General Mangi
JF-Expert Member
- Dec 21, 2013
- 15,303
- 23,055
Hakika naona sasa CCM wanashikana mashati, hawajui wafanyee nini.
Wajumbe wa kamati kuu wahoji uhalali wa naibu spika kuingia kikao cha kamati kuu kinyume cha taratibu na kanuni za chama.
Katiba inasema Spika wa bunge atakuwa mjumbe wa kamati kuu ya chama, na haisemi kwamba kama spika hatokuwepo basi awakilishwe na Naibu spika
Sote tunajua spika Ndugai yupo kwenye matibabu India, hakuwepo kwenye kikao cha kamati kuu juzi. Lakini cha kushangaza Naibu spika, Tulia akahudhiria kama kumwakilisha spika, jambo ambalo ni kinyume na taratibu za chama, kwani hakuna kanuni inayotamka hivyo.
Hakuna mjumbe yoyote wa kamati kuu atawakilishwa na mtu mwingine kama yeye hatokuwepo.
Jambo hili limemkera kikwete, kiasi kwamba hata wajumbe wa kamati kuu kuhoji inakuaje rais anaingilia utendaji wa chama?
Katika kikao hicho Magufuli wala Shein hakuwepo.