM wasishughulike ni sensa wakati kule Zanziba Buibui kulikuwa na mkutano wa CCM. Sensa inaendelea mkoa wa Iringa tu? CCM ndiyo iliyoitumbukiza nchi shimoni kwa uongo wao na unafiki.

Nchi iko shimoni tayari kwa ufedhuli, ulaghai, ufisadi na rushwa kwa CCM kuvikumbatia. Matokeo yake ni umaskini, ujinga na mateso ya kila rangi kwa wannchi ijapokuwa Tanzania ni kati ya nchi chache duniani zenye utajiri wa maliasili wakupindukia unaonufaisha watawala wachache. Labda wewe ni mmoja wanaofaidi. CHADEMA WANAONEWA NDIYO HATA KWA MTOTO MDOGO HILI LIKO WAZI.
 
Kwa majibu haya sidhani kama Nape bado hajaomba msamaha. Wakina Mwangosi, Mwakalobo, Mwanjuni, Mwakasege, Mwabukusi, Mwakisole, Mwakambonja,Mwangulubhe, Mwasalemba, Mwaigomole, Mwakalwasya,Mwaipaja, Mwasandende, Mwanjuni....... bila kushau...... Mwanyingili, Mwankusye, Mwakibhopile, Mwakibete, Mwambene, Mwakalikamo, Mwasanyamba, Mwalubhwele, Mwakalinga, Mwakipesile, MwakafwilaMwandabwila, Mwakamboja, Mwangupili, Mwakalonge,Mwandosya, Mwakyembe, Mwandemele, Mwalukunga, Mwakalwasya, Mwakamele, Mwansasu, Na wengine wengi kwa ujumla wao wanakushushia sehemu ya raana ya muuaji isipokuwa ukiomba msamaha haraka iwezekanavyo....@ NAPE
 
Nape acha unafiki ,mauji mpange nyie awajibike mwingine. Lazima utakua na mtindio wa ubongo.
 
Kwa maelezo hayo,nimeamini kuwa mauwaji yanayotokea kwenye mikutano ya CDM yanafanywa na polisi kwa maelekezo ya CCM ili CDM ionekane ni chama cha kusababisha vifo ya watanzania kwenye mikutano yao(CCM ikiamini kuwa ndiyo njia ya kukidhoofisha CDM)...............Kwa hili,CCM nadhani mmepotea njia.CCM nawashauri mtafute strategy nyingine.
Inanitia hasira sana kwa mtu mwenye nafai kama ya Nape ndani ya CCM kuwa na maelezo kama haya............
Viongozi wa aina hii ya Nape ndio wanaoiua CCM,lakini kwa upande mwingine ndio wanaoimarisha CDM kwa kutoa hoja zisizo na mashiko mbele ya umma ya watanzania
 
Laiti Chama hicho kingesubiri siku chache zilizobakia kabla ya Sensa kuisha kabla ya kuendelea na mikutano yake ni dhahiri mauaji haya yasingetokea. Lakini kauli za kukebehi na uamuzi wa kukaidi amri ya Jeshi la Polisi na kusema "tupo tayari kwa lolote" ni ishara kwamba Chama hiki kiliandaa na kujiandaa na fujo zilizotokea.

Huu ni unafiki mbona kule Zanzibar Buibui CCM ilikuwa na mkutano na tamasha la Fiesta liliendelea kule Mwanza wakati huo huo CDM ikiwa katika shughuli za kichama wala si mkutano wa M4C? HUU UNDUMILAKUWILI UFE haraka sana. Shame on you Kijana tarumbeta la magamba.

Mojawapo ya Mambo yaliyoniuma ni hili la NYINYIEM Kufanya Mkutano kule zanzibar kufungua kampeni huku Bilali akihutubia..Huko sijasikia Polisi wakizuia mkutano..sembuse kuua hata Inzi..Lakini CHADEMA Ikifanya kitu tu Inakuwa Nongwa.NASEMA HUU NI UONEVUUU..IMENIUMA SANA JINSI SERIKALI YA CCM INAVYOCHEZA RAFU ZA AINA HII..MUNGU IBARIKI CHADEMA..MUNGU MBARIKI NA MLIPIE NDUGU DAUDI MWANGOSI
 
nape siamini kama ni wewe unakuwa na akili mgando kiasi hiki?nakuheshimu sana,ila wakati mwingine nakuona chenga kutokana na matamshi yako,pengine kazi yako hapo lumumba ni propaganda kiasi unajisahau,pole sana ndugu yangu unatudhalilisha.....Mchezo ulioubuni ni hatari sana kwa usalama wa wa nchi yetu,mnatengeneza visasi......sensa kwa chadema tu?mbona makamu wa rais kazindua kampeni ya mgombea huko zanzibar?sheria hipi ina ubaguzi ambayo ameitumia mw bilali na chadema aiwezekani!!!!,kwani zanziba sio tanzania?
 
Ningeshangaa Nape kuendelea na ukimya baada ya mauaji waliyopanga kutimia. Nitamshangaa Kikwete akikaa kimya baada ya mkakati wao kutimia. Jamani nionacho mimi kila ccm wanachofanya kinachangia kubainisha uozo wao. Wanajitahidi sana kutaka kutuonyesha ubaya wa wasio wabaya, lakini bahati mbaya wanakwama kwenye kila kitu! Maskini Nape, maskini ccm...sasa watz hatudanganyiki. Kanunueni silaha zaidi mje muue zaidi, lakini kila tone la damu inayomwagika linaashira ukombozi na ukombozi u-mlangoni sasa. Hamjajua tu?
 
Kwa kifupi kabisa, taarifa hii ya "Nape", imedhihirisha wazi uwezo finyu alionao katika kutathmini matukio, na badala yake ameonyesha dhahiri kwamba yeye ni mtu asiyekuwa tayari kuukabili ukweli hata pale makosa yao yanapokuwa wazi!

Hapa serekali na watendaji wake wameharibu, wawajibishwe!

Nashangaa RPC wa Iringa bado yupo anakula bata, si ni huyu huyu aliyehusika kule Songea, au siye Kamhanda?

Wasitafute wachawi, wamekoroga wenyewe, Dr. Slaa wa nini?
 
Wakati mwingine huwa najisikia kichefuchefu ninaposikia baadhi ya watu wa aina ya nepi wakitoa matamko. Ptuuuu!
 
Iringa
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI.

Itakumbukwa tarehe 02/09/2012 katika operesheni za Chama cha Demokrasia na Maendeleo(CHADEMA) mkoani Iringa kulitokea vurugu zilizosababisha kuuawa kwa mwanahabari mzoefu Ndg. Daudi Mwangosi na kujeruhiwa vibaya kwa *askari watatu wa kuzuia fujo.

Chama Cha Mapinduzi kimepokea kwa masikitiko makubwa sana taarifa za kifo hicho na kujeruhiwa kwa askari hao. CCM inachukua nafasi hii kutoa pole kwa wafiwa, wanahabari nchini na wote walioguswa na msiba huu kwa namna moja au nyingine.*

Tunatoa wito kwa vyombo na tume mbalimbali zilizoundwa kuchunguza swala hili, vichunguze kwa umakini na weledi mkubwa ili kubaini yote - ikiwemo chanzo cha vurugu zilizotokea na mazingira ya kifo cha ndugu yetu Daudi Mwangosi.*

Pamoja na wito wetu wa kuchunguzwa suala hili kwa umakini na weledi mkubwa, pia tunatoa rai kwamba uchunguzi huu ufanyike kwa kutumia muda mfupi ili ukweli uweze kubainika mapema na hatua zinazostahili ziweze kuchukuliwa haraka iwezekanavyo.

Vilevile CCM inasikitishwa sana na mfululizo wa matukio ya watu kupoteza maisha au kujeruhiwa katika mikutano na operesheni mbalimbali zinazoendeshwa na CHADEMA nchini hasa zile zilizofanyika kwa kukaidi amri halali za vyombo vya ulinzi na usalama. *

Kutaja matukio baadhi tu ni pamoja na lile la kuuwawa kwa kada wa CCM Mkoani Singida, kuuawa kwa Ndg. Ally Hassan mjini Morogoro, kuuawa kwa Ndg. Daudi Mwangosi Mjini Iringa hivi majuzi,kujeruhiwa kwa askari polisi Iringa na matukio mengine mengi ambayo yametokea wakati wenzetu wa CHADEMA wakiendesha operesheni zao mbalimbali nchini.

