CCM yatafuta kick Moshi

CCM yatafuta kick Moshi

Mkuu uliyosema kimsingi yana ukweli, lkn je ni hilo tu ulililo liona juu ya ccm?hujawahi kuona mambo mengi machafu zaidi ya hayo yanayo andikwa na wana ccm juu ya viongozi wa upinzani?tena
maneno machafu kabisa nashindwa hata kuyaandika hapa jukwaani hujayaona?nakama umesha yaona mbona hujawahi kukemea kama ulivyokemea hili?

Mimi huwa nakemea wote. Nakumbuka wako wana-CCM waliokuwa (wakati wa kampeni) wanamtukana Lowassa kwa matusi makubwa, kwa mfano, kuwa 'anaji....' mimi nilikuwa nawakemea humu JF. Kimsingi naichukulia JF kuwa ni sehemu ya kupashana habari na kuelimishana na siyo sehemu ya kuonyesha ujuzi wa matusi. Binafsi sipendi matusi. Kwa bahati mbaya wapo vijana wengi nchini mwetu wasiojua kabisa historia ya nchi hii. Wengi wamekulia katika Enzi hizi za mfumo wa vyama vingi vya siasa na wanadhani kuwa matusi ni sehemu ya demokrasia. Inasikitisha kweli kweli kuona kuwa wako ambao wanajaribu hata kumtukana 'Head of State'. Tena bahati mbaya ilioje kuona kuwa wanaoendesha matusi wamo wanasiasa wa pande zote mbili, CCM na upinzani, na wasijue kuwa tunajenga misingi mibovu ya kukosa uzalendo, heshima na busara kwa kizazi hiki na kwingineko. Yaani uhuru wa kutoa mawazo tulio nao nchini mwetu unachukuliwa kuwa ni tiketi ya kuwadhalilisha viongozi wetu na jamii yetu kwa ujumla. It is a shame... Ndiyo maana mimi nasema aje mtu afanye kosa na kuniambia uso kwa uso kuwa mimi ni shoga, nadhani huo ndio utakuwa ni mwisho wa chapter...
 
teh teh teh

pale stendi ya Moshi kuna vinywaji kinaitwa Ndizi kuku ..... yaani banana na kiroba jogoo
 
Kashfa za namna na aina hii ndizo ambazo hazitakiwi. ni maneno ambayo hupandikiza chuki katika jamii. Huna sababu ya kuandika kuwa CCM ni Chama Cha Mashoga. Huna sababu hiyo kabisa zaidi ya utoto na nadhani hata umri wako unaweza kuwa chini ya miaka 18. Nchi hii wako walioijenga kwa moyo wa dhati. Kama huipendi CCM huna sababu ya kuandika maneno ya ovyo. Tumia busara, hekima na ujasiri wa kukubali kuwa Tanzania inaendeshwa na mfumo wa vyama vingi vya siasa. Kuna watu wengi kwa mamilioni wanaipenda CCM. Kuna watu kwa mamilioni wanaipenda CHADEMA. Lakini wote ni watanzania na lengo lao ni moja la kuijenga nchi. Sasa ikitokea mwanaCCM akaandika kuwatukana CHADEMA kuwa ni chama cha wachaga huyo naye anapotoka. Na akatokea mtu kama wewe na ambaye nina hakika hajui historia ya nchi hii akatukana kuwa CCM ni chama cha mashoga kwa maana kuwa CCM wote ni mashoga sasa hilo nalo ni jambo la hatari kwa umoja na mshikamano wa nchio hii. Ungekuwa China umeandika maneno hayo kuwa Chama cha Kikomunisti cha China ni Chama cha mashoga saa hizi tayari ungekuwa umefuatwa na kesi yako kuamliwa kwa siku moja na kupigwa risasi. Vijana wengi mnautumia vibaya uhuru uliopo nchini mwetu wa kutoa mawazo. Ni uhuru huu ndio unaokufanya utembee na kujidai nchini. Uhuru huu ukipotea hutakuwa na nafasi ya kuandika upuuzi kama ulivyofanya.

