EasyFit
JF-Expert Member
- Jul 4, 2011
- 1,269
- 1,082
WENYEVITI wa mitaa ya Ilemi na Ilolo Kati, Wilaya ya Mbeya Mjini wa Chama cha Mapinduzi (CCM), wamejiunga na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA).
Wanasiasa hao Ngamba Ngamba wa Ilolo Kati na Joseph Mbele wa Ilemi, walirudisha kadi za CCM na kujiunga na CHADEMA jana katika mkutano uliofanyika katika Kata ya Sinde jijini hapa.
Mbali na wenyeviti hao makada wengine watatu wa chama hicho akiwamo Atusekelege Asubisye, ambaye ni balozi katika Mtaa wa Ilolo Kati nao walijiunga na CHADEMA, kwa kile walichodai ni kuchoshwa na CCM yenye ahadi nyingi zisizotekelezeka.