Matukio haya si mazuri kutokea kwenye shughuli za Chama cha siasa. Kwakweli ni aibu, inayohitaji uwajibikaji,hata kama ni wa kisiasa. Inapotokea shughuli za chama chako zinasababisha kupotea kwa maisha ya watu kila unapozifanya na bado usitake kuwajibika, inahitaji roho ngumu na ujasiri wa aina yake.

Inakuwa mbaya zaidi pale vifo hivi vinaposababishwa na Chama hicho kutotii amri halali zilizotolewa kwa mujibu wa sheria na katiba ya nchi inayovipa pia uhalali *vyama vya siasa kuwepo na kuendesha shughuli zake kwa mujibu wa sheria.*

Laiti Chama hicho kingesubiri siku chache zilizobakia kabla ya Sensa kuisha kabla ya kuendelea na mikutano yake ni dhahiri mauaji haya yasingetokea. Lakini kauli za kukebehi na uamuzi wa kukaidi amri ya Jeshi la Polisi na kusema "tupo tayari kwa lolote" ni ishara kwamba Chama hiki kiliandaa na kujiandaa na fujo zilizotokea.

Tunatoa wito kwa vyama vya siasa na wanasiasa kwa ujumla kujenga utamaduni wa kuheshimu utawala wa sheria. Amani na utulivu vulivyopo nchini ni kazi nzuri iliyojengwa kwa muda mrefu na waasisi wetu kwa kujenga utamaduni wa kuzingatia utawala wa sheria.

Imetolewa na;
Nape Moses Nnauye
Chama Cha Mapinduzi
Katibu wa NEC-Itikadi na Uenezi Taifa.

Kwani kuna mikutano au maandamano yoyote yaliyofanywa na CHADEMA au kundi lolote yaliyopelekea majaruhi au mauaji bila polosi wa serikali kuhusika? siku zote wanaoua kwenye matukio hayo ni polisi, fullstop!!!
 
kazi ya polisi ni kulinda raia na mali zake na si kuua raia kama wafanyavyo na kusingizia CDM hili hata mtoto mdogo humdanganyi kwa yanayotokea na mwenye akili timamu kulijua ilo
 
Iringa
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI.

Itakumbukwa tarehe 02/09/2012 katika operesheni za Chama cha Demokrasia na Maendeleo(CHADEMA) mkoani Iringa kulitokea vurugu zilizosababisha kuuawa kwa mwanahabari mzoefu Ndg. Daudi Mwangosi na kujeruhiwa vibaya kwa *askari watatu wa kuzuia fujo.

Chama Cha Mapinduzi kimepokea kwa masikitiko makubwa sana taarifa za kifo hicho na kujeruhiwa kwa askari hao. CCM inachukua nafasi hii kutoa pole kwa wafiwa, wanahabari nchini na wote walioguswa na msiba huu kwa namna moja au nyingine.*

Tunatoa wito kwa vyombo na tume mbalimbali zilizoundwa kuchunguza swala hili, vichunguze kwa umakini na weledi mkubwa ili kubaini yote - ikiwemo chanzo cha vurugu zilizotokea na mazingira ya kifo cha ndugu yetu Daudi Mwangosi.*

Pamoja na wito wetu wa kuchunguzwa suala hili kwa umakini na weledi mkubwa, pia tunatoa rai kwamba uchunguzi huu ufanyike kwa kutumia muda mfupi ili ukweli uweze kubainika mapema na hatua zinazostahili ziweze kuchukuliwa haraka iwezekanavyo.

Vilevile CCM inasikitishwa sana na mfululizo wa matukio ya watu kupoteza maisha au kujeruhiwa katika mikutano na operesheni mbalimbali zinazoendeshwa na CHADEMA nchini hasa zile zilizofanyika kwa kukaidi amri halali za vyombo vya ulinzi na usalama. *

Kutaja matukio baadhi tu ni pamoja na lile la kuuwawa kwa kada wa CCM Mkoani Singida, kuuawa kwa Ndg. Ally Hassan mjini Morogoro, kuuawa kwa Ndg. Daudi Mwangosi Mjini Iringa hivi majuzi,kujeruhiwa kwa askari polisi Iringa na matukio mengine mengi ambayo yametokea wakati wenzetu wa CHADEMA wakiendesha operesheni zao mbalimbali nchini.

Matukio haya si mazuri kutokea kwenye shughuli za Chama cha siasa. *********Kwakweli ni aibu, inayohitaji uwajibikaji,hata kama ni wa kisiasa. Inapotokea shughuli za chama chako zinasababisha kupotea kwa maisha ya watu kila unapozifanya na bado usitake kuwajibika, inahitaji roho ngumu na ujasiri wa aina yake.***************

Inakuwa mbaya zaidi pale vifo hivi vinaposababishwa na Chama hicho kutotii amri halali zilizotolewa kwa mujibu wa sheria na katiba ya nchi inayovipa pia uhalali *vyama vya siasa kuwepo na kuendesha shughuli zake kwa mujibu wa sheria.*

Laiti Chama hicho kingesubiri siku chache zilizobakia kabla ya Sensa kuisha kabla ya kuendelea na mikutano yake ni dhahiri mauaji haya yasingetokea. Lakini kauli za kukebehi na uamuzi wa kukaidi amri ya Jeshi la Polisi na kusema "tupo tayari kwa lolote" ni ishara kwamba Chama hiki kiliandaa na kujiandaa na fujo zilizotokea.

Tunatoa wito kwa vyama vya siasa na wanasiasa kwa ujumla kujenga utamaduni wa kuheshimu utawala wa sheria. Amani na utulivu vulivyopo nchini ni kazi nzuri iliyojengwa kwa muda mrefu na waasisi wetu kwa kujenga utamaduni wa kuzingatia utawala wa sheria.

Imetolewa na;
Nape Moses Nnauye
Chama Cha Mapinduzi
Katibu wa NEC-Itikadi na Uenezi Taifa.

## ANGALIA *********

Semea basi na ile ya Mabwepande ya Dr. Ulimboka!
 
Tunatoa wito kwa vyama vya siasa na wanasiasa kwa ujumla kujenga utamaduni wa kuheshimu utawala wa sheria. Amani na utulivu vulivyopo nchini ni kazi nzuri iliyojengwa kwa muda mrefu na waasisi wetu kwa kujenga utamaduni wa kuzingatia utawala wa sheria.

Kuna misingi muhimu ya utawala wa sheria, kama hiyo misingi haifuatwi usitegemee asilani kuwa kutakuwa na utii wa sheria:

Usawa mbele ya sheria ni msingi mmoja muhimu kama chadema na CCm wanapewa treatment tofauti usitegemee anayeonewa atang'ang'ania utawala wa sheria.
 
Kumbe waliambiwa wasitishe mikutano yao mpaka sensa iishe?

Wanaleta fujo na machafuko halafu wanakuja humu JF kujidai wameonewa? hawa wana matatizo makubwa sana na wakiendelea kuachwa wataitumbukiza shimoni hii nchi, wadhibitiwe mapema sana, hatua nzuri ni kukifuta tu hiki chama.
Wale wabakaji wa demokrasia wa kijani na njano wao katazo halikuwahusu, mbona walijazana bububu wanazindua kampeni, hamuwezi kukwepa lawama, nyinyi ni wafamaji, mtalipa damu za watu mnaowaua.
 
Kumbe waliambiwa wasitishe mikutano yao mpaka sensa iishe?

Wanaleta fujo na machafuko halafu wanakuja humu JF kujidai wameonewa? hawa wana matatizo makubwa sana na wakiendelea kuachwa wataitumbukiza shimoni hii nchi, wadhibitiwe mapema sana, hatua nzuri ni kukifuta tu hiki chama.

ndicho unacho ota wewe na Nape! Mwambie Nape atoe maagizo kwa Tendwa
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom