Kurzweil
JF-Expert Member
- May 25, 2011
- 6,623
- 8,426
Diwani wa Kata ya Pemba Mnazi (CCM), Maabadi Hoja ameshinda umeya wa Halmashauri mpya ya Kigamboni baada ya kupata kura tisa dhidi ya tano za Celestine Maufi wa Chadema.
Uchaguzi huo umefanyika leo (Jumamosi )katika Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Julisu Nyerere kilichopo Kigamboni.
Mwenyekiti wa uchaguzi huo, Rachel Mhando amesema jumla ya kura zilizopigwa ni 15 na moja iliharibika.
Mhando ambaye ni Katibu Tawala wa Kigamboni, amesema nafasi ya naibu meya imekwenda kwa Amin Sambo kutoka CCM aliyemshinda Ernest Mafimbo wa CUF chini ya Ukawa.