CCM yashindwa vibaya

Asha Abdala

JF-Expert Member
Mar 21, 2007
1,130
44
CCM imeshindwa vibaya na CHADEMA katika uchaguzi wa udiwani wa kata ya machinjiano. Kwenye kata hiyo, CCM iliweka kambi kwa siku 30 na viongozi mbalimbali wa kitaifa wa chama hicho walikwenda kwenye kampeni kata kata hiyo kwa awamu mbalimbali.


CCM Kigoma waibuka na Operesheni Ndoano
Fadhili Abdallah, Kigoma
Daily News; Sunday,January 04, 2009 @00:03

Habari nyingine
JK: CCM Z'bar jiandaeni kwa ushindi mkubwa
Wachache wapiga kura Mbeya
Walinzi wanyongwa lindoni
Maofisa uhamiaji kufunzwa lugha
Shein ahimiza upendo, ushirikiano
Mkapa aichangia KKKT Iringa milioni 5/-
Kikwete amzika Mzee Waryuba
Msafara wa Shein wasimamishwa njiani
Operesheni ya kusafisha bandari Dar yaanza
Wilaya 11 zapatiwa fedha kununua chakula

Chama Cha Mapinduzi (CCM) mkoani Kigoma kimeanza kampeni za kuwania kiti cha udiwani cha kata ya Machinjioni katika manispaa ya Kigoma/Ujiji kwa kuibuka na mkakati maalumu wa ushindi unaojulikana kama Operesheni Ndoano.

Akitangaza mkakati huo katika mkutano huo wa uzinduzi wa kampeni Mwenyekiti wa CCM mkoa Kigoma, Azim Premji alisema kuwa mkakati wa operesheni hiyo ni kuwavua sangara wote na kuwapeleka mahali panapostahili.

Premji alisema pamoja na kuwavua sangara wote, lakini alisema kuwa mkakati huo una lengo la kuwaonyesha watu wote wanaopenda siasa kuwa CCM ndiyo mahala sahihi wanapoweza kwenda na kufanya harakati zao mbalimbali za kisiasa.

Mwenyekiti huyo wa CCM amewaomba wapiga kura katika kata hiyo kuchagua mgombea udiwani wa Chama Cha Mapinduzi ili iwe rahisi kushirikiana katika mkakati mzima wa kuleta maendeleo kwenye kata hiyo.

Naye Mbunge wa jimbo la Kigoma Mjini Peter Serukamba aliwataka wapigakura katika kata hiyo kumchagua mgombea wa CCM, kwani kwa kufanya hivyo itakuwa rahisi kwao kuongoza manispaa hiyo na kufikia malengo yao ya utekelezaji wa kuleta maendeleo kwa wananchi.

Serukamba alisema kabla ya kifo cha diwani huyo Manispaa ya Kigoma Ujiji ilikuwa na idadi sawa ya madiwani na jambo hilo kwao linakuwa gumu kama wana ajenda ya maendeleo ambayo wanataka kuipitisha.

Lakini alisema kama uchaguzi huo CCM itafanikiwa kunyakua kiti hicho itawawia rahisi kuongoza kwa sababu watakuwa na viti 11 dhidi ya viti tisa vya wapinzani wao wa Chadema.

Akijinadi kwa wapiga kura, mgombea wa kiti hicho kwa tiketi ya CCM, Salum Akilimali alisema anao uzoefu mkubwa katika uongozi na ndiyo maana chama kikampa dhamana ya kugombea, kutokana na hilo amewaomba wapiga kura wamchague ili akapeleke hoja zao za maendeleo katika manispaa.

Uchaguzi huo mdogo wa nafasi ya udiwani wa kata ya Machinjioni unafanyika kutokana na kifo cha diwani wa kata hiyo, Hamisi Bilantanye wa Chadema ambaye alikuwa diwani wa kata hiyo kwa miaka 13 mfululizo.

Kumekuwa na ushindani mkubwa baina ya CCM na Chadema katika kuwania kiti hicho na uchaguzi mdogo wa Tarime umekuwa darasa tosha kwa Chama Cha Mapinduzi kuhakikisha wanajipanga vizuri na kushinda kiti hicho
 
CCM imeshindwa vibaya na CHADEMA katika uchaguzi wa udiwani wa kata ya machinjiano. Kwenye kata hiyo, CCM iliweka kambi kwa siku 30 na viongozi mbalimbali wa kitaifa wa chama hicho walikwenda kwenye kampeni kata kata hiyo kwa awamu mbalimbali.


Dada Asha

Ni ukweli CHADEMA imeshinda, lakini imeshinda kwa asilimia ngapi? Walijitokeza wapiga kura wangapi?


PM
 
Hapo tumeshindwa kwa uzembe wa Azim Premji. Wakati ule Rajab Maranda yuko mzingoni hawa tungewasambaratisha kabisa.

....ndiyohiyo
 
Back
Top Bottom