CCM yapoteza Wenyeviti wa mitaa Mbeya; wahamia CHADEMA

EasyFit

JF-Expert Member
Jul 4, 2011
1,269
1,082
WENYEVITI wa mitaa ya Ilemi na Ilolo Kati, Wilaya ya Mbeya Mjini wa Chama cha Mapinduzi (CCM), wamejiunga na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA).

Wanasiasa hao Ngamba Ngamba wa Ilolo Kati na Joseph Mbele wa Ilemi, walirudisha kadi za CCM na kujiunga na CHADEMA jana katika mkutano uliofanyika katika Kata ya Sinde jijini hapa.

Mbali na wenyeviti hao makada wengine watatu wa chama hicho akiwamo Atusekelege Asubisye, ambaye ni balozi katika Mtaa wa Ilolo Kati nao walijiunga na CHADEMA, kwa kile walichodai ni kuchoshwa na CCM yenye ahadi nyingi zisizotekelezeka.
 
Mbeya, Mwanza, Kilimanjaro, Arusha..
Hii ndio mikoa pekee inayoifahamu taasisi wa Wakr...., na wakask...(CDM) hapa tanzania
 
Mbeya, Mwanza, Kilimanjaro, Arusha..
Hii ndio mikoa pekee inayoifahamu taasisi wa Wakr...., na wakask...(CDM) hapa tanzania

kaka unawashwa na kanzu la udini,nyie ndo wale mnaotaka kupiga sarakasi huku mmevaa taulo.shame on you.
 
Mbeya, Mwanza, Kilimanjaro, Arusha..
Hii ndio mikoa pekee inayoifahamu taasisi wa Wakr...., na wakask...(CDM) hapa tanzania

Umesahau taasisi ya wauza 'unga' inayaongozwa na ridh1 wa ikulu...
 
Na nyie chadema kueni makini na hawa watu wanaohamia kwenu from ccm, msije na nyie mkawa CCM part 2 mkaanza kujaza na kutunza mafisadi
 
Mbeya, Mwanza, Kilimanjaro, Arusha..
Hii ndio mikoa pekee inayoifahamu taasisi wa Wakr...., na wakask...(CDM) hapa tanzania



Gamba tumwa at work!

Rejao kuwa na akili ya kutambua alama ya nyakati!
Utakuja acha na ukakosa mbele wala nyuma!

Haujakosa wa kukuambia lakini!
TUSILAUMIANE TAFADHALI Rejao!
 
Mbeya, Mwanza, Kilimanjaro, Arusha..
Hii ndio mikoa pekee inayoifahamu taasisi wa Wakr...., na wakask...(CDM) hapa tanzania
Lakini hauoni taasisi hiyo ya kikristo ndiyo heartbeat ya nchi na ndiko kura za tz zinakotoka? Ushindwe na uchochezi wako wa kidini!
 
kaka unawashwa na kanzu la udini,nyie ndo wale mnaotaka kupiga sarakasi huku mmevaa taulo.shame on you.

Amini Amini kaka,dhambi ya udini ambayo wanaitumia wanamagamba ndiyo watakaozikwa nayo,walianza na ooh cuf ya waislam yakawashinda,chadema ya wakatoriki yakawashinda,sasa chadema ya wakristu,bila shaka yatawashinda kwa sababu dhambi hii waliyo nayo ccm ni sawa na kula nyama ya mtu,hawataiacha.Hata hivyo si vibaya kujikumbusha kwamba ndani ya vyama vyote kuna wanachama wenye dini na wasio na dini pia,je ccm hawayaoni haya kwao?Fuatilieni hili hapa'matokeo ya urais 2000,2005 na 2010' Bara na visiwani kisha tupime udini ulikuwa kwa chama gani?WATU WALIO OGOPA UMANDE HAPA TZ WENGI NI WA CCM.
 
Anayeleta mambo ya udini hana akili' sisi kwetu ni kanjanja kama alivyosema mwenyekiti wao wa chama cha magamba' chichiemu.
 
Tunawakaribisha ila tuwe nao makini maana ccm huwa inamchezo wakuingiza hata mamluki ili waje kuharibu chama
 
Sasa jana Vwawa mjini Mbozi wanachama kibao wa magamba wamerudisha kadi za ccm pamoja na bendera na kukabidhiwa kadi za cdm. Kigogo wao mkubwa mama alie kuwa anshikilia nyazifa kibao za magamba hadi ngazi ya taifa nae amebwaga manyanga. Hakika CDM inakubalika.
 
Sombasomba inaipiga CCM, na soon itamsomba waziri mkuu
220px-Hurricane_Katrina_August_28_2005_NASA.jpg
Animated_hurricane.gif
 
Mbeya, Mwanza, Kilimanjaro, Arusha..
Hii ndio mikoa pekee inayoifahamu taasisi wa Wakr...., na wakask...(CDM) hapa tanzania
Sio hiyo tu bro, ni Mbeya, Ruvuma, Iringa, sumbawanga, Kigoma, Mwanza, Mara, Arusha, Kilimanjaro, Dar, Morogoro, Manyara, Shinyanga yote ni CDM. Tabora, Kagera, Dodoma ni CCM. Zanzibar, Pemba, Mtwara, Lindi na Tanga ni CUF na CCM japo wote wanazidi kupoteza mvuto. Nadhani mpaka Dec 2014 tutakuwa tumepata picha kamili ya strongness ya kila chama katika eneo husika.
 
Back
Top Bottom