CCM yashinda Umeya Kigamboni

CCM yashinda Umeya Kigamboni

a070577b9140fae753a5b0f6634f3754.jpg
 
picccm+yashinda.jpg

Meya mpya wa Kigamboni Maabadi Hoja (katikati) akizungumza na wanahabari baada ya kuchaguliwa leo kulia ni Naibu meya Amin Sambo na kushoto ni Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo Steven Katembo. Picha na Bakari Kiango

Kwa ufupi
  • Uchaguzi huo umefanyika leo (Jumamosi )katika Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Julisu Nyerere kilichopo Kigamboni.
  • Mwenyekiti wa uchaguzi huo, Rachel Mhando amesema jumla ya kura zilizopigwa ni 15 na moja iliharibika.
By Bakari Kiango, Mwananchi bkiango@mwananchi.co.tz
Dar es Salaam. Diwani wa Kata ya Pemba Mnazi (CCM), Maabadi Hoja ameshinda umeya wa Halmashauri mpya ya Kigamboni baada ya kupata kura tisa dhidi ya tano za Celestine Maufi wa Chadema.

Uchaguzi huo umefanyika leo (Jumamosi )katika Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Julisu Nyerere kilichopo Kigamboni.

Mwenyekiti wa uchaguzi huo, Rachel Mhando amesema jumla ya kura zilizopigwa ni 15 na moja iliharibika.

Mhando ambaye ni Katibu Tawala wa Kigamboni, amesema nafasi ya naibu meya imekwenda kwa Amin Sambo kutoka CCM aliyemshinda Ernest Mafimbo wa CUF chini ya Ukawa.

Chanzo: Mwananchi
Pamoja na kupambana bado tu hujakumbukwa kwenye uteuzi?
 
Hamna anayehangaika na mafisadi chadema kwa sasa.

Hasa hiki kitendo Cha Mbowe kwenda ulaya kutoa hotuba za kuichafua nchi kimewaudhi sana watanzania.

2020 wajiandae kupungua bungeni.
 
Hivi wale walio wanyiwa utafiti na NMRI na kuthibitika kuwa wana virus vya ZIKA si wanaweza kupatikana ili kuondoa hii sintofahamu ya kutenguliwa kwa Dr.Mwele au ni ngumu kupatikana?
 
Diwani wa Kata ya Pemba Mnazi (CCM), Maabadi Hoja ameshinda umeya wa Halmashauri mpya ya Kigamboni baada ya kupata kura tisa dhidi ya tano za Celestine Maufi wa Chadema.

Uchaguzi huo umefanyika leo (Jumamosi )katika Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Julisu Nyerere kilichopo Kigamboni.

Mwenyekiti wa uchaguzi huo, Rachel Mhando amesema jumla ya kura zilizopigwa ni 15 na moja iliharibika.

Mhando ambaye ni Katibu Tawala wa Kigamboni, amesema nafasi ya naibu meya imekwenda kwa Amin Sambo kutoka CCM aliyemshinda Ernest Mafimbo wa CUF chini ya Ukawa.
Sasa uchaguzi WA Meya wa jiji urudiwe ili halmashauri mpya zipate fursa ya kuchagua Meya!!
 
ila waandish wa habar kwel makanjanja,m2 anakunyima uhuru wa habar lkn bado unamwandikia matukio yake,kwa nn na we2 usimchunie il aone umuhm wake? anakuja m2 anasema atashirikiana na wanababar inaingia akilin kwel? waandish wa habar dawa ya moto n moto au njaa kal kitaa?
 
Wameshinda kwa kura au wamejipa ushindi fisiemu
 
Jambo moja tu huwa nawashanga CCM na Serikali /DED; pale ambapo wanajua watashinda, husikii wala kuona mizengwe kutoka CCM na Mkurugenzi wa Halmashauri. Kimbembe huwa pale ambapo hesabu zao zinagoma, yaani Mkurugenzi, CCM, na hata Polisi hutengeneza mazingira ya tension kama vile tuko Ethiopia au Eritrea! Mbona wapinzani wao wakijiona wachache kwa kura huwa hatushuhudii vurugu na mizengwe?

Vv
 
Wakati mwingine ficha ujinga wako mbele za wengine. Ccm walikuwa wajumbe 9 na ukawa 5 nipe kigezo cha ccm kushindwa au ni kwanini ukawa hawakushinda? Hesabu ndogo hizo zinakutesa na unakuja kifua mbele kujisifu na kusifia ujinga.
Kama Ukawa wangekuwa na wajumbe wengi kuliko CCM ungeshuhudia vurugu na mizengwe ya ajabu, wangejazwa Polisi na FFU kama vile kuna tukio la ujambazi.

Vv
 
Watu wanangalia chama badala ya uwezo.huyo diwani wa Ukawa ndio think tank ya halmashauri,kuanzia kwa mkurugenzi mpaka madiwani,halafu wamempiga chini
sure, hili ndo janga tulilonalo watanzania. ccm, chadema, cuf wote wanaangalia vyma bila kujali mtu. tusingekuwa tunajali vyama kusingekuwepo na figisu za kukodi wabunge wa viti maalum kuja kupiga kura
 
Diwani wa Kata ya Pemba Mnazi (CCM), Maabadi Hoja ameshinda umeya wa Halmashauri mpya ya Kigamboni baada ya kupata kura tisa dhidi ya tano za Celestine Maufi wa Chadema.

Uchaguzi huo umefanyika leo (Jumamosi )katika Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Julisu Nyerere kilichopo Kigamboni.

Mwenyekiti wa uchaguzi huo, Rachel Mhando amesema jumla ya kura zilizopigwa ni 15 na moja iliharibika.

Mhando ambaye ni Katibu Tawala wa Kigamboni, amesema nafasi ya naibu meya imekwenda kwa Amin Sambo kutoka CCM aliyemshinda Ernest Mafimbo wa CUF chini ya Ukawa.
Sawa
 
Back
Top Bottom