Malata Junior
JF-Expert Member
- Nov 29, 2011
- 3,104
- 2,549
Heshima mbele wadau.
Baada ya chama cha mapinduzi kufutika kabisa katika ramani ya kisiasa manispaa ya Moshi na mkoa wa Kilimanjaro kwa ujumla sasa wanajaribu kutafuta kiki ya kutokea kupitia mlango wa madhehebu ya dini.
Chama cha mapinduzi kimeandaa 'maombi' ya kumuombea Rais Magufuli jumamosi 20 Februari 2016 yatakayotanguliwa na maandamano yatakayoanzia katika ofisi za CCM mkoa na kuishia stendi kuu ya mabasi mjini Moshi ambako 'maombi' hayo yatafanyika!
Katibu wa CCM mkoa ndugu Ruta amesema maandamano na 'maombi' hayo hayana itikadi na kuwaomba wananchi wote washiriki lakini cha kushangaza shughuli zote zinaratibiwa na CCM na gari la CCM ndiyo linatangaza 'maombi' hayo!
Hata hivyo viongozi wa madhehebu yanayoheshimika mkoani Kilimanjaro kanisa katoliki,KKKT na Bakwata wamegoma kushiriki kwenye maombi hayo kwa madai kwamba hawashiriki shughuli za kisiasa na kuwa kama ni maombi kwa Rais wetu yanapaswa kuratibiwa na madhehebu ya dini yenyewe na kufanyika sehemu inayostahili na siyo stendi ya mabasi ambako kuna walevi na wahuni wa kila aina ambao wanaweza kupelekea uvunjifu wa amani na kudhalilishwa kwa viongozi wa dini.Kwa sababu hiyo 'maombi hayo yataendeshwa na madhehebu ya 'uchochoroni'
Wachambuzi wa masuala ya kisiasa mkoani hapa wanasema kitendo cha CCM kuandaa 'maombi' stendi kunatokana na hofu ya kukosa mahudhurio endapo yatafanyika sehemu rasmi,hii inatokana na CCM kutokukubalika kabisa mkoani Kilimanjaro. Pia wamemtaka Kamanda wa Polisi RPC kuzuia 'maombi ' hayo ili kuepusha kero kwa abiria badala yake wayahamishie kwenye viwanja vinavyotumika kwa mikutano ya kisiasa na kidini ambavyo viko vingi mjini Moshi.