1954;
Mkuu naona umeandika kwa uchungu kweli kumwonya huyu mtoto. Sawa kabisa, ila najua weye ni ccm dam dam, si mbaya nia haki yako. Ila ulipokosea ni kule kusema ati, huyu kijana (mtoto) hajui walio ijenga hii nchi.
Ama kweli, nyani haoni kundule. Inakuwaje mtu kama weye kuweza kutamka neno hilo? Weye ulizaliwa ccm?? CCM ndo babako na mamako?? Hakuna mwenye haki ya kusema ati ndo aliijenga nchi hii. Hayupo. Uliijenga nchi, ilikuwa imebomoka??
Kila mtu anahusika na Tanzania. Waliouomba uhuru hawapo tena, hata weye hukuijenga nchi. Waache watu wajisemee watakavyo kwani HAKUNA NAMNA TENA. iLIPOTUFIKISHA CCM TUNAPAJUA. Miye sina chama, ila naumia ninapoona watu wakijihesabia haki. Watu wenye mawazo ka yako wanajiona kuwa ndo wanajua hata saa ambayo mimi natakiwa kulala.
Nilidhani ungejikita kwenye mada. CCM wakiratibu maandamano hata kama ni ya kwenda Ikulu, intelijensia inaona usalama. Chama kingine chochote kikiratibu maandamano, hata kama ni kwenda Pugu mnada wa ng'ombe, intelijensia inaona kuwa ng'ombe wataanguka kifafa.
Haya, waacheni waandamane mpaka Stand kuu ya mabasi, kando tu ya kituo kikuu cha Polisi, ila polisi siku hiyo hawatakuwa na hofu yeyote bali watawapa hata brass band.
Mku hilo lichama lishajifilia lenyewe. JPM hana haja ya kuombewa Stand kuu ya mabasi. Kwanza pale ni usumbufu hata malaika anayepokea maombi hatasikia. Pale kuna dini sijui 7 zimeizunguka ile stend kama jografia yangu ya Moshi haijapotea sana. Sasa ni kiongozi wa dini gani mtakaye mlipa kitu kidogo. Kwaheri, ila usiache kutuletea mrejesho
 
Uhuru huu ukipotea...
Uhuru huo ni haki ya kikatiba au unatolewa kwa hisani? Waliomwita Lema shoga walikuwa kina nani kama si wana CCM? Huo mshikamano wa taifa unapotea kwa CCM kuitwa chama cha Mashoga ila CHADEMA wakiitwa chama cha Wakatoliki na wachaga ni sawa, au CUF wakiitwa chama cha Wapemba na waislam ndiyo amani inadumishwa?
 
Heshima mbele wadau.
Baada ya chama cha mapinduzi kufutika kabisa katika ramani ya kisiasa manispaa ya Moshi na mkoa wa Kilimanjaro kwa ujumla sasa wanajaribu kutafuta kiki ya kutokea kupitia mlango wa madhehebu ya dini.

Chama cha mapinduzi kimeandaa 'maombi' ya kumuombea Rais Magufuli jumamosi 20 Februari 2016 yatakayotanguliwa na maandamano yatakayoanzia katika ofisi za CCM mkoa na kuishia stendi kuu ya mabasi mjini Moshi ambako 'maombi' hayo yatafanyika!

Katibu wa CCM mkoa ndugu Ruta amesema maandamano na 'maombi' hayo hayana itikadi na kuwaomba wananchi wote washiriki lakini cha kushangaza shughuli zote zinaratibiwa na CCM na gari la CCM ndiyo linatangaza 'maombi' hayo!

Hata hivyo viongozi wa madhehebu yanayoheshimika mkoani Kilimanjaro kanisa katoliki,KKKT na Bakwata wamegoma kushiriki kwenye maombi hayo kwa madai kwamba hawashiriki shughuli za kisiasa na kuwa kama ni maombi kwa Rais wetu yanapaswa kuratibiwa na madhehebu ya dini yenyewe na kufanyika sehemu inayostahili na siyo stendi ya mabasi ambako kuna walevi na wahuni wa kila aina ambao wanaweza kupelekea uvunjifu wa amani na kudhalilishwa kwa viongozi wa dini.Kwa sababu hiyo 'maombi hayo yataendeshwa na madhehebu ya 'uchochoroni'

Wachambuzi wa masuala ya kisiasa mkoani hapa wanasema kitendo cha CCM kuandaa 'maombi' stendi kunatokana na hofu ya kukosa mahudhurio endapo yatafanyika sehemu rasmi,hii inatokana na CCM kutokukubalika kabisa mkoani Kilimanjaro. Pia wamemtaka Kamanda wa Polisi RPC kuzuia 'maombi ' hayo ili kuepusha kero kwa abiria badala yake wayahamishie kwenye viwanja vinavyotumika kwa mikutano ya kisiasa na kidini ambavyo viko vingi mjini Moshi.
kwani Magembe na mathayo was chama gani
 
Nijuavo ndugu zangu wa kaskazini hawana muda wa mikutano au maombi yasiyo na tija.wako bussy kutafuta pesa
 
Ujue kumbe mtu kumlk smartphone sio kua na akil timamu sasa lowasa washukuru nn watu wakat hajashnda au kwasababu n darasa huru bas kila mtu anaandka tu afu et ccm nchi nzima bas mngekua na wabunge weng ukawa achen utoto kuen na mawazo endelevuuuu
 
Back
Top Bottom