CCM yapokea mamluki huku ikidanganywa kuwa ni vigogo wa CHADEMA

Apr 9, 2011
38
3
CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Wilaya ya Tanga kimewashukia viongozi wake waliohamia Chama Cha Mapinduzi (CCM) na kusema kuwa ni waroho wa madaraka.
Akizungumza katika mkutano wa hadhara katibu wa chama hicho Khalid Rashid, amemponda aliyekuwa Mwenyekiti wa CHADEMA Wilaya ya Tanga, Mohamed Waziri Kinomina na wenzake waliokihama chama hicho na kuhamia CCM.
Kadhalika amewaponda kwa kudanganya nyadhifa walizokuwa wakishikilia ndani ya chama hicho huku mmoja wao akidai kuwa alikuwa ni mwenezi wa chama hicho Wilaya ya Tanga, ambao hivi karibuni walihama CHADEMA kwa kile walichodai kuwa kimetawaliwa na udini na ukabila.
Katibu huyo alidai kuwa mwenyekiti huyo wa zamani wa CHADEMA wa Wilaya ya Tanga, Kinomi na wenzake, Aufi Kidege ni waroho wa madaraka na kamwe CHADEMA haitakubali kukumbatia watu ambao wanaifuata kwa masilahi yao binafsi badala ya kuangalia matatizo ya wananchi.
“CCM wamedanganywa nao wanakubali eti wamepokea vigogo kutoka CHADEMA, nani kigogo? Mohamed Waziri Kinomi kwetu si kitu na tuliliona hilo mapema, anahama kila chama, CCM kama hawajui hakutoka CHADEMA tu alianzia vyama vingine na kote huko anatafuta madaraka tu na si kingine,” alisema.
Aliongeza kuwa CHADEMA ipo kwa lengo la kuwatumikia wananchi na si kushughulikia masuala ambayo ni ya kibinafsi.
 
Kuwa mwanachama CDM siyo lelemama,huku kunahitaji watu wanaotumia akiri,wenye kuwajibika kwa wananchi na si kwa nyumba ndogo wala kwa matumbo yao

sasa hatuzuii mtu kuja CDM lakini kama ulikuja kwa bahati mbaya ni lazima utaondoka maana huku hatuna pilau,usafiri wala 10,000,na kamwe CDM si nyumba ya nyoka,nyoka wenye magamba,wenye kutema sumu,wanaopondwa vichwa!
 
CDM isisite kuwafukuza watu wote wanaojiunga na chama kwa malengo ya kujinufaisha wao binafsi badala ya kukinufaisha chama
 
Kuwa mwanachama CDM siyo lelemama,huku kunahitaji watu wanaotumia akiri,wenye kuwajibika kwa wananchi na si kwa nyumba ndogo wala kwa matumbo yao

sasa hatuzuii mtu kuja CDM lakini kama ulikuja kwa bahati mbaya ni lazima utaondoka maana huku hatuna pilau,usafiri wala 10,000,na kamwe CDM si nyumba ya nyoka,nyoka wenye magamba,wenye kutema sumu,wanaopondwa vichwa!

Maneno yako mazito baada ya wewe kusema mie sina la kuongeza maana umesema vyema .
 
Kuwa mwanachama CDM siyo lelemama,huku kunahitaji watu wanaotumia akiri,wenye kuwajibika kwa wananchi na si kwa nyumba ndogo wala kwa matumbo yao

sasa hatuzuii mtu kuja CDM lakini kama ulikuja kwa bahati mbaya ni lazima utaondoka maana huku hatuna pilau,usafiri wala 10,000,na kamwe CDM si nyumba ya nyoka,nyoka wenye magamba,wenye kutema sumu,wanaopondwa vichwa!

Kuzomea na Kuandamana kuna hitaji akili?
 
CHADEMA siyo pipi ya kulamba na kuyeyuka kama wazee wa magamba wanavyodhani, huku ni kazi tuuu!!!!
 
Kuzomea na Kuandamana kuna hitaji akili?

Hata kidogo haihitajiki.
Unahitaji akili nyingi sana kubuni mbinu nyingi za kutumia madaraka yako kuhujumu nchi kwa maslahi binafsi Kama Kubuni EPA, Stimulus package, Radar, Twin Tower, Richmond/Dowans/Symbion....
endelea..
 
Hakuhitaji akili bali kuvuana magamba lazima uwe na PhD za kupewa.

Hujakosea maana sisi tunasubili hizo siku 90 zifike hapo ndo watajua kweli kuvuana magamba kunahitaji akili na hizo tarehe walizoanza kuzihesabu mimi nazikumbuka sana kwani ilikuwa trh 10 april
